Rais Samia atakapokuwa anamaliza muhula wake mwaka 2030 tutamkumbuka kwa mengi sana,Tutapiga magoti na kutembelea magoti chini kumshukuru kwa kazi kubwa na yakipekee sana aliyoifanyia nchi na Taifa letu. Mpaka sasa amefanya yafuatayo japo nitaeleza machache kati ya mengi.
Rais Samia katika kuinua maisha ya watanzania na kuacha alama isiyo futika katika mioyo yao kutokana na kuandikwa kwa wino wa Dhahabu amefanya jambo la kishujaa sana,kwanza kwa kutambua ya kuwa asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima akaamua kuweka mikono yake na nguvu yake kwa kutoa Ruzuku ya Billion mia moja hamsini katika pembejeo hasa mbolea ,hali iliyopelekea kushuka kwa bei ya mbolea sokoni,mfano mbolea ya DAP iliyokuwa inauzwa kwa laki na 40 ikaanza kupatikana kwa Elfu 70 Tu. Hatua hii kwa hakika ni alama ambayo haitafutika katika mioyo ya watanzania wakulima .kwani watanzania watakumbuka siku zote kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo kilimo kikawa mkombozi wa maisha yao,ni wakati wa Rais samia ambapo wakulima wengi waliaga umaskini,Ni wakati wa Rais samia ambapo kilimo kikaanza kukimbiliwa na wasomi hasa vijana,ni wakati wa Rais samia ambapo wakulima walianza kujenga nyumba bora na za kisasa.Hii ni baada ya bei ya mazao kuwa nzuri kutokana na masoko ya mazao kuwa ya uhakika baada ya Rais samia kuimarisha Diplomasia yetu na kufanya Watanzania kupata masoko nje ya nchi.
Watumishi wa umma nao kwa machozi ya furaha watahadithia na kusimulia kwa uchungu mkubwa kuwa ni wakati wa samia ndipo walipoanza kuona wakipandishwa madaraja na kupewa stahiki zao,ni wakati wa Rais samia ndipo walipopandishiwa mishahara kwa 23% hasa wale wa kima cha chini,Ni wakati wa Rais samia ndipo watumishi wa umma walipoanza tena kupewa nyongeza ya mshahara ya kila mwaka,ni wakati wa Rais samia ndipo walipoanza kulipwa malimbikizo ya madeni yao,ni wakati wa Rais samia ndipo walipoanza kuheshimika na kuthaminiwa mchango wao katika ujenzi wa Taifa lao na Ni wakati wa Rais samia walipoanza kusikilizwa na serikali yao.
Vijana mbalimbali kwa upole na unyenyekevu watasimulia kuwa ni wakati wa Rais samia ndipo walipobahatika kupata ajira serikalini na kuinua na kuamsha matumaini yao kwa familia zao,Ni wakati wa Rais samia ambapo walipata mikopo mingi sana kupitia halmashauri zao,ni wakati wa Rais samia ambapo walifungua biashara nyingi pasipo kulipa mapato mpaka upite mwaka mmoja wa kukua na kusimama kibiashara,ni wakati wa Rais samia ambapo vijana walianza kupewa kipaombele katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kupata ajira.
Wazazi watawasimuliwa watoto wao kuwa ni wakati wa Rais samia walisaidiwa mzigo na gharama za kusomesha baada ya serikali ya Rais samia kutoa Elimu bure hadi kidato cha sita na kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa kila mwanafunzi mwenye sifa,ni wakati wa Rais samia ambapo watoto wao waliohangaika kwa miaka mingi walipoanza kupata ajira serikalini na kuwasaidia wazazi wao.
Watanzania watakumbuka na kumkumbuka Rais samia kuwa ni wakati wake ambapo wanafunzi wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza walipoanza kuripoti wote kwa wakati mmoja kutokana na serikali ya Rais samia kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu ishirini Nchini.ni wakati wa Rais samia ambapo shule zilijengwa kwa ubora utafikiri tupo ulaya huku zikiwa zimewekwa madirisha ya aluminium.
Wafanyabishara nao pia watamkumbuka Rais samia na kusema kuwa ni wakati wake ambapo walifanya biashara kwa uhuru,walikuwa huru kuweka hela benki bila hofu ya kuchotewa fedha zao pasipo utaratibu wa kisheria na kibenki,watasema kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo mzunguko wa fedha na biashara ulikuwa mzuri na biasht zilifanyika vizuri mpaka kupelekea wao kulipa mapato pasipo shida wala wasiwasi.
Wanafunzi wa vyuo vikuu watamkumbuka mama yao kuwa ni yeye ndiye aliyefanya uamuzi wa kijasiri wa kuanza kuwapa shilingi Elfu kumi kila siku kama fedha ya kujikimu,na hivyo kuongeza hamasa ya kujisomea kwa utulivu.
Wanasiasa na wanaharakati na wananchi mbalimbali watamkumbuka Rais samia na kusema ni wakati wake ambapo demokrasia ilikalia kiti chake na kutoa uhuru kwa kila mtu kuzungumza chochote kile pasipo hofu wala wasiwasi ,waandishi wa habari watasema ni wakati wa Rais samia ambapo wakiweza kuandika habari na kutangaza habari pasipo uoga wa aina yoyote ile.
Watanzania watasema ni wakati wake ambapo waliishi kwa furaha na viwango vya furaha vikiongezeka nchini kutokana na uongozi wa Rais samia kuwagusa na kuwainua kiuchumi,ni wakati wake ambapo uchumi ulionekana kukua katika mifuko ya watanzania na ni wakati wake ambapo yeyote mwenye kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa aliweza kujipatia kipato pasipo shida yoyote ile.
Nitaendelea baadaye au kesho panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu ngoja nipumzike kidogo.