Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ni kweli ana mambo mazuri..ila suala la uchumi,haki na utawala bora..bado anapwaya.

Miundo mbinu heko..ingawa mingi ni madeni na mikopo.
 
1.Ambao maisha kwao ni raha tu/bila chembechembe ya shida
2.Tulipata wadangaji wa kutosha wake kwa waume.
3.Tulipata walevi wengi wa Pombe
4.Tulikuwa na kizazi cha watumia madawa ya kulevya.
5.Mashoga waliongezeka.
6.Vijana hawakupenda shule
7.Vijana waliolewa sana na wamama watu wazima.
8.Matapeli wengi
9.Kipindi ambacho Vijana walifanya maamuzi rahisi na si maamuzi sahihi
10.Nchi isingeweza kujengwa na wasiofanya kazi!!!
"Pamoja na mapungufu yako kama mwanadamu,pa 1 sana JPM"
Umevimbiwa maharage ya wapi mzee?
 
Hakika msema kweli ni mpenzi wa Mungu, MAENDELEO hayana vyama!
Nchi yetu ilibahatika sana mwaka 2015 kupata Rais bora kabisa barani Africa ikiwa pamoja Na ubora wake anafanyakazi sawa tu Mwl Nyerere.
Ufanano upo katika maeneo mengi mfano Taifa stars ilishiriki AFCON kipindi cha Nyerere, na Leo inashiriki kipindi cha JPM, Nyerere alinunua ndege Na JPM kanunua ndege, Nyerere alinunua Na JPM hivyo hivyo,Nyerere alitoa Elimu bure Na JPM hivyo!
Kwa kifupi tuendelee kumshukuru Mungu kwa kutupa Rais bora Na kutupa amani iliyotukuka.
Mwisho nasema kwa uwazi simpendi kabisa kabisa Tundu Lissu.
 
Hakika msema kweli ni mpenzi wa Mungu, MAENDELEO hayana vyama!
Nchi yetu ilibahatika sana mwaka 2015 kupata Rais bora kabisa barani Africa ikiwa pamoja Na ubora wake anafanyakazi sawa tu Mwl Nyerere.
Ufanano upo katika maeneo mengi mfano Taifa stars ilishiriki AFCON kipindi cha Nyerere, na Leo inashiriki kipindi cha JPM, Nyerere alinunua ndege Na JPM kanunua ndege, Nyerere alinunua Na JPM hivyo hivyo,Nyerere alitoa Elimu bure Na JPM hivyo!
Kwa kifupi tuendelee kumshukuru Mungu kwa kutupa Rais bora Na kutupa amani iliyotukuka.
Mwisho nasema kwa uwazi simpendi kabisa kabisa Tundu Lissu.
Umesahau kitu kizuri kweli .Enzi ya Nyerere hakuna kujenga Nyumba bora na kumiliki pesa na sasa hivyo hivyo.
 
Naunga mkono hoja lakini kuhusu kumchukia tundu lissu nimekataa sikubaliani na wewe.kuna mambo nimeyaacha tutajua huko mbele kwa mbele ya kiti Cha hukumu Cha mwenyeziMungu..ila Magufuli tumekubali
 
Naunga mkono hoja lakini kuhusu kumchukia tundu lissu nimekataa sikubaliani na wewe.kuna mambo nimeyaacha tutajua huko mbele kwa mbele ya kiti Cha hukumu Cha mwenyeziMungu..ila Magufuli tumekubali
Ndege JOHN !!! uko vizuri kumbe una akili zinakutosha kabisa nahisi hukuwahi enda pale club billinicana!!
 
Ndege JOHN !!! uko vizuri kumbe una akili zinakutosha kabisa nahisi hukuwahi enda pale club billinicana!!
Nimewahi kwenda Mara moja tu na rafiki zangu kina dark master huyuhuyu wa chemba squad,Tyson mcee wa mbeya ilikuwa mwaka 2011..kwanini kwanza umegusia habari za club billicanas
 
Nimewahi kwenda Mara moja tu na rafiki zangu kina dark master huyuhuyu wa chemba squad,Tyson mcee wa mbeya ilikuwa mwaka 2011..kwanini kwanza umegusia habari za club billicanas
Wengi walijiunga kwny matumizi ya vilivyopigwa stop duniani kote
 
Wengi walijiunga kwny matumizi ya vilivyopigwa stop duniani kote
Inasikitisha Sana jinsi watu wachache walivyoumiza ndugu zetu na kuwaharibu kwa kuwauzia ngada halafu Inauma Zaidi unapogundua KIONGOZI ambaye anajinasibu kutetea vijana kumbe ndo muuza unga mkubwa
 
Kwa hali hii ya uchumi kukua kwa viwango hasi!!!!.... Tutakubaliana baadaye.
 
Let support our presdent: Mimi sinachama ingawa ninaitikadi za kipinzani, mwaka 2015 sikupiga kura yangu palipoandikwa ccm, yaani sikupoteza muda.
This man is brave, najiikia ufahari kulipa Kodi kwa ajili ya ujenzi wa nchi yangu. Najionea kwa macho yangu vile Kodi yangu inafanya kazi. Jenzi mbalimbali hapa jiji Dar hazikuwezekana hapo awali but now I witness by naked eyes yakuwa kumbe vitu vilikuwa vinawezekana. I love my presdent the way anasimamia kodi yangu. Wakazi wa dar mtaniunga mkono, Ni miaka mingapi tulisikia ujenzi wa barabara za juu lakini hayakutekelezwa zaidi ya siasa? Sasa mbezi, Kibamba inakuwa a new town, stand yakoa ipo onajengwa, barabara sitaki kutaja maana Ni nyingi mno za mitaa na main roads, ubungo interchange etc.

Enyi wakazi wa Ludewa barabara ya Njombe Ludewa ilikuwa ni ndoto kujengwa lakini Sasa mnashuhudia ya kwamba kumbe inawezekana, wakazi wa mbambabay ni mashahidi. Ni mengi ya kusema wadau wa pande zote nne za beautiful tz tunaweza ongea ukweli wa yanayoendelea maeneo yenu.

Tumpe moyo raisi wetu na tulipe Kodi kwa moyo wa kujenga nchi yetu tusiwe na dhana Kodi km adhabu au kuonewa! Let's pay tax kwa ujenzi wa nchi yetu.

I enjoy paying tax, I enjoy using my contries inglustructure I love my presdent JPM. Mungu akitujalia uhai kura ya raisi 2020 nikupa JPM.

Nilikwazika: kutunyima bunge live, kuwakumbatia DAB na wengine wa hulka km hizo, kubana upinzani, vyombo vya habari. Dhana as kila mpinzani ni adui
 
Sidhani kama kuna asiyemuunga mkono
kiongozi wetu. Kumshauri kinyume na anavyoona, sio kutomuunga mkono.

Mfano leo korosho zimekwama magalani na nyingine zinaingia sokoni soon, tunaenda kupoteza mamalioni ya dola kwa staili za kukurupuka na kuunga mkono kinafki.
 
Na Shilatu E.J

1. Amesimamia vyema utolewaji wa ELIMU BURE kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kwa wanyonge.

2. Amesimamia vyema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini.

3. Amesimamia vyema kulinda maisha na kuhakikisha rasilimali za nchi ni mali ya Watanzania wote.

4. Amesimamia vyema nidhamu, uwajibika na uadilifu kwa Watumishi wa umma

5. Amefufua shirika la ndege la ATCL kutoka kutokuwa na ndege hadi kuwa na ndege mpya 6 za kisasa zinazopasua anga za kitaifa na kimataifa.

6. Amesimamia Tanzania kufika uchumi wa kati unaokuwa kwa asilimia 7.1% kupitia mafanikio ya sera ya Tanzania ya viwanda zaidi ya 3000 vilivyojengwa.

7. Amesimamia vyema Serikali kuhamia Dodoma ikiwa ni ndoto aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

8. Amejenga reli ya kisasa yenye kasi inayotumia umeme (SGR) na kufufua reli ya Dar - Tanga - Moshi Kilimanjaro.

9. Ameongeza makusanyo ya mapato ya ndani na kusimamia nidhamu ya matumizi ya pesa.

10. Amesimamia ujenzi wa mradi wa umeme Mto Rufiji wa Stiglers gogle utakaozalisha megawatts 2115.

11. Amesimamia ujenzi miundombinu ya kisasa ya mitandao ya barabara, flyover na madaraja.

12. Amekomesha biashara ya ujangiri na madawa ya kulevya nchini.

13. Ameleta maboresho ya afya nchini kwa kujenga hospital zaidi ya 57, vituo vya afya zaidi ya 350, ununuzi wa madawa na vifaa tiba hospitalini.

14. Ameisimamia vyema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulinda amani na usalama nchini hali inayofanya Watanzania tuendelee kujivunia uhuru wetu na kuvutia Watalii nchini.

15. Amejenga umoja, mshikamano wa kitaifa nchini.

Rais Magufuli ameyafanya yote haya, Mimi ni nani haswa nisimchague tena 2020. [emoji736]
 
NI NINI DHAMIRA YA MZEE KINANA, MAKAMBA NA GENGE LAO?

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa nafasi hii ili niweze kuzungumza na Watanzania wenzangu leo, hasa wanaCCM. Nimeamua kutumia uhuru huu wa kikatiba ibara ya 18 baada ya kuona habari mbali mbali kwenye vyombo vya habari ambazo ni za kifedhuli kwa Chama na Serikali yetu. Hatuwezi kukubali CCM na serikali kutunwa na Waliotufisha anakotutoa JPM.

Mwanzo ilitokea barua iliyosadikika imetoka kwa wazee wetu wastaafu yaani mzee Kinana na Mzee Makamba. Nimesema inasadikika kwa kuwa hawajajitokeza hadharani kukubali au kukanusha. Barua yenyewe iliandikwa kama wito au tamko ambalo lilielekezwa kwenye Baraza la wazee wa CCM linaloongozwa na Mzee Mwinyi kama Mwenyekiti na Mzee Pius MSEKWA kama Katibu wa Baraza hilo. Na kwenye tamko lao waliandika wakionyesha kukerwa na lugha za kudhalilisha zinazotolewa na Ndugu Musiba.

Makamba na MH Nape kwa mwendelezo wa mikakati hiyo hiyo Siku chache baadae zimetokea sauti zinazosadikika zilizodukuliwa. Mwanzo inaonyesha mzee Kinana akizungumza na Mh Nape na wakiwa kwenye mkakati huu ambao ninadhani ndio zao la barua hiyo.Baadae imetokea sauti ya Mh Ngereja na Mh Nape wakiwa kwenye mikakati hiyo ovu. Baada ya siku chache imetokea tena sauti ya Mh Makamba akizungumza na Mh January Makamba na baadae January anamuunganisha Mzee.

Kabla sijatoa kusudio langu la kukemea na kulaani uhaini huu ndani ya CCM, ninaomba tuunganishe dots kidogo. Barua au tamko linalosadikika kutolewa na hawa wazee kwenda kwa Katibu wa Baraza na baadae katibu wa Baraza kujibu ni kuwa mzee Msekwa kwenye barua yake anakiri alipokea barua ya Mzee Kinana na Mzee Makamba kutoka kwa Mh Nape. Kitendo cha Mh Nape kwenda kumpelekea mzee Msekwa barua nyumbani, kitendo hiki kinanifanya niamini hizi sauti hazijatengenezwa na ni sauti zao ambazo maudhui yao ni kujenga mpasuko ndani ya CCM.

Si jambo jema na la hekima sana kwetu vijana kuwakosoa, kuwasahihisha, kuwakemea na kuwakumbusha wazee wetu au viongozi wetu. Lakini ni wajibu wetu vijana wa kuhakikisha tunalilinda Taifa na tunalinda misingi ya CCM. Inapotokea mzee au kiongozi ambaye kwa makusudi anajaribu kutengeneza jaribio la kuhatarisha umoja huu, basi ni wajibu wetu vijana kuvaa uzalendo na kuwakosoa bila aibu wazee hawa ambao baada ya kula matunda ya umoja wa taifa hili sasa wanataka kuharibu misingi ya umoja huu.

Kitendo cha Ndg Kinana na Mzee Makamba kuandika barua ile kwenda kwa Mzee Msekwa ili kuonyesha hisia zao si dhambi, lakini kitendo cha kuandika na kusambaza kwenye mitandao kunaonyesha hawana nia njema. Tukipima actus reus na mens rea(nia) zao zilikuwa ni za hujuma na za kulibagaza Taifa. Ni wazee hawa waliotufundisha maadili ya Chama na kutufundisha namna ya kuyafuata, iweje walimu wa kanuni ndio wawe wa kwanza kuvunja? Nia yao ilikuwa nini? Kwa nini hawakwenda Lumumba kupeleka malalamiko yao?

Labda niwakumbushe tu kuwa wakati wa mzee Makamba ndicho kipindi ambacho mzee Lowasa alitukanwa sana na kufedheheshwa sana. Kipindi cha Kinana mzee Warioba alitukanwa na kupigwa na watu waliosadikika ni Wana CCM na hakuna hatua iliyochukuliwa. Kipindi cha Kinana wakati wa oparesheni vua gamba akiwa Mtwara, Ruvuma na Mbeya alisema kuna mawaziri mizigo na akasema bila kuwasema hadharani tutakuwa wanafiki. Sasa kama wao walitumia mfumo huu wa matusi kwenye kujivua gamba wanalalamika nini kwa ndg Musiba kwenye kujenga CCM mpya? CCM mpya haiwezi kujengwa bila kuwataja wezi, wahaini, na waliotumia hovyo mali za Chama.

Nyie ndio mliotudanganya kuwa CCM ni ya wakulima na wafanyakazi lakini kiuhalisia kipindi chenu CCM ilikuwa ni ya Wafanyabiashara, Wezi na Mafisadi. Mh Magufuli anajaribu kurudisha misingi haswaa ya CCM ili hata wakulima wa Ileje, Nkasi, Namtumbo, Nyakanazi, Ikungi n.k wale matunda ya CCM. Hatuwezi kuendelea kuwa na CCM ya utwana na ubwana mliyokuwa mnajaribu kutujengea. Muacheni Mwenyekiti anyoshe Nchi. Miaka mitatu na ushee ya uongozi wake tunaona vitu vinavyoonekana. Sasa hakuna mapapa ndani ya CCM, hata sis watoto watoto wa vijijini tumekuwa na nafasi ndani ya CCM.

Uhauri wangu kwa viongozi wakuu wa CCM, Ukisoma ile barua na ukisikiliza zile audio ni wazi hawa watu hawana nia njema na Taifa. Wakati tunapendekeza kuwapa adhabu kali ambayo itakuwa fundisho kwa wanaCCM wote wanatakiwa kujitokeza hadharani na kuliomba taifa msamaha kwa uhaini ndani ya CCM. Haiwezekani watu ambao ndio wametufikisha hapa kumuita Rais mshamba na anaogopa kurudi Da res salaam. Huu si upuuzi wa kuendelea kuulea. Tunapohitaji kurudisha Taifa kwenye misingi ya haki na usawa basi hatunahaja ya kumtazama mtu usoni. Mtu yeyote anayejaribu kukwamisha juhudi za Mh Rais si tu si mzalendo bali ni mtu anayetakiwa kutazamwa kwa jicho la tatu.

Mh Rais ni binadamu na si Mungu, hivyo wakati mwingine anaweza kukosea katika kuwatumikia Watanzania Zaidi ya milioni 50. Anaweza kukosea kwa kupotoshwa au kwa namna nyingine. Lakini kwa viongozi kama hao niliowataja hawawezi kutumia lugha kama hiyo kufikisha ujumbe kwa Mwenyekiti. Ili kulinda heshima ya Chama na serikali kama ambavyo Watanzania wengine wamekuwa wakitumbuliwa kwenye nafasi zao wakionyesha utovu wa nidhamu, ni wazi hawa watu wanaoonyesha dhahiri wanaajenda ya siri na huenda huko nyuma kuna ujanja walikuwa wanaufanya maofisini. Ni muda wa kuwachunguza na kupitia upya mafaili yao kama hawajauhusika kulihujumu Taifa wakiwa madarakani.

Wakati ninaandika haya ninajiuliza maswali mengi. Mwaka 2012 niliingia kwenye mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Kizota. Yapo makundi yalijitokeza kuhamasisha MH KIKWETE apigiwe kura za hapana za Uwenyekiti. Mzee Makamba ndiye alisimama na kukemea tabia hiyo kwa ukali na kumuombea mh Kikwete kura. Kutokana na hotuba yake nzuri huku Mh Mkapa akiwa mwenyekiti wa mkutano wa uchaguzi ukumbi ulizizima na tukasimama kumpa fedha za shukurani mzee Makamba. Mkutano wa kumchagua Mh MAGUFULI ni mzee Makamba alipewa nafasi ya kushukuru baada ya Magufuli kupata kura nyingi. Aliongea maneno mengi mazuri, lakini mwisho alimalizia kwa kusema JK aliwabatiza kwa maji, HUYU ATAWABATIZA KWA MOTO. Hivi alitaka ubatizo hupo uwe wa matabaka au usawa? Kama ni wahi basi ni muda wa CCM kuwabatiza hawa wazee kwa ubatizo wa moto.
Barua yao iko wazi imewalenga viongozi wakuu wa CCM, Kwani angekuwa mtu mwingine analengwa kuwa anamkingia kifua Musiba basi barua ingeenda kwenye chama na isingepelekwa kwenye mitandao kuleta taharuki. Sisi Watanzania tuliozoea kula viazi na maziwa ya ng’ombe wa kienyeji hatuna shaka kabisa na Mh Rais. Tunaona ndege zinanunuliwa, barabara zinajengwa hata huku kwetu Ileje, vituo vya Afya, Elimu bure na shule zinaboreshwa, Meli zinanunuliwa, Viwanja vya ndege vinajengwa, safari za hovyo hovyo kwenda nje zinaisha, Utendaji maofisi umeongezeka mara dufu, makusanyo kwa mwezi yamepanda kutoka bilioni 8 hadi 1.3 trillion n.k unaanzaje kuzungumza Rais Mshamba? Huu ni upuuzi na tunaosoma historia ya nchi yetu ilikotoka na tunakoenda sasa hatuwezi kumwacha Mh Rais ambaye wazi ni mzalendo kufedheheshwa na watu waliokula Taifa bila kuwaonea wenzio huruma.

Chama imara huzaa serikali imara, na Chama dhaifu huzaa serikali dhaifu. Ili serikali ipone na Mh Rais aweze kufanya kazi zake vema hakutakiwi kuoneana aibu kwa mtu yeyote. Inawezekana wa mijini msielewe, sisi tulikulia vijijini tunajua shida zilizokuwepo huku. Rushwa ilitamaraki lakini kwa sasa hali hata ukienda hospitali unatibiwa haraka bila kuhonga honga honga.

Hili genge ni kubwa. Mwanzo nilikuwa ni mtu ambaye nilikuwa nikimpuuza ndg Musiba, na nitumie furusa hii kumuomba radhi sana hata kama njia alizotumia kufikisha ujumbe hazikuwa sahihi. Lakini baada ya kusoma barua na kuzisiliza clip ambazo inasemekanna ni za hawa Watu wakubwa ninaona ndg Musiba alikuwa sahihi mno. Ninawaomba Watanzania hasa WANACCM wenzangu ni muda mwafaka wa kumlinda Mh Rais na kuwapuuza hawa watu ambao hawana nia njema. CCM inawatu wengi.Waliondoka nab ado CCM ipo. Tunapotaka kuirudisha nchi tusiangalie sura hata kama mtu ni mkubwa kama mlima Kilimanjaro ashughulikiwe tu.

Ahsante

Elius W ndabila
Ibaba-Ileje
 
Back
Top Bottom