mbikagani
JF-Expert Member
- Dec 5, 2014
- 3,107
- 1,782
Mwanaume mwenye akili za kisayansi hawezi msifia mtu hivi.
Acha na akiba ya maneno.
Acha na akiba ya maneno.
*JPM NI ZAIDI YA TUMJUAVYO*
Niungane na *Watanzania* Wengi kwanza Kumshukuru Mungu kwa Kutuinulia *Ndugu John Pombe Magufuli,* kama *Mwenyekiti* wa *CCM* Taifa, Sidhani kama katika Wakati Huu tunaweza Kuwa na *Mtu* wa Aina yake, Wengi wananielewa *ninachomanisha.*
*TATU BOMBA*
Katika Maisha ya *Siasa* nimejifunza kuwa *UZOEFU* ni Muhimu, lakini Hauwezi kuzidi *Ubunifu* , *Uweledi,* *Uthubutu* na *Utashi* wa *Kisiasa.*
Ingizo la *Ndugu Mizengo Peter Pinda* waziri Mkuu Mstaafu, na *Ndugu Makongoro Nyerere* sikuelewa Vizuri, ila alipopendekeza Jina la *Ndugu Dkt. Bashiru Ally Kakurwa* kuwa Katibu Mkuu wa *CCM* nilielewa huu utatu mtakatifu.
*KWANINI HAWA WATATU*
Tuanze na *Ndugu Pinda* , ukitazama viongozi wakuu wenye *Umri,* uzoefu na uadilifu ambae mienendo yake hata baada ya kumaliza kazi ya *Uwaziri Mkuu* utakubaliana na mimi kuwa Ndugu *Pinda* ni ingizo Sahihi ukiwaacha Marais wastafu, sisemi ni *Bora* kuliko wengine lakini *Haiba* yake inahitajika zaidi katika kushikilia *Dhana* ya Uzoefu kwenye *Chama* na *Serikali,* Uwepo wake utaisaidia CCM kwa miaka 10 ijayo.
*Ndugu Makongoro Nyerere*, wengi bado wanauliza Kaingia kufanya nini? Kwa wanaomjua *Makongoro* katika Siasa za *UDAMBWIUDAMBWI*, kama hunielewi Jiulize Kwanini Ndugu Wasira bado ana Nguvu kwenye CCM japo alikosa Ubunge kule Bunda, Sina maneno ya kuwaelezea hawa watu ila itoshe kusema kuwa *CCM* inahitaji watu wa Aina ya *Makongoro* ambao Wamezaliwa na kukulia ndani ya Misingi ya Chama cha *Mapinduzi*.
*UJIO WA DKT. BASHIRU CCM*
Ndugu *Magufuli* kama Ni kwenye Mpira wa Miguu amemudu kuucheza na kumaliza Dk 90 akiwa *Nyota* wa mchezo.
Ujio wa Dkt. Bashiru kama Katibu Mkuu wa CCM unasadifu Mambo Muhimu yafuatayo :-
1. Chama kimeanza kujenga safu ya Utendaji wa watu wenye *Uweledi wa Modern Politics* siasa za kisasa zinazohitaji Hoja na Sio kelele, *Dkt. Bashiru* kama wengi wakivyosema wamefundishwa nae Siasa pale Udsm na mimi nikiwa Mmoja wapo *2003-2006* , mbali na kuwa mwalimu wa Sayansi ya Siasa jambo zuri ni kuwa yeye ni Muumini wa Siasa za kumkomboa mtu Mweusi katika *Umajumui* wa Maendeleo.
*CCM* imeanza Kurudisha *Misingi* ya kuanzishwa kwake chama cha *Wakulima* na *Wafanyakazi* (hapa kwa Wafanyakazi ni pamoja na wafanyabiashara au mtu anaefanya kazi halali ya kumuingizia kipato) ambacho kinaanza Kuwavutia *Wasomi* wa Kati, kawaida na wale wa kiwango cha Juu.
2. Ccm Inaanza kuonekana kwa vitendo kuwa ni chama Cha *Wote* ili mradi uwe na Uweledi na Maarifa ya *Kuongoza,* haijalishi ulikuwa Nani Ccm Utapata fursa ya kusimama na Kuongoza, Hili limetimia kwa Dkt. Bashiru ambae mimi nimemjua mwaka 1998 akiwa mwenyekiti wa Tawi la Ccm *Abiyani* pale Ubungo, na zaidi ya Hapo wengi wamekuja kumuona akiwa Mwenyekiti wa Tume ya kuhakiki Mali za *CCM* , hakuwa mtu maarufu au *Mashuhuri* ndani ya *CCM*
Hii ni *Karata* nzuri katika Kuwaaminisha wananchi kuwa *Ccm* sio mali ya mtu au kikundi fulani Bali ni *Bidii* na maarifa yako tu, sasa naamini watu ambao ni *Wasomi* watagombea nafasi ndogo na za kawaida mfano kata z matawi, Wilaya na Mkoa.
3. Ujio wa *Dkt. Bashiru* unatoa fursa ya kuanza kushughulikia tatizo *SUGU* la matumizi mabaya ya *RASILIMALI* za Chama, yeye amezunguka Karibu nchi nzima ameona chama kikoje na kina nini, katika siasa za sasa suala la kujiimarisha *KIUCHUMI* ndio Agenda kubwa ambayo itaendelea kuleta Uhai wa chama mana uko mbeleni naona kila dalili ya kuondolewa au kupunguzwa kwa *Ruzuku* kwa Vyama vya Siasa mana zinatafunwa tu kama fedha za Capacity Charge kwa IPTL, Songas na Richmond.
*HITIMISHO*
Naomba nihitimishe kwa Kuwatazama watu wawili wakubwa kwanza ni Wana CCM wenzangu, na pili *Dkt. Bashiru*
Ndugu zangu wana CCM Tumepata Katibu Mkuu Mweledi, Mbunifu na Msomi najua wako *Majeruhi* baadhi waliofisadi Mali za chama najua hawa hawatamtaka kabisa Dkt. Bashiru watamkwamisha kila kona na *kumuhujumu* , mimi nasema hao mafisadi ni wachache sisi wanachama ni wengi hivyo mkae kimya kwa sasa muacheni *Katibu Mkuu* mpya afanye kazi, najua mtaibuka na *Agenda* zenu mfu kuwa Hakijui chama na Sio mzoefu, ila mjue siasa zimebadilika sasa ni siasa za hoja na Sio *Matusi* au kushambuliana, lakini mwenyekiti alishasema anataka kujenga *Ccm* mpya ndio hii sasa.
Kwako *Dkt. Bashiru,* wewe kwangu ulikuwa *Mwalimu* tuliona misimamo yako, *hukuogopa* na tunaamini uku utaendeleza zaidi.
Yako Mambo Mazuri unapaswa kujifunza kutoka kwa Mtangulizi wako *Ndugu Kinana,* yeye alikuwa kama *Kisima Jangwani* chukua *Mazuri* yake, endeleza pale alipoishia ila kubwa Endelea *Kujenga Umoja* , *Mshikamano,* *UTII* na *uadilifu* kwa Chama na wanachama, Wasaidie wenzako kufanya vizuri, na wale wanaofanya vizuri waendeleze *wafanye vizuri zaidi na zaidi* , Naamini katika Wewe, tutamuona *Mwalimu Nyerere* kwenye Chama, mana tumeshamuona Serikalini kupitia *Dkt. John Pombe Magufuli.*
Jua pia kuna *wanafiki* Wachache sana japo wana *Vinguvu* kwa Kiwango cha *PhD*
*Usiyumbe Wala Kuyumbishwa*
Wako katika Uzalendo
*Jerry C. Muro*