Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Tuna rais kichaa na mawaziri vichaa.

Dah! Tanzania ya viwanda.
 
Eideed,

..sera za uchumi za Mwalimu na Sokoine zilifeli.

..Sasa badala ya wao kukubali kuwajibika, walitafuta KISINGIZIO.

..kisingizio ilikuwa uchumi wetu umeporoshwa na WAHUJUMU UCHUMI na WALANGUZI.

..Lakini ukweli ni kwamba Walanguzi na hao walioitwa Wahujumu Uchumi walikuwa ni matokeo ya sera uchumi zilizoshindwa na siyo chanzo.

..Mwalimu Nyerere na Sokoine waliunda mahakama ya wahujumu uchumi.

..Lakini watuhumiwa wengi waliofikishwa ktk mahakama hiyo walikuwa wamekamatwa na kusota mahabusu kabla bunge halijapitisha sheria ya uhujumu uchumi.

..Tawala zinazozingatia haki za binaadamu na utawala bora, hupitisha kwanza sheria, halafu baada ya hapo hukamata wale watakaovunja sheria hiyo.

..Kipindi ambacho Sokoine alikuwa Waziri Mkuu hali ya uchumi na maisha kwa ujumla ilikuwa ngumu kuliko kipindi chochote kile ninachokikumbuka mimi.

..Watanzania wa leo hawawezi kuvumilia shida tulizovumilia sisi wakati wa Sokoine.

Cc chige, Pascal Mayalla
Mkuu kumbuka ufisadi uliofanyika katika kipindi cha awamu ya tatu na nne ulikuwa wa kutisha na CCM iligeuka kuwa chama cha watu wenye maslahi maalum binafsi. Makundi yenye nia mbaya yalijengeka hata kufukia kutaka kuingia Ikulu kwa njia yeyote. Rais Magufuli kama binadamu anaweza kukosea lakini tuangalie mazuri mangapi anayoyafanya.
 
Mkuu JokaKuu,

Kwanza nianze ni mada ya Eideed kuhusu ujasiri wa JPM katika kupambana na ufisadi!

Niliwahi kuhoji hapo kabla na hapa nitarudia! Je, JPM "anapambana" na ufisadi kwa maslahi ya nani hasa? Ni kwamba anapambana kwa maslahi ya utawala wake TU ili aache legacy au anapambana kwa maslahi ya taifa?

Kama anapambana kwa nia ya kuacha legacy TU na si vinginevyo, well and good! Hapa atapata wengi wa kuusifia utawala wake mara atakapoondoka madarakani! Zile simulizi za akina Sokoine bila shaka zitamhusu pia JPM!

Inawezekana mimi ni jitu roho mbaya lenye husuda na chuki tele dhidi ya JPM! AS FOR NOW, mimi si miongoni mwa wale watakaomsifia JPM katika hili! Sitamsfia kwa sababu hadi sasa naona JPM ana-target sana only one side of the corruption equation!

Ili ufisadi mkubwa (Grand Corruption ) uweze kufanyika... two parts have to complete the corruption equation. Pande hizo ni upande wa wafanyabiashara (and the like) na upande wa watendaji wakuu wa serikali na/au high profile politicians! Hizi ndizo pande mbili zinazounda corruption equation.

Tangu aingie madarakani, JPM anaonekana sana ku-target upande wa wafanyabiashara huku akiacha kabisa upande wa high profile politicians and/or top government officials!

Yaani ni kama anatuambia yule Rugemalila na mwenzake walienda na vifaru pale BoT na kubeba ile minoti bila uhusika wa watendaji wakuu na/au wanasiasa!

Yaani ni kama anatuambia yule Said Lugumi ufisadi alioufanya pale Mambo ya Ndani aliufanya bila msaada wa mkubwa yeyote!!

Na ndio maana haishangazi kuona wakati Ruge na mwenzake wapo mahabusu (for show?), wale waliofanikisha Ruge na Seith kuchota yale mabilioni wanadunda tu mitaani huku JPM akiogopa hata kuwataja!!! Na ndio maana hadi leo wala hatufahamu ni nani walihusika kumpa Said Lugumi mkataba wa mabilioni ya pesa kisha wakamlipa 99% huku kazi ikiwa hajaifanyika kwa miaka kadhaa sasa!!

Huyo hapo juu ndie JPM anayetaka kuaminisha Watanzania kwamba anapambana na ufisadi! Kwamba, kumbe Watendaji Wakuu na Wanasiasa nchi hii hawafanyi kabisa ufisadi na hao akina Manji wamekuwa wakifanya ufisadi bila kushirkiana na kiongozi yeyote yule!!!

SORRY... sina cha kumsifia kiongozi kama huyo! Isitoshe, mimi kama mwananchi sina mkataba na akina Manji au Rugemarila! Mkataba wangu ni na wanasiasa pamoja na watendaji wa serikali wanaolipwa kwa kodi zangu! Hawa ndio hasa nilitarajia wawe wa kwanza kuchukuliwa hatua kwenye masuala ya ufisadi kabla ya hata hao akina Rugemarila!!!!

Huwezi kupambana na ufisadi wakati unawafumbia macho Wanasiasa na Watendaji Wakuu wa serikali na idara/taasisi zake! Ni hawa ndio wanafanikisha grand corruption!! Ni hawa ndio ambao Malcom Lumumba aliwataja kama sehemu ya wahusika wakuu wa utakatashaji pesa!

REMEMBER, hapo juu nilihoji ikiwa JPM anapambana na ufisadi kwa maslahi yake binafsi ili hatimae aache legacy kwa wale wanaosifia kila kitu au "anapambana" kwa maslahi ya taifa!

Nimeshasema hata kama anafanya just for a legacy, kwangu, at least for now, sioni cha kumsifia kwa sababu wala haielekei kama anapambana na another side of the corruption equation ! Na kama kipo basi wala hakina value ya kumtengenezea legacy!

What about kupambana na ufisadi kwa maslahi ya taifa?!

I hate to say this but hata hapa napo, he's COMPLETELY FAILURE to the point wala sipati shida ku-conclude kwamba hapambani kwa maslahi ya taifa bali anachojaribu kufanya ni kujenga legacy yake binafsi!!

Rushwa haipigwi vita na mtu wala watu bali inapigwa vita na mfumo!! Mfumo unaweza kuishi milele lakini hakuna mtu anayeweza kuishi milele!

Leo hii hata kama Magufuli ataweza kuipiga vita rushwa kwa 101%, kwa mujibu wa katiba, by November 2025 hatakiwi tena kuwepo madarakani! Sasa kama anatarajia ni yeye ndie apambane na ufisadi na sio mfumo, je akishatoka madarakani?! Ina maana taifa lirudi kule kule alikolitoa?!

Ilivyo ni kwamba, hata kama kweli anapambana na ufisadi, basi akishatoka tu madarakani tunarudi kule kule! Tena itakuwa ni kama fungulia mbwa unless awe amepatikana mwingine "kama yeye!"

Lau kama JPM angekuwa na nia thabiti ya kupambana na ufisadi basi angeanza kwanza kujenga mifumo thabiti ya kupambana na ufisadi ili hata yeye atakapotoka madarakani, mifumo aliyoijenga iendelee kupambana na ufisadi!

Anaenda mwaka wa tatu sasa... sijaona nia yoyote ya kujenga mifumo ya kupambana na ufisadi! Mbaya zaidi, hata mfumo wa uhuru wa kujieleza na flow of information ameubana!

Huwezi kupambana na ufisadi ikiwa unabana flow information kwa sababu yoyote ile! JK na utawala wake walionekana sana kama mafisadi kwa sababu palikuwa na uhuru wa watu kuripuwa mabomu!! Bomu liliachwa huru liichane chane serikali na matokeo yake, ilikuwa ni jambo la kawaida kabisa baraza la mawaziri kubadilishwa kila kikao cha bunge kwa sababu wabunge walikuwa na uhuru wa kuisema serikali na watendaji wake!

Turudi kwa huyo Sokoine na Nyerere vs Magufuli!

Hapa hapa JF niliwahi kuhoji kuhusu Marehemu Sokoine! Kwamba, ni kweli kabisa Mwalimu Nyerere alianza vizuri sana, tena sana pasipo na mfanowe kwa viongozi wote waliomfuatia!

Hata hivyo, from mid 1970's, uchumi wa Tanzania ukaanza kuvurugika vibaya mno! Na pale tulipoingia vitani Uganda, hali ikaja kuwa mbaya na hoe hae maradufu!!

Baada ya hapo, nchi ilikosa hata vitu vidogo vidogo kama dawa ya meno na sabuni!! Uzalishaji viwandani ulikuwa chini kupita maelezo na kwa viwanda vingine haukuwapo kabisa! Nchi haikuwa hata na pesa za kigeni!

Ndipo nikahoji na bado nahoji kwa sababu sijapewa jibu la kueleweka: Je, huyu Sokoine huyu... alipambana na Wahujumu wa uchumi upi wakati uchumi wenyewe ulikuwa ICU?! Hivi huyu Sokoine huyu alipambana na Wahujumu wa Uchumi au alipambana na Wafanyabiashara walio-take advantage ya nchi kutokuwa na bidhaa muhimu na hivyo walizitafuta popote pale duniani?!

Anyway, by the time I was too young to care what's exactly going on the country! Matokeo yake, I have strong feelings kwamba hata hawa Wachaga waliochomoza sana kibiashara ni matokeo ya nchi wakati wa Nyerere kukosa bidhaa na matokeo yake, wakatumia fursa ya ukaribu wao na Kenya kuweza kufuata bidhaa na kuziingiza Tanzania kwa kile kilichoitwa "...njia za magendo!"

Kuna Mchaga yeyote humu mtu mzima anielimishe na kunikoa katika hili?! Pascal Mayalla, do you have anything to say on this? jmushi1, any idea?!

So, kama hao Walanguzi na Wahujumu wa Uchumi wengi wao walikuwa ni hawa Wachaga and of course Wahindi waliovuka mpaka na kutafuta bidhaa popote zilipo kisha kuziingiza nchini na hatimae kupata tuhuma za kuziingiza bidhaa kwa magendo; then nina kila sababu ya kuendelea kuhoji vita ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa imepiganwa na Sokoine!!!

Uhujumu uchumi upi ikiwa hata dawa ya meno hao Walanguzi walikuwa wanaitoa Kenya?! Au ni hujumu kwa sababu maghara ya viwanda vyetu yalikuwa yamesheheni bidhaa lakini bado Wahujumu Uchumi wakafuata bidhaa nje na kuziacha bidhaa zetu zikikosa soko?!

Hivi Jasusi yupo wapi siku hizi?! Huyu Bwana pamoja na kuonekana alikuwa karibu au na undugu na familia ya Nyerere, mara kwa mara alijitahidi kuwa honest! Mkuu Jasusi, unaweza kunipa ilmu kuhusu huo uchumi uliokuwa unahujumiwa ni upi hasa?!

Halafu kuna Mkandara, sijui nae yupo wapi! Siku moja tukiwa tunajadili Vita vya Kagera aliwahi kugusia suala la yeye enzi hizo kwenda Uganda kufuata bidhaa! Man, are you still in?! Kama upo, hebu nitoe matongo tongo katika hili... sio kwamba napinga suala la Sokoine na Wahujumu uchumi lakini nashindwa kuelewa elewa... something doesn't add up!!!

FisadiKuu na Wicky, any idea?!

Guys, please tag anyone unayedhani anaweza kutupa idea ya uhujumu uchumi ambao Sokoine alipambana nao au at least anayefahamu upatikanaji wa bidhaa enzi zile!!

JokaKuu
Well said Mkuu
 
Wapi baadhi ya watu katika mtandao huo wa Jf kazi yao ni kutafuta vikasoro kasoro kwenye kila analolifanya Mh.Rais na watumishi wenzake, akisaidia kuichangia shule, utasikia mtu anapost upumbavu humu eti shule zote ziko hivyo, lakini upumbavu wa wabunge flani wanaoibuka hadharani kudai wakurugenzi ni wezi bila kutoa vithibitisho, cha ajabu hakuna anayekemea hiyo tabia chafu. Mtu anayediriki bila aibu kuchafua taswira na Juhudi zinazofanywa na Serikali hii hakika ni Shetani na anadhambi kubwa. Lakini kama mtu huyo ni Chadema binafsi namsamehe bure, kwani Chadema wanajulikana kwa mapungufu yao, mioyo yao ni makazi ya Ibilisi, hata wakipinga hatuoni ajabu, Shetani alipinga hata mema ambayo Mungu wa mbinguni aliyapanga, Chadema ni wakala wa Shetani.
 
Ccm isiogope kupingwa maana hata wale wanaoamini Vitabu vitakatifu YESU na Uungu wake alipingwa. Hata Mungu alipata upinzani kutoka kwa Lucifer.

Upinzani ni kitu kipo tangu ulimwengu usimikwe.
 
Shetani ni wewe unayeacha kutumia akili zako kwa maslahi ya tumbo lako. Ninyi ndio mko radhi kuliuza Taifa kwa maslahi yenu kwa sababu ya kutothamini mustakabali wa Taifa letu.

Kuna mdau kakwambia upinzani upo enzi na enzi na hata hapa tulipitisha rasmi 1992. Sasa kwa nini wapinzani waonekane maadui na wakose haki ndani ya Taifa lao. Mnawafunga, mnawapiga, mnawabambikia kesi, wengine mpaka mnawauwa. Mnajenga mustakabali gani wa Taifa huko baadae? Hali hii itaenda mpama lini umewahi kukaa kujiuliza hilo au unawaza tumbo lako. Mnadai mnapendwa lakini uchaguzi ukija tume na polis ndio waokozi wenu

Uzalendo ni kuweka Taifa lako mbele. Litizama Taifa kwa ukubwa wake hivi vyama vitakuja na kuondoka. Na pia uelewe sio mkosoaji ni Chadema au CUF wengine hatuna vyama

Sasa unataka Tusifie kitu gani wakati maovu ni mengi.

NIKUULIZE, UKIPEWA JUICE KWENYE GLASS YA NUSU LITA HALAFU MTU AKAWEKA KIPANDE KIDOGO CHA KINYESI UTAKUNYWA? .

Hakuna demokrasia, hakuna utawala wa sheria, bunge liko mfukoni hata wabunge wenzenu huko wakitetea maslahi ya wananchi wanatishwa wanaambiwa watapigwa mpaka shangazi zao.

Mitandao haumuipendi kwa sababu huku angalau watu wanaona kuna nafasi ya kutoa maoni yao. Ndio maana mnajitahidi kuidhibiti. Mmeanza kuwabana bloggers na sasa mmeenda kwa vituo vya runinga. Yote haya mnajua hampendwi na hamuungwi mkono. Akija asiweza kulazimisha namna hii ndio mwisho wenu.

Utafiti wa Twaweza unaonesha wananchi hawawaungi mkono na ndio maana mnapita denge kuwanunua, kuwatisha na kuwarubuni wanasiasa ili wahamie kwenu mkiwaahidi nafasi zile zile tena mnavunja na taratibu za Chama chenu. Siasa za kishamba kabisa

Uchumi unayumba sasa hivi kila siku tunakopa, hadi bil 200 nazo tunakopa, na hapo ndio mnakamua kodi kila mahala na kubana matumizi lakini ajabu mishahara haipandishwi,Sekta binafsi zinakufa watu ajira wamepunguzwa.

Si ajabu hata wewe unajua hali halisi lakini kwa sababu unalipwa kutetea kama wenzako inakubidi ufanye hivyo maana msipotetea hakuna wananchi wa kawaida wa kuwatetea
 
Nimesoma kwa kina sana mawazo yako, nilichogundua ni kwamba elimu yako ni ndogo na imepelekea hata uelewa wako use finyu, kama kweli Watanzania wameichoka Serikali yao ya awamu ya 5, umefuatilia mikutano ya Mhemiwa Rais ? Watu wanajaa kupita kiasi, je watu yao wanalazimishwa ? Wanakamatwa na polisi na kuletwa kwenye hadhara? Kama hawampendi Rais na Serikali yake kwanini waje? Kuhusu kukopa ni jambo la kawaida, mwaka Jana Marekani ilikopa US $ 900 kutoka World bank, je ndiyo kusema ilichukiwa na Wamarekani? Huko Marekani jumbo moja walijaribu kumpinga Trump kwa kuendeleza maandamano, kilichotokea walipiga sana, na 3 wenye asili ya kiafrika na kiasia walipata ulemavu wa kudumu, 7 walifungwa miezi 3 kila mmoja, sasa ikifanyika Tanzania tena kwa mujibu wa sheria kwanini inakuwa nongwa? Chadema hamfai, na hii tabia ya kishetani itawapeleka kuzimu.
 
Mikutano ya kusomba wanachama wenu na Malori kuwaweka sehemu moja kwa nini wasijae. Na sio kila anayekuwepi mkutanoni anakuunga mkono. Hata mimi akiwepi ntaenda.

Kuhusu elimu yangu ukitaka unaweza ukafahamu kisha ukalinganisha na yako .

Wasomi wengi hawawaungi mkono poa. Ndio maana mfano wa wasomi wanasheria Tz nzima hawawaungi mkono wako radhi wawachague viongozi wanaikosoa sana Serikali ndio maana wanawachagua watu kama Karume. Huo ni mfano tu. Kwa ufupu mmechokwa sana mnalazimisha mambo. Kazi mnayo angalia hata humu mitandaobi hamupendwi.
 
Argument zenyewe chali, mistari miwili !!! Tena haina hata mawazo yenye tija, thibitisha Ccm imechokwaje? Wakati Wabunge na wanachama wa vyama vingine tena Wasomi na wanasheria wanatimukia Ccm? Huko Chadema mbona hawaendi? Kumchagua Karume kuongoza TLS hakumasnishi kuichukia Ccm, kwani TLS ni Chama cha Siasa? Sasa unalingaishaje Chama cha Wanasheria Tanzania na Chama cha Siasa? Nfdiyo maana nimesema Elimu yako na uelewa wako ni mashaka matupu, huenda wewe ni miongoni mwa watu wenye vyeti feki.
 
Ngoja nifanye mengine. Maana mwenzangu hapo unalipwa siwezi kuendelea kubishana na wewe Mkuu The Genius. Naona umehama kutoka kutokuwa na elimu, umehamia vyeti mwisho utasema na jina nililotumia nimenunua kwa mtu sio langu ukadhani ni kama Bashite. Siku njema😀
 
NJAA mbaya sana usije kuta huyu naye ni musomi mzuri tu ila kageuzwa msukule au anajifanya hayawani na watawala yuawatumikia
 
Rais yeyote anayependa luxury life huwa hathubutu wala kujihusisha na coplicated projects hata kama zinafaida kwa wananchi wake kwa sababu zitamnyima muda wa kula bata, kweye hili,, Rais Magufuli ni kama mbingu na ardhi ndio maana anathubutu.

Big 5 My President!
 
Rubbish! Glorifying a dictator!
 
Anathubutu kwasababu hera sio ya kwake na pia hana huruma na wa Tznia.....huwezi kucheza kamali na maisha ya wtznia
 
Back
Top Bottom