Mafanikio ya Royal Tour yaanza kuonekana kwa kasi ya kutisha, Hongera Rais Samia

Mafanikio ya Royal Tour yaanza kuonekana kwa kasi ya kutisha, Hongera Rais Samia

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Leo gazeti za Citizen limeripoti mawakala wa Utalii kutoka Nchini Marekani wameingia Tanzania kujionea vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini Kwa ajiri ya kuwaleta Wamarekani. Hii ni wiki chache tu tangu Rais Samia Suluhu Hassan afanye kipindi maarufu duniani kinachohusiana na utalii na fursa za uwekezaji cha The Royal Tour.

Ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii na fursa nyingi za uwekezaji, Tanzania imekuwa nyuma sana katika kupokea watalii wengi hapa Africa Kwa kupokea watalii chini ya Milioni 2 kwa mwaka. Hili limekuwa linatokea huku sekta ya utalii ikiwa ndo sekta inayochangia kwa Kiwango kikubwa zaidi pato la Taifa kabla ya kutokea Kwa janga la corona!

Kwa mafanikio haya makubwa yanayoanza kuonekana katika sekta ya utalii Tanzania inaweza kufikisha watalii Mil 5 ifikapo mwaka 2025 na pato la Taifa kukua kwa kiwango cha kutisha.

Hongera sana Rais Samia kwa Ubunifu wa kufanya program ya Royal Tour na hakika The future is now promising for Tanzania.

Go Samia! Go Tanzania

77EC0564-BFC9-4639-BAC6-09EB441A49F0.jpeg
 
"to sample tourist attractions" sijui umeelewa?
Hao matapeli wanakuja kutalii bure.

Unamkumbuka yule black Amerika alimwambia Mwakyembe anakuja kujenga tren ya juu Dar?? mpaka Mwakyembe akamuita "huyu baba"
 
"to sample tourist attractions" sijui umeelewa?
Hao matapeli wanakuja kutalii bure.

Unamkumbuka yule blach Amerika alimwambia Mwakyembe anakuja kujenga tren ya juu Dar?? mpaka Mwakyembe akamuita "huyu baba"
Pingapinga Fc tumeshawazoea! Nyie kila kitu kupinga na kuzua nadharia zenu!
 
Acha uongo wewe!!!

Leo gazeti za Citizen limeripoti mawakala wa Utalii kutoka Nchini Marekani wameingia Tanzania kujionea vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini Kwa ajiri ya kuwaleta Wamarekani. Hii ni wiki chache tu tangu Rais Samia Suluhu Hassan afanye kipindi maarufu duniani kinachohusiana na utalii na fursa za uwekezaji cha The Royal Tour....
 
Makampuni ya utalii yamekuwa yakifanya kazi na agents walioko nchi mbali mbali, na hao agents wamekuwa wakija nchini mara kibao tokea zamaniiiii. Hakuna jipya hapo
 
Watalii wamekua wakija mara zote ila tukubali Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza wigo kwa kusimama kuitangazi nchi
Royal Tour ndo kipimo kikuu linapokuja suala la nchi kujitangaza. Baada ya hapo hata watu wakiona Visit Tanzania au Tanzania Unforgettable watakuwa wanajua ni Tanzania ipi inayozungumzwa.

Ndo mana Visit Rwanda ilikuja baada ya Kagame kufanya Royal Tour.

The future is really promising!
 
Back
Top Bottom