Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Kwa hatua nyingine ya kununua ndege Mpya ya Airbus A220 - 300 iliyopewa jina la Ngorongoro.

Ndege Ngorongoro Ni Airbus ya pili kutua nchini. Ya Kwanza ni Airbus Dodoma. Tukumbuke ndege Aina ya Airbus Ni ndege ya Kwanza kabisa Afrika inayomilikiwa na Watanzania. Hiyo ni alama isiyofutika iliyoandikwa na Rais Magufuli kwa Tanzania, Afrika na Dunia Kwa ujumla.

Tukumbuke ndege iliyotua Leo Ni ya sita kununuliwa na Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli. Ndege nyinginezo no Bombardier Q400 ambazo zipo 3, Dreamliner 1, na Airbus A220 - 300 ambazo zipo 2. Jumla kuu Ni ndege 6, bado ndege moja.

Ndege hizo zitasaidia kukuza utalii, kuitangaza nchi yetu Tanzania, kukuza biashara, kuongeza mapato ya ndani ambayo yataimarisha uwezo wa ndani wa Serikali kuwahudumia Wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Tunachojivunia Kwa Rais Magufuli sio tu ndege 6 bali ameweza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari; kujenga miundombinu Kama flyovers; ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango Cha standard gauge inayotumia umeme; ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000; ujenzi wa vituo vya afya vipya pamoja na madarasa.

Mengineyo Ni ongezeko la mapato ya ndani kutoka Tsh. Billion 800 Hadi Trillion 1.3; Ongezeko la wastani wa asilimia 1.5 ya ukuaji wa uchumi nchini; Ongezeko la Tsh. Billion 107 ya makusanyo ya mapya ya madini nchini; Ujenzi was strigler's gogle itakayozalishi zaidi ya megawats 2100.

Hayo ni kwa uchache zaidi ya Mambo mema yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli. Hakika huyu ndio Rais Watanzania tuliokuwa tukimwitaji zaidi.

*Shilatu E.J*

Sent using Jamii Forums mobile app
hivii yale makinikia yetu pale bandarini veepeee[emoji12] [emoji196]
me nimeweka oda ya noah[emoji604] [emoji604] [emoji12] [emoji12]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Miaka 3 ndege 6 lkn kumbuka maendeleo ya nchi yamesimama,ajira imesimama,kupandisha vyeo imesimama hata swala la kikokoyoo lisingepigiwa kelele ingeleta ndege nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..tangu tununue ndege tumepata FAIDA kiasi gani?

..au tangu tununue ndege serekali imetoa RUZUKU kiasi gani kwa ATCL?

..Je, CAG atatupa majibu ktk taarifa yake inayokuja?

Au atazuiwa kukagua mahesabu ya ATCL?

Cc chige
 
Hakika Rais Magufuli ana uthubutu ambao sijawahi ona...

Kila nikitafakari amewezaje kuyafanya haya kwa muda mchache hivi, tena kwa fedha zetu wenyewe naona watangulizi wake walikiwa wazinguaji sana...

Hapo bado 8 ways, stigler gorge na SGR. Hakika Mungu ampe maisha marefu Rais wetu
 
Kwani hazikuwepo mbwa nyie.

Zilikuwepo ziko wapi sasa...

Atleast kwa Mheshimiwa Rais Mali za umma zimeanza kuogopwa kama ukoma, kwa upande wa pili naona waanzilishi wake walikuwa wazembe kiasi...

Kwa hizi za sasa na imani zitashuhudiwa na wajukuu zetu..
 
Mkuu huu uzi wako ni mzuri lakini utasogea taratibu. Wadau humu ndani akili zao wamezipeleka kwenye mada za CAG na Ndugai.
 
Acha ushamba, fedha ambazo zingeajir wafanyakaz wapya na kupandisha madaraja waliopo ndo zimetumika kununua ndege, ni sawa na ww upunguze kunywa bia ili upate pesa ya kununulia iphone 7. Ni reallocation of funds tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Reallocation of funds, umetumia neno sahihi kabisa. Miaka ya JK bunge lilikuwa linaidhinisha mabilioni kwa ajili ya chai, unabaki kujiuliza hivyo vikombe vya hiyo chai ni vya dhahabu!.
 
Wastaafu wamekatwa mafao yao, watumishi hawajawahi panda vyeo toka JP awe mkulu, hamnaga annual increment ni kodi kila kona mwisho wa anasifiwa alietumia kodi zetu na siyo yule aliechangia kodi mpaka familia ikalala njaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huu uzi wako ni mzuri lakini utasogea taratibu. Wadau humu ndani akili zao wamezipeleka kwenye mada za CAG na Ndugai.

Hao bavicha akili zao zinaendeshwa na tetesi tu, wananchi wenye akili huwezi wasikia wakisema maana wanajua Magufuli ni mzalendo kwelikweli na amedhamilia kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati...
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Kwa hatua nyingine ya kununua ndege Mpya ya Airbus A220 - 300 iliyopewa jina la Ngorongoro.

Ndege Ngorongoro Ni Airbus ya pili kutua nchini. Ya Kwanza ni Airbus Dodoma. Tukumbuke ndege Aina ya Airbus Ni ndege ya Kwanza kabisa Afrika inayomilikiwa na Watanzania. Hiyo ni alama isiyofutika iliyoandikwa na Rais Magufuli kwa Tanzania, Afrika na Dunia Kwa ujumla.

Tukumbuke ndege iliyotua Leo Ni ya sita kununuliwa na Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli. Ndege nyinginezo no Bombardier Q400 ambazo zipo 3, Dreamliner 1, na Airbus A220 - 300 ambazo zipo 2. Jumla kuu Ni ndege 6, bado ndege moja.

Ndege hizo zitasaidia kukuza utalii, kuitangaza nchi yetu Tanzania, kukuza biashara, kuongeza mapato ya ndani ambayo yataimarisha uwezo wa ndani wa Serikali kuwahudumia Wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Tunachojivunia Kwa Rais Magufuli sio tu ndege 6 bali ameweza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari; kujenga miundombinu Kama flyovers; ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango Cha standard gauge inayotumia umeme; ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000; ujenzi wa vituo vya afya vipya pamoja na madarasa.

Mengineyo Ni ongezeko la mapato ya ndani kutoka Tsh. Billion 800 Hadi Trillion 1.3; Ongezeko la wastani wa asilimia 1.5 ya ukuaji wa uchumi nchini; Ongezeko la Tsh. Billion 107 ya makusanyo ya mapya ya madini nchini; Ujenzi was strigler's gogle itakayozalishi zaidi ya megawats 2100.

Hayo ni kwa uchache zaidi ya Mambo mema yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli. Hakika huyu ndio Rais Watanzania tuliokuwa tukimwitaji zaidi.

*Shilatu E.J*

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio Gavana Shilatu tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom