Mafanikio ya Royal Tour yaanza kuonekana kwa kasi ya kutisha, Hongera Rais Samia

Hiyo Royal Tour haijaonyeshwa popote pale mara imeshaanza kuzaa matunda!!! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hujui kuwa kipindi kikianza kutengenezwa tu tour agents huwa wanapata taarifa huko duniani! Sasa wanafanya kukamata fursa ili kipindi kikirushwa tu wawe na bookings tayari?

Tatizo mmekulia ushambani mambo yanavyoenda duniani hamjui
 
Hiyo Royal Tour haijaonyeshwa popote pale mara imeshaanza kuzaa matunda!!! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hahaha haha nimecheka kwa sauti, royal tour itatukomesha kila atakaye kuja sasa hivi tutaambiwa ni matunda ya royal tour.
 
Makampuni ya utalii yamekuwa yakifanya kazi na agents walioko nchi mbali mbali, na hao agents wamekuwa wakija nchini mara kibao tokea zamaniiiii. Hakuna jipya hapo

Ingefaa Sana tuwe mabalozi wa kimataifa kupitia hao maagent kuliko kuwa na hawa mabalozi wa utalii wa ndani ya nchi....
 
Ndo ujue ni kwa jinsi gani hiki kipindi kinaleta matokeo! Hapo hakijarushwa tu hali iko hivi watu wanakuja kuchangamkia fursa! Je kikirushwa hali itakuwaje?
Wewe una idea yoyote ile ya utalii?
 
Nafikiri wewe unatatizo la kutoelewa kitu gani wamekuja kufanya.

Digest this in-depth and come out with an objective opinion "...to sample tourist attractions..."

Kwanza haamini kilichotangazwa mpaka wahakiki kwenye uhalisia ndio maana wanakuja kuona na kuanisha vivutio vifaavyo kwao kuhamasishwa na kuvutiwa
 
Reactions: PNC
Mwenye Tatizo ni mimi au wewe?
Tatizo mmekalia ushamba na ndo mana unawapa shida!
Hao wanajua kuwa Tanzania tumetoka kurekodi Royal Tour, wanajua kuna soko kubwa la utalii linakuja kwa Tanzania.

Wanachofanya wanakuja kuweka mikataba na makubaliano na ma hoteli makubwa kwa sababu wanajua soon booking za kuja Tanzania zitakuwa nyingi kwao.

Kataa au kubali ni matokeo ya The Royal Tour
 
"to sample tourist attractions" sijui umeelewa?
Hao matapeli wanakuja kutalii bure.

Unamkumbuka yule black Amerika alimwambia Mwakyembe anakuja kujenga tren ya juu Dar?? mpaka Mwakyembe akamuita "huyu baba"
Dr. Shumake🀣
 
Kuna jamaa alileta uzi humu kulalamika kwamba alidhani kwamba ukienda kutalii mbugani utawakuta wanyama wameshonana hapo na kuanza kuangalia na kuchukua selfie, badala yake ikawa ni kutafuta huku na kule......sasa waambieni wazungu kabisa, maana wao wanajua wanyama wapo kila mahali na wametapakaa kwenye makazi ya watu. Ukimwambia mzungu unatokea serengeti anaweza kuduwaa namna ulivyofanya hadi ukafanikiwa kuishi na wanyama pori....
 
Alienda mbuga gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…