Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Write your reply...huyu anaemzuia CAG asikague madini na kumpa mtoto wa dada wizara ya madini, au unamaanisha john pombe maharage?
 
Anti Corruption hero? Which corruption are you talking about? 😳




Uzi mchungu.. kashalala mbele.
 
Wasalamu ndugu zangu,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosomeka, mimi kwangu napenda kumleta kwenu His Ex. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa jamhuri ya Muungano Tanzania kama nominee katika ushujaa wa upambanaji wa rushwa hapa afrika.

Tumpe sapoti mkuu wetu wa nchi azidi kuyatenda yale yaliyomema kwetu.

Kataa rushwa.. usitoe,usishawishi wala kupokea.
Acha mzaha ndugu.
 
Wasalamu ndugu zangu,

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyosomeka, mimi kwangu napenda kumleta kwenu His Ex. John Pombe Magufuli, Rais wetu wa jamhuri ya Muungano Tanzania kama nominee katika ushujaa wa upambanaji wa rushwa hapa afrika.

Tumpe sapoti mkuu wetu wa nchi azidi kuyatenda yale yaliyomema kwetu.

Kataa rushwa.. usitoe,usishawishi wala kupokea.
May be he is a hero coz he is not a "nepotist"
 
Amejiondoa kwenye mkataba wa kuendesha serikali kwa Uwazi halafu unasema anapambana na ufisadi?. ufisadi unapiganwa gizani?

Hakuna high profile political leader au Katibu mkuu au mwanasheria mkuu aliyefikishwa mahakamani mpaka sasa kujibu tuhuma za mikataba mibovu au matumizi mabaya ya fedha za umma, Huo ufisadi anaoupigia kelele majukwaani utaondoka kwa maneno tu?

CAG alilirudisha suala la Lugumi kuwa bado hajatoa huduma stahiki kulingana na pesa aliyopewa, Huyo Lugumi amechukuliwa hatua gani?

Kanunua ndege bila pesa kuidhinishwa na bunge na pia Shirika la ATCL kalihamishia ofisini kwake ili lisikaguliwe na CAG, sasa hapo anapambanaje na ufisadi?

It seems jamaa ni bingwa wa kupambana na ufisadi kwenye speech lakini siyo kwenye Actions
 
siku zote mtu akitoa maamuzi wakati wa shida anakuwa anaropoka tu, naona hiyo post yako ni mafano halisi (wa kuropoka eti hata ukatwe mikono humpigii kura)wa kufundishia UD. Shida zipo ila usije na hukumu za kishida shida, utamaduni TZ uko wazi ndani ya chama na hata serikalini so far win first term get a second term for free. Usijichatue akili

Hatuwezi kubadili sheria za mchezo katikati ya mchezo wenyewe, you may hate him but the rule of the game knows nothing but the rule itself.
 
Hivi utamaduni, desturi Na katiba kipi kipo juu! Ccm Ni chama kikongwe lakini kinaendeshwa kimizengwemizengwe sana.
 
1568898564458.png


SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imevunja rekodi kwa kuunganishia umeme wananchi 949,000 kwa kipindi cha miaka mitatu, ikilinganishwa na idadi ya wananchi milioni 1.3 waliounganishiwa huduma hiyo miaka 50 iliyopita baada ya Uhuru.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alipokuwa akizindua uwashaji umeme kwenye kitongoji cha Kisasa, kata ya Tambani, wilaya ya Mkuranga na kueleza kuwa, lengo ni kuhakikisha umeme unamfikia kila mwananchi.

Alisema idadi hiyo imefikiwa kupitia miradi mbalimbali ya umeme ikiwamo inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Ujazilizi na Tanesco, lengo likiwa ni kuwafikia wananchi wote wa Tanzania ifikapo 2021. “Awamu hii ya tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria wananchi wote kupata nishati ya umeme kwani umeme ni maendeleo na kwa miradi mingi ambayo inaendelea malengo ya nchi nzima yatafikiwa ifikapo 2021,” alisema Mgalu.

Alisema mradi wa umeme katika miji iliyo pembezoni ambao utawafikia wananchi 4,293 wa awali, Tanesco imetenga kiasi cha Sh bilioni 3.3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020. “Mradi huu utavifikia vijiji 11 na vitongoji 30, ambapo REA Awamu ya Tatu mzunguko wa pili utaanza Desemba, mwaka huu na mradi wa Ujazilizi awamu ya pili utahusisha mikoa tisa,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdala Ulega, alisema wakati anaingia kwenye nafasi hiyo umeme ulikuwa katika vijiji visivyozidi 10, lakini kwa sasa vimefika vijiji 43. Alisema licha ya vijiji hivyo kuwa na umeme katika kata za Panzuo, Visegese, Njianne, Kitomondo, Magawa, Bupu na Mchonga, lakini pia mwaka huu huduma hiyo itapelekwa katika vijiji na kata zote.

Kwa upande wake, Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mkuranga, Octavian Mmuni, alisema umeme uliowekwa kwenye kata ya Tambani una njia kubwa ya kilometa sita na njia ndogo yenye urefu wa kilometa 11 na utawafikia watu 101 ambao wameshalipia. Alisema mradi huo una thamani ya zaidi ya Sh milioni 400 na umefikia asilimia 96.
 
Mwanzoni nilitafakari sana kama hii falsafa ya Hapa Kazi Tu inaweza kufua dafu kwa ile iliyozoeleka ya Kazi na Bata.

Kiukweli wananchi kwa ujumla wao wanachapa kazi isipokuwa wanasiasa wachache walionuna baada ya mirija yao ya dili kuzibwa.

Ziko wapi zile mbwembwe za wanasiasa vijana waliokuwa wanakula bata tu bila kufanya kazi?

Wapinzani je bado wana hoja kufuatia kazi kubwa za maendeleo zinazoendelea kufanyika katika awamu hii?

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
 
AHSANTE RAIS WETU
Serikali inajenga vihenge 12 kwa gharama ya shilingi Bilioni 23.4 kwa ajili ya kuhifadhi mahindi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. • Vihenge hivi vitaongeza uwezo wa kuhidhi mahindi kutoka tani 29,000 hadi 84,000.

IN MAGUFULI AND SHEIN WE TRUST
Vitalis Konga

vitalisikonga83@gmail.com
0717354277
 
AHSANTE RAIS WETU
Serikali inajenga vihenge 12 kwa gharama ya shilingi Bilioni 23.4 kwa ajili ya kuhifadhi mahindi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma. • Vihenge hivi vitaongeza uwezo wa kuhidhi mahindi kutoka tani 29,000 hadi 84,000.

IN MAGUFULI AND SHEIN WE TRUST
Vitalis Konga

vitalisikonga83@gmail.com
0717354277
Nadhani wewe ni Lumpen, tena proletaria, short of that usingeliweza kuandika nonsense kama hii! au ni mnafiki wa njaa kama akina bana!
 
Mkuu karibu nikuelewe. Vihenge 12 kwa bilioni 23.4. Sawa na takriban bilioni mbili kila kimoja! Mkuu anacheza kama Messi.
 
Back
Top Bottom