Kwanza una matatizo mawili ya msingi.
1.Wewe ni mshamba, na kutokana na ushamba wako unaona kilichofanyika Ubungo ni kama muujiza na unadhani hakijawahi kufanyika mahali pengine duniani.
Wakati ukweli ni kwamba kwa mji kama dar, kilichofanyika hakifanani na interchange katika miji na majiji ya nchi za wenzetu. Lakini wewe nakufanananisha na hadithi ya kipofu ambaye hakuwahi kuona kabisa katika maisha yake, lakini siku moja akafunuliwa na kubahatika kumuona mbwa kwa dakika moja kisha upofu ukamrudia. Basi toka siku hiyo ikawa kila akifika mahali watu wanapiga stori kusifia kitu kizuri au kikubwa basi yeye akawa akiuliza hicho kitu kinaweza kuwa kizuri au kikubwa kumzidi mbwa? Hata hivyo hakuwa na makosa maana maishani mwake hakuwahi kuviona vitu vingine zaidi ya mbwa. Ni sawa na wewe kwasababu hujawahi kuona interchange yoyote zaidi ya hiyo ya ubungo hivyo kwako unaona huo ni muujiza.
2.Hujui wajibu wa serikali ni nini. Kwako wewe unaona serikali ikifanya kitu ni kama hisani.
Hapa kinachokusumbua ni ukosefu wa elimu ya uraia.
Jielimishe.