Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mgao ni nini kwani na ni nani anayetoa taarifa ya hitilafu mara umeme unapokatika?

Mara ngapi watu wa Dar umeme umekuwa unakatika kwao kila wiki mara moja ama zaidi ya mara moja?
Kumbe hata hujui mgao wa umeme. Haya siku njema.
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

Habari zaidi, soma =>Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...
Naomba urudishe uzi huu mikononi mwangu kabla sijawajulisha moderators. Uzi huu niliuanzisha mimi inakuwaje leo uko kwako?
 
Kama unaweza bet. Jina Rais wa sasa wa Tanzania basi. Unaliwa tena Unaliwa mcha kweupe.

Hana mchezo Wala Usije fanya mchezo na agizo lake Wala Usije cheka wakati hacheki.

Amesema amesema 5 years sasa Tz hakuna mgao na usiniulize nin kafanya
Miaka mitano sasa hakuna bei kupanda na usiniulize kafanya nini.

Miaka mitano na tuna madege yakutisha usiniulize kafanya nn.

Kizazi cha majizi anakifuta kabisa kama sio kukipoteza ktk system

Miradi yote kukamilika before 2025 nalazima imalizike kama. Una duwa lingine omba ila usi bet Rais wa sasa utaliwa tutusa

Wale ambao maslahi yao yamekanyagwa wote wanapigwa mawe ya gizani...Ukisikia nywii ujue kaguswa nyeti zake...Katika hali ya kawaida hakuna ambaye hakubaliana Mh. Magufuli ni jembe na wala hana wakufananishwa naye...Ana track record inayojitetea tangu alivyoingia kwenye decision making level 24 years ago...Hajawahi punguza kasi wala badili tabia...For me kusema ukweli hata pamojana kuwa binadamu na mabaya yake mie ya Magufuli yamefunikwa na chanya kabisaaa...Hapa mie ni mahaba niue ni galagaze ndiyo yaliyonikuta....
 
ebu tutajiyeni hayo aliyofanya japo moja halafu musisahau tu kwamba huu sasa ni mwaka wa 60 toka ccm kutawala nchi hii halafu huyo mtu katika mambo mazuri atakayo fany ni pamoja na kuiba kura 2020 na kufanya mapinduzi tena zanzibar
 
Nimezungumza na hawa Wazee Wasomi na Maarufu ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikitaka kujua nini hasa sababu ya Ukimya wao katika awamu hii ya tano.

"Mimi ni Msomi, napaswa kutumia usomi wangu kusimama katika ukweli, naridhika na jinsi Rais Magufuli anavyotekeleza zilizokuwa agenda za Chadema tangu wakati wa Katibu Mkuu, Dr. Wlbrod Slaa, sina sababu ya kurudisha nyuma jitihada za Mhe. Rais, Tanzania kwanza vyama baadaye" Hayo ni maneno ya Prof. Mweisigwa Baregu.
Wengine wenye mtazamo huo ni Mwasisi wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei na Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Prof. Abdallah Safari.
Sikuweza kumpata Mwanasheria Mabere Nyaucho Marando na watu wengine maarufu ndani ya Chama ili kujua kama nao Ukimya wao unatokana na sababu zilizotolewa na akina Mzee Mtei na Wenzake. juhudi za kuweza kuwafikia zinaendelea.

Tanzania kwanza, Vyama baadaye.
Mungu ibariki Tanzania
Siku njema Watanzania wenzangu.
 
Imekuwaje tena mbona CCM huwa wanasema wapinzani wanapinga kila kitu kinachofanywa na serekali ya Magufuli?.
 
Hivi mleta mada unajua huu ni mwisho wa mwaka wa kuaminishwa kwa clip???

Bila clip post yako ni ya 'hovyooo haijawahi tokea"

By MTUNDU VOICE.
 
Ulitaka usikie majibu yao ili muwafungulie kesi ya money laundry kama Kabendera?
Maana siku hizi ukitoa maoni tofauti na kuunga mkono 'juhudi' unakumbana na money laundry au uhujumu uchumi.
Labda uwe jasiri kama kina Mbowe, unamuweka gerezani miezi mitatu anatoka anatabasamu tuu na bado unamtembelea kwake anaendesha maombi kukuombea kwa Mungu hadi unaona aibu.
 
Hii nchi kuna haja kutunga sheria ya mind laundering ili mnaotakiwa kurudi mirembe mrudi tu mmezidi kutupigia kelele
 
Nakumbuka Mzee Baregu hata wakati Wa Bunge la Katiba alitumia maneno hayo alipohojiwa kwanini alikubali uteuzi Wa kuwa Mjumbe Wa Bunge hilo , alisema akiambiwa achague nchi na chama atachagua nchi kwanza. Hana kona kona kwa kweli huyo mzee
 
Hadi umeandika kwa font size kubwa kabisa ili watu wote wasome!!!
 
Hapo ndiyo utajua tofauti kati ya Msomi aliyeelimika na Msomi ambaye usomi wake uliishia kwenye makaratasi kama akina Lissu.
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

Habari zaidi, soma =>Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...
Labda mwanachadema wa Lumumba ndo ameridhika.
 
Mkuu nimeona nikukumbushe uzidi kukaza buti,kama ni dawa imewaingia kisawasawa,kwa sasa wanatapatapa tu.

Kazi ulioifanya ndani ya miaka minne kwa taifa hili ni ya kutukuka ,haiitaji tochi kuiona.

Mafanikio ya serikali yako ya awamu ya tano, kila nyanja yanonekana. Kwa uchache ni ,Afya,elimu,miundo mbinu,nk, ni mengi mazuri
Piga kazi kwa speed ileile na ikibidi ongeza speed,
Wewe ndie Amiri jeshi mkuu,katiba imekupa mamlaka kiutendaji,itendee haki Tanzania hii yenye utajiri mkubwa kila siku inaitwa maskini.
Sisi sio maskini,tulikosa usimamizi mzuri wa raskimali zetu,wewe umepatikana,simamia kwa nguvu zote.

Kuna kakikundi flani kanajaribu kukuzuia kufanya kazi,kakishirikiana na baadhi ya wakoloni wapuuzi.haka kakikundi kashughulikiwe ipasavyo bila huruma.

Ili taifa lisonge ni lazima wengine wachache waumie ,iko hivyo duniani kote,(especially puppets),sisi sio wa kwanza .

Haiwezekani wakatokea watanzania wachache ambao wako kimaslahi zaidi, kazi yao ni kuipaka nchi matope kila uchao wachekewe kisa wana mahusiano na waingereza na wamarekani,washughulikiwe tu,hata hizo nchi wanazozishitakia zimewaadhibu watu wa aina hii kwa tabia kama hizi tunazoziona hapa nchini.
Mbaya zaidi wanakua bias,kana kwamba nchi hii hakuna mazuri yanayofanyika wakayatangaza.

Mwisho, fanya yaliomema kwa maendeleo ya watanzania ,kwani lawama hazikosi popote pale,hakikisha unawapa watanzania walio wengi furaha kwa kuwaletea maendeleo,achana na hawa wachache wachumia tumbo,ambao wamejikita mitandaoni kufarijiana
 
HUNA AKILI WEWE
 
Back
Top Bottom