Rais wangu Magufuli songa mbele. Wengi tunakusasapoti.
Tunafahamu ili nchi hii ijengwe tunapaswa tuumie kwanza. Kwa mfano, mwaka huu watu wamechapa kazi kweli. Huko vijijini hata waliokataa kulima miaka ya nyuma mwaka huu wamelima. Maana hukupenda siasa. Umewaambia watu serikali haina shamba. Wasipolima watakufa. Hiyo ilikuwa safi sana. Zamani walikuwa wanaambiwa serikali iko na chakula cha kutosha.
Nchi za Ulaya waliumia kwa kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi na sasa hawataki kutuona tukienda kufaidi matunda yao.
Wamarekani hata sasa wanaendelea kuumia kwa kulipa kodi nyingi kugharamia jeshi na huduma za jamii. Leo hii wameweka conditions ngumu kuingia kwao. Kuingia Marekani ni mchakato bali kuingia Tanzania ni ishu ndogo sana. Hawataki kuona mtu anafaidi matunda yao. Leo hii waafrika wengi tunataka tuende marekani na Ulaya kufaidi matunda ya uchumi watu tusiyoujenga. Mgeni yeyote kwa marekani na wait wa ulaya ni kama adui.
South Africa wamehangaika kutafuta uhuru wao kwa jasho na sasa hawatutaki.
Tumuunge mkono Rais wetu Magufuli katika kujenga nchi yetu. Tukubari kuumia kwa muda.
NB: Nikiwa Kama mwanaccm sioni haja ya rais wangu kuendelea kuwakumbatia Gambo na Makonda. Kazi unazofanya mh. Rais zinaonekana. Wanachofanya hawa watu wawili ni ujinga na umbumbumbu. Kura zetu hazitaongezeka kwa kuwachukia wapinzani. Kura zetu zitaongezeka kwa kufanya maendeleo. Maendeleo yanayofanywa chini ya serikali ya awamu ya tano yanaonekana na watu wote.
Kisha mh. Rais huyu Makonda ndiyo yuko na matatizo makubwa kuliko. Ningekuwa ni mm ningeonyesha cheti au ningejihudhuru tu.
Mwisho mh. Rais uhakiki uliofanywa bado hauko fair. Viongozi wote wa kiserikali isipokuwa wabunge wakaguriwe na kupewa adhabu stahiki.