Habari za wazalendo wote walio ndani na nje ya Tanzania,
Lengo la uzi huu ni kumpongeza magufuli tu kwa mazuri anayofanya,
Mchangiaji kama umeguswa na Jambo lolote ambalo kafanya liandike na utoe pongezi,
Tunajua Ana mabaya yake, lakin we waweza ona ni baya mwingine akaona ni zuri,
Kwanza kama umependa uzi huu "like" then comment,
Tujikumbushe kidogo kulaumiwa kwa viongozi ni Jambo la kawaida hasa kwa watanzania wanafiki hasa wa kwenye mitandao,
Naanza kwa kuwasihi magufuli na serikali yake pia na ndugai na bunge lake ,hata waliopita walisemwa sana , lakin cha kushangaza mda huu wanashangiliwa,
Hizi comments chini ni za mwaka 2008
Pitia uone walivyomnanga kikwete na Samweli sitta, Leo hii wanajifanya kuwakumbuka
Walianza kufanya biashara Ikulu kama vile ni mradi wa Kuku, wakagawiana fedha za BoT kama vile wanagawana njugu, sasa wamefikia mahali kuwa Spika hamuamini Naibu wake, na haamini kuwa Bunge linaweza kufanya shughuli zake pasipo yeye. Kwa mtetezi wa lugha nzuri Bungeni, Spika Sitta amemdhalilisha sana na kumshushia heshima Naibu wake kwa kumuona kuwa hana uwezo wa kuamua nini jambo la muhimu na ni nini kinaweza kujadiliwa. Kwa kusema Naibu Supika asije "kukurupuka" Mzee Sitta hana budi kuliomba radhi Bunge kwa matumizi ya lugha ya kibabe, kizandiki na yenye mlengo wa unyanyasaji wa kijinsia.
Na sipendi Spika ajifanya ana Bunge mfukoni. Ni wazi kuwa suala la Richmond na BoT siyo suala muhimu sana kwa Taifa ukilinganisha na ziara yake ya "kuliwezesha Bunge". Kwani kama masuala hayo yangekuwa muhimu angebadilishana nafasi ya kumpa Bi. Makinda ziara na yeye (kama alivyosema mtu mwingine hapa) abakie kusimamia mambo haya.
But then, akifanya hivyo atakiumbua chama chake na utii wake ni kwa CCM.
Weka comment yako juu ya magufuli unampongeza kwa lipi na u like thread,
Kwa upande wangu nampongeza kwa haya,
1. Kurudisha heshima kwa umma hasa watumishi
2. Ununuzi wa ndege mpya
3. Ujenzi wa miundombinu mbali mbali nchini (DSM based)
4. Kupunguza rushwa ,si kama nyuma
5. Elimu bila malipo kwa secondary hadi kidato cha sita,.
6. Uhuru wa vyombo vya habari mpaka sasa tupo tunamchambua
7. Kuzuia rasili Mali zetu zisiibiwe,
Kwakweli kafanya mengi,
Mods naomba uzi huu msiuondoe wala kuunganisha maana maudhuhi yake ni kusifu tu, si kama nyuzi Nyingine