Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Naomba kuwasilisha waungwana
Katika kipindi cha takribani miaka minne ya Mh.Rais watumishi Wa umma wamekuwa wakilia na kulalamikia nyongeza.
Naomba nikili kuwa si kweli kuwa mh rais aliamua kuzuia nyongeza kwa makusudi Bali ni kutokana na mipango mipana aliyokuwa nayo Mh.Rais katika kuhakikisha taifa linasonga mbele
Ili kuonesha kuwa rais wetu anajali masrahi ya watumishi Wa umma kuna taarifa nimepenyezewa toka chanzo cha kuaminika kuwa kilio cha watumishi Wa umma kitatatuliwa hivi karibuni ambapo Mh .rais JPM atapandisha mishahara ya watumishi Wa umma maradufu kwa mwaka Wa fedha 2019/2020
Naomba nitoe pongezi zangu za dhati kutoka kwenye uvungu Wa moyo wangu kwa Mh. JPM kwa hatua hii ya kuwajali watumishi Wa ummma
Viva magufuli,Magufuli for 2020-2025
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Serikali ya JPM mimi sina shaka na hili, hata kama haitakuwa kwa kiwango hicho lakini naamini kila mtumishi wa umma lazima ataridhika na nyongeza itakayotolewa. Ushauri wangu tu ni kuwa wakishapandisha mishahara, wahakikishe kuwa mishahara mipya inalipwa by July 2019 ili kusudi kusiwe na accumulations ya arrears! Imekuwa trend tangu mwaka 2012 kuna taasisi ambazo zimesha-specialize kwenye issue ya ku-deal na arrears tu kwamba ukishakuwa na arrears sababu ya mabadiliko ya mshahara, basi hizo ndiyo imetoka usahau kuzipata. Mimi mara ya mwisho nilipata arrears ilikuwa kabla ya 2012, na baada ya hapo huwa nazisikia tu kwenye bomba hadi leo. Hayo ndiyo maisha ninayoishi na ninasikitika kwamba imefikia hatua hadi nimeyaweka wazi kwenye mtandao; siyo mropokaji wa kiwango hicho. Mimi naomba JPM aukarabati kabisa uchafu huu uliokuwa umekithiri huko nyuma. Huwa inaniumiza sana mimi kuona mshahara wangu unaliwa na mtu mwingine au unatengenezewa mazingira ya kulazimisha kuliwa na mtu mwingine. Halafu ukiangalia taasisi zingine wala hazifanani na mambo kama haya. Mimi kwa kweli siku nikawa nina rungu halafu nikabahtaika kukamata mtu anafanya mambo ya aina hii kama ninayoyalalamikia hapa,...., kwa kweli nitashukuru ila.....