The Stig
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,113
- 1,105
Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015 Rais Magufuli kwa maoni ya watanzania wengi walimpa nafasi ndogo ya kuwa mgombea urais kupitia CCM hata yeye mwenyewe aliwahi kukiri ali beep na ikaiitikia.
Kwa muda wa utawala wake Mheshimiwa Rais Magufuli amefanya mambo ambayo nina uhakika hakuna mgombea yeyote ndani ya CCM na nje ya CCM angeweza kufanya.
Ninaposema Rais Magufuli ni chaguo la Mungu ni kuwa taifa linapozidi Ufisadi na Dhuluma mwenyezi mungu huleta kiongozi kama Rais Magufuli ili aje kuondoa hiyo dhuluma na ufisadi kwenye ardhi ya Tanzania.
Madhambi yakipungua mwenyezi mungu hushusha neema leo sehemu nyingi mfumko wa bei ya chakula umeshuka kwa kiasi kikubwa.
Mheshimiwa Rais Magufuli wewe chapa kazi na ufahamu kuwa Mwenyezi Mungu yupo nyuma yako hawa wanaojiita watetezi wa Demokrasia walikuwa wanaipeleka nchi hii kubaya sana.
Haya tena. Mleta mada ni mtaalam mwingine tena anayedandia basi kwa mbele. Kadhri siku zinavyoenda, udandiaji wa namna hii umetumika kuwavusha wengi na hata kupelekea wadandiaji kadhaa kupata teuzi kubwa kubwa.
Nakutakia uteuzi mwema. Ila ngoja tueleze uhalisia ili angalau taifa lisiwe duwanzi moja kwa moja.
Iukua kwa uchumi hakupimwi kwa kuteremka mfumuko wa bei pekee. Ni lazima uangalie na indicator nyingine, hususan kukua kwa pato la taifa kwa kichwa (GDP per capita). Tanzania tulifikia gdp pc ya juu kabisa mwaka 2013, ambapo ukubwa wa uchumi ulimaanisha kila mtanzania anazalisha wastani wa usd 902 kwa mwaka. Tulibakiza usd 100 tu kufikia kiwango cha uchumi wa kati, yaani usd 1,005 kwa mwaka. Leo hii gdp pc imeshuka mpaka usd 810, na inaendelea kuporomoka kwa sababu kasi ya ukuwaji wa uchumi uko chini kufuatia uwekezaji kupungua na biashara kufungwa.
Kupungua kwa bei ya vitu inaweza ikatokea kufuatia uchumi kupormoka, kwani mzunguko wa hela unakuwa pungufu kuliko huduma zinazozalishwa katika eneo. Watoa uuduma wanapunguza bei ili angalau wapate chochote, lakini katika kufanya hivyo, wanakuwa hawapati faida linganifu na juuudi zao na mwisho wanafunga biashara. Hii inapelekea uchumi kuendelea kusinyaa mpaka huduma zinazotelewa zilingane na mzunguko uliopo. Nilishangaa sana siku nilisikia mwanasiasa anasifia mapango ya nyumba kupungua... ni dalili ya kutoelewa mambo. Kati ya viashiria vikubwa kabisa ya uchumi kusinyaa, ni kupungua kwa bei za nyumba, ikiwapo na bei ya pango.