Mafanikio ya Rais Samia kwa 3 years ni yapi? Nijue nikae sawa

Mafanikio ya Rais Samia kwa 3 years ni yapi? Nijue nikae sawa

Rais Samia atakapokuwa anamaliza muhula wake mwaka 2030 tutamkumbuka kwa mengi sana,Tutapiga magoti na kutembelea magoti chini kumshukuru kwa kazi kubwa na yakipekee sana aliyoifanyia nchi na Taifa letu. Mpaka sasa amefanya yafuatayo japo nitaeleza machache kati ya mengi.

Rais Samia katika kuinua maisha ya watanzania na kuacha alama isiyo futika katika mioyo yao kutokana na kuandikwa kwa wino wa Dhahabu amefanya jambo la kishujaa sana,kwanza kwa kutambua ya kuwa asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima akaamua kuweka mikono yake na nguvu yake kwa kutoa Ruzuku ya Billion mia moja hamsini katika pembejeo hasa mbolea ,hali iliyopelekea kushuka kwa bei ya mbolea sokoni,mfano mbolea ya DAP iliyokuwa inauzwa kwa laki na 40 ikaanza kupatikana kwa Elfu 70 Tu. Hatua hii kwa hakika ni alama ambayo haitafutika katika mioyo ya watanzania wakulima .kwani watanzania watakumbuka siku zote kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo kilimo kikawa mkombozi wa maisha yao,ni wakati wa Rais samia ambapo wakulima wengi waliaga umaskini,Ni wakati wa Rais samia ambapo kilimo kikaanza kukimbiliwa na wasomi hasa vijana,ni wakati wa Rais samia ambapo wakulima walianza kujenga nyumba bora na za kisasa.Hii ni baada ya bei ya mazao kuwa nzuri kutokana na masoko ya mazao kuwa ya uhakika baada ya Rais samia kuimarisha Diplomasia yetu na kufanya Watanzania kupata masoko nje ya nchi.

Watumishi wa umma nao kwa machozi ya furaha watahadithia na kusimulia kwa uchungu mkubwa kuwa ni wakati wa samia ndipo walipoanza kuona wakipandishwa madaraja na kupewa stahiki zao,ni wakati wa Rais samia ndipo walipopandishiwa mishahara kwa 23% hasa wale wa kima cha chini,Ni wakati wa Rais samia ndipo watumishi wa umma walipoanza tena kupewa nyongeza ya mshahara ya kila mwaka,ni wakati wa Rais samia ndipo walipoanza kulipwa malimbikizo ya madeni yao,ni wakati wa Rais samia ndipo walipoanza kuheshimika na kuthaminiwa mchango wao katika ujenzi wa Taifa lao na Ni wakati wa Rais samia walipoanza kusikilizwa na serikali yao.

Vijana mbalimbali kwa upole na unyenyekevu watasimulia kuwa ni wakati wa Rais samia ndipo walipobahatika kupata ajira serikalini na kuinua na kuamsha matumaini yao kwa familia zao,Ni wakati wa Rais samia ambapo walipata mikopo mingi sana kupitia halmashauri zao,ni wakati wa Rais samia ambapo walifungua biashara nyingi pasipo kulipa mapato mpaka upite mwaka mmoja wa kukua na kusimama kibiashara,ni wakati wa Rais samia ambapo vijana walianza kupewa kipaombele katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kupata ajira.

Wazazi watawasimuliwa watoto wao kuwa ni wakati wa Rais samia walisaidiwa mzigo na gharama za kusomesha baada ya serikali ya Rais samia kutoa Elimu bure hadi kidato cha sita na kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa kila mwanafunzi mwenye sifa,ni wakati wa Rais samia ambapo watoto wao waliohangaika kwa miaka mingi walipoanza kupata ajira serikalini na kuwasaidia wazazi wao.

Watanzania watakumbuka na kumkumbuka Rais samia kuwa ni wakati wake ambapo wanafunzi wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza walipoanza kuripoti wote kwa wakati mmoja kutokana na serikali ya Rais samia kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu ishirini Nchini.ni wakati wa Rais samia ambapo shule zilijengwa kwa ubora utafikiri tupo ulaya huku zikiwa zimewekwa madirisha ya aluminium.

Wafanyabishara nao pia watamkumbuka Rais samia na kusema kuwa ni wakati wake ambapo walifanya biashara kwa uhuru,walikuwa huru kuweka hela benki bila hofu ya kuchotewa fedha zao pasipo utaratibu wa kisheria na kibenki,watasema kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo mzunguko wa fedha na biashara ulikuwa mzuri na biasht zilifanyika vizuri mpaka kupelekea wao kulipa mapato pasipo shida wala wasiwasi.

Wanafunzi wa vyuo vikuu watamkumbuka mama yao kuwa ni yeye ndiye aliyefanya uamuzi wa kijasiri wa kuanza kuwapa shilingi Elfu kumi kila siku kama fedha ya kujikimu,na hivyo kuongeza hamasa ya kujisomea kwa utulivu.

Wanasiasa na wanaharakati na wananchi mbalimbali watamkumbuka Rais samia na kusema ni wakati wake ambapo demokrasia ilikalia kiti chake na kutoa uhuru kwa kila mtu kuzungumza chochote kile pasipo hofu wala wasiwasi ,waandishi wa habari watasema ni wakati wa Rais samia ambapo wakiweza kuandika habari na kutangaza habari pasipo uoga wa aina yoyote ile.

Watanzania watasema ni wakati wake ambapo waliishi kwa furaha na viwango vya furaha vikiongezeka nchini kutokana na uongozi wa Rais samia kuwagusa na kuwainua kiuchumi,ni wakati wake ambapo uchumi ulionekana kukua katika mifuko ya watanzania na ni wakati wake ambapo yeyote mwenye kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa aliweza kujipatia kipato pasipo shida yoyote ile.

Nitaendelea baadaye au kesho panapo majaliwa ya mwenyezi Mungu ngoja nipumzike kidogo.
Samia hoyeeeeeeeee!

Na mimi nampongeza pia kwenye swala la kikokotoo cha mafao.
 
Shida yenu hamjui mlitakalo. Mkienda huko vijijini kwenu mkiamua hata kuangalia majengo ya shule aliyowajengea inatosha kupima mafanikio ya Samia. Ila ndo hivyo Chuki ni ugonjwa mkubwa sana.
 
By the way SAMIA ukimlinganisha na mtangulizi wake-Magufuli,SAMIA ana mafanikio mengi zaidi.
1.Democracy
2.Uchumi
Uchumi upi? Mtaani zero
Hata kwenye karatasi zero

Bank ya dunia imetuondoa kutoka uchumi wa kati alipoachia jpm mpaka nchi masikini


Democracy inakusaidia nini? Kama watu hawashibi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jobless wanaongezeka tu mtaani, Uwekezaji wa hifadhi za Ngorongoro, Mpango wa kuwekeza bandari za Tanganyika. Safari na matamasha yanaongezeka Tanganyika. Ukaguzi wa sare za jeshi mtaani. SSM oyee
 
Katoa jobless wachache mtaani tatizo lililotengenezwa na mtangulizi wake
 
I will be short,

Naomba watu wanipe . Mafanikio ya mama. Kwamba Leo akitoka tutamkumbuka ?? kwa kuweka maisha ya mtanzania kuwa mepesi?
1. Kawa Daktari
2. Yanga imefika fainali
3. Taifa stars imeenda Afcon finals
4. Kauhuru ka kuongea kameongezeka
5. Nyongeza za mishahara
6. Sisi wengine tumerudishiwa upigaji
7. Masai wamehamishwa ngorongoro
 
Taifa liko kwenye shida kuu kama zilivyoorodheshwa hapa
 

Attachments

  • IMG-20230910-WA0001.jpg
    IMG-20230910-WA0001.jpg
    65.9 KB · Views: 2
I will be short,

Naomba watu wanipe . Mafanikio ya mama. Kwamba Leo akitoka tutamkumbuka ?? kwa kuweka maisha ya mtanzania kuwa mepesi?
Kwani haujashuhudia timu za Yanga, Simba na Taifa Stars zikishushiwa maburungutu instant yaani hapohapo uwanjani hata kukiwa na giza! Hata marekani hawajawahi kumudu.
 
I will be short,

Naomba watu wanipe . Mafanikio ya mama. Kwamba Leo akitoka tutamkumbuka ?? kwa kuweka maisha ya mtanzania kuwa mepesi?
Ajira lukuki both serikalini na private sector iliyokufa kipindi Cha jpm. Miradi mipya mingi na ya zamani kumalizea japo ilikuwa wastage of resources. Nchi Ina demokrasia kubwa ambapo jpm alifunga mikutano yote ya vyama vya upinzani akaruhusi ya ccm halafu akajigamba ccm inapendwa wakati mshindani kafungiwa kabati.

Uchumi ambao ni transparent siyo Yale mauongo ya jpm eti tumeingia uchumi wa kati.

Mikataba kuwa wazi tena kupelekwa bungeni wakati kipindi Cha jpm ilikuwa haiwezekani kabisa mkataba hata mmoja kuwa wazi au tenda yoyote kuwa wazi mfano ununuzi wa ndege.

Nikiorodhesha mafanikio yote nadhani hii platform haitoshi
 
I will be short,

Naomba watu wanipe . Mafanikio ya mama. Kwamba Leo akitoka tutamkumbuka ?? kwa kuweka maisha ya mtanzania kuwa mepesi?
Ajira lukuki both serikalini na private sector iliyokufa kipindi Cha jpm. Miradi mipya mingi na ya zamani kumalizea japo ilikuwa wastage of resources. Nchi Ina demokrasia kubwa ambapo jpm alifunga mikutano yote ya vyama vya upinzani akaruhusi ya ccm halafu akajigamba ccm inapendwa wakati mshindani kafungiwa kabati.

Uchumi ambao ni transparent siyo Yale mauongo ya jpm eti tumeingia uchumi wa kati.

Mikataba kuwa wazi tena kupelekwa bungeni wakati kipindi Cha jpm ilikuwa haiwezekani kabisa mkataba hata mmoja kuwa wazi au tenda yoyote kuwa wazi mfano ununuzi wa ndege.

Nikiorodhesha mafanikio yote nadhani hii platform haitoshi
 
Back
Top Bottom