Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Na Emmanuel J. Shilatu

1. Watoto wetu wasingesoma elimu ya msingi mpaka sekondari bure na wangeendelea kutumikishwa majumbani, kuwa Watoto wa mitaani kama ilivyo awali. Juhudi za Rais Magufuli zimemkomboa Mzazi/mlezi na mzigo wa ada na michango na ameokoa kizazi na vizazi dhidi ya mapambano ya adui ujinga.

2. Nidhamu na uwajibikaji kwa Watumishi wa umma usingeimarika na dharau, matusi, uvivu, rushwa na ufisadi ungeendelea kutamalaki kama awali. Juhudi za Rais Magufuli zimeirejesha Tanzania kwenye nidhamu ya kazi.

3. Suala la ujenzi wa flyovers lingeendelea kubaki kwenye makaratasi tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Watanzania tunashuhudia flyover ya Tazara. Hizi ni juhudi za kiuwezeshi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kupambana na foleni nchini.

4. Ujenzi wa reli ya kisasa kwa standard gauge inayotumia umeme usingekuwepo. Bila ya juhudi hii ya Rais Magufuli, Watanzania tungeendelea kutumia muda mrefu njiani, gharama za usafiri na usafirishaji zingeendelea kuwa juu.

5. Watanzania tungemiliki lini tena ndege za kisasa aina ya dreamliner 787-8 ama ndege ya Bombadier kwani shirika letu la ndege lilishakuwa juu ya mawe. Juhudi za Rais Magufuli zimemrudisha "Twiga" (ndege) angani na leo hii anaonekana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania huku akitengeneza faida ya Tsh. Bilioni 4.5

6. Watuhumiwa wakubwa 'Mapapa' ya rushwa na ufisadi wasingepandishwa Mahakamani. Uonefu, upigaji na matabaka ndani ya jamii yangeendelea kukua. Juhudi za Rais Magufuli zimesaidia Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na 2017 huku ikishika nafasi ya pili (2) kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama haitoshi zaidi Tsh. Bilioni 127.9 zimeokolewa na Serikali kwa kuzuia vitendo vya rushwa na mali zenye thamani ya Tsh. Bilioni 4.5 zimezuiliwa na nyumba 6 zimetaifishwa. Hayo ni matunda ya juhudi ya Serikali ya Rais Magufuli.

7. Suala la Serikali kuhamia Dodoma lingeendelea kubaki kwenye makaratasi tangu yalipoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere mwaka 1973. Juhudi za Rais Magufuli zimefanya leo hii Serikali kuhamia Dodoma na Dar es Salaam kubaki jiji la biashara.

8. Mradi wa ujenzi wa umeme wa Stiegler's Gorge ambao utazalisha megawatz zaidi ya 2100 ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere mwaka 1981 ungeendelea kubaki kwenye makabati. Juhudi hizi za Rais Magufuli zitapelekea Watanzania tuwe na umeme wa uhakika na hata bei ya umeme itapungua na gharama za maisha kuendelea kupungua zaidi.

9. Nidhamu na heshima ya Serikali imeimarika sana. Juhudi za utawala wa Rais Magufuli zimepelekea uimarikaji wa ulinzi, amani na usalama nchini; heshima ya viongozi wa Serikali imeimarika; na suala la migomo na maandamano limebaki historia.

10. Mapambano dhidi ya uhuru wa kiuchumi tungechelewa sana kuyaanza. Kwa juhudi, ujasiri, nidhamu na uzalendo wa Rais Magufuli leo hii Watanzania tunaendelea vyema na mapambano ya kujenga uchumi wetu kwani makusanyo ya mapato yetu kwa mwezi yamefikia Tsh. Trilioni 1.3 , ukuaji wa uchumi wetu umefikia asilimia 7.2 , reli inajengwa, bomba la mafuta linajengwa, ndege zinanunuliwa na madini yetu yamedhibitiwa vilivyo ili rasilimali hizi zimnufaishe Mtanzania pekee.

*Shilatu E.J*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo la elimu ni bora elimu wala si elimu bora. Wanafunzi 120 darasani na unategemea mwalimu atafahamu mwenye kuhutaji msaada zaidi wa hesabu hapo?

Huko la ndege ni bomu kitalipuka si muda mrefu.
 
Afadhali afanyaye, hata akiboronga, kuliko asiyefanya na kutegemea "wahisani" na safari za kuhemea!
 
Hilo la elimu ni bora elimu wala si elimu bora. Wanafunzi 120 darasani na unategemea mwalimu atafahamu mwenye kuhutaji msaada zaidi wa hesabu hapo?

Huko la ndege ni bomu kitalipuka si muda mrefu.
Punguzeni uzinzi.
 
Kwa kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Rais Magufuli ni dhahiri wazi kiongozi huyu ameonyesha ujasiri wa hali ya juu kama alivyokuwa Hayati Edward Sokoine.
Wakati Rais Magufuli alipoanza kasi ya kupambana na ufisadi wananchi wengi walitegemea ingekuwa ni vita vya muda mfupi lakini ni wazi Mheshimiwa Rais Magufuli amedhamiria kufuta ufisadi wote hapa nchini. Kwasasa nakubali Mheshimiwa Rais Magufuli amechukua hatua ama njia ambayo Hayati Edward Sokoine aliyotaka kuifuata wakati akiwa Waziri Mkuu kabla mauti haijamkuta mwaka 1984.
 
Katika Historia ya Dunia toka iumbwe Tanzania ndio Taifa lililowahi kuwa na Watumishi hewa wengi....Walikua 20,000, Walikua wakilipwa mshahara wa wastani Bilioni 226 kwa mwaka Tunaposema Hewa ni watu ambao hawapo, ni Majina aidha Feki au ya Waliofariki lakini yapo kwenye Payroll, Fedha zinaingia Mifukoni mwa Makanjanja wachache, wanapiga, Achilia Mbali Mshahara, hizo Hewa zilikua zikilipwa mpaka Fedha za Likizo, House Allowances, Overtime, Posho za safari n.k

NOTE : Utasikia Nyumbu inasema Namchukia Magufuli kweli, Maisha yamekuwa Magumu".
FB_IMG_1536175182360.jpg
 
Mkuu mbona hueleweki unakusudia nini?! Kusifu na kuabudu au?! .
Tangu wsmetumbuliwa hata ajira za maana kwa Vijana wahitimu hamna!!
 
Unadhani hivyo viwanda anavyopigia kelele kila siku ni kwa ajili ya ajira ya Jesca? vijana wengi watapata ajira humo au ulitaka awaajiri vijana wapi kwa mfano, kama huna sifa utaajiriwaje, kucha kutwa mnabeti mnatoka na GPA za 32 nani akuajiri.
 
Back
Top Bottom