Mafanikio ya TARURA, Yaibeba TAMISEMI na Kumng'arisha Rais Samia, Speed Iliendelea Hivi, 2025 Hatahitaji Kupiga. Itakuwa ni "Anameremeta"

Mafanikio ya TARURA, Yaibeba TAMISEMI na Kumng'arisha Rais Samia, Speed Iliendelea Hivi, 2025 Hatahitaji Kupiga. Itakuwa ni "Anameremeta"

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi

Nimepata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Vijijini, deep interior, nikashangaa sana kukuta Barabara za lami hadi Vijijini.

Kuulizia nikaelezwa ni kazi nzuri ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini, TARURA baada tuu ya Mama Samia kushika nchi, ame I double na ku triple bajeti ya TARURA kwa karibu mara 3.

Nilipofuatilia majadiliano ya Bungeni kwenye Bajeti ya TAMISEMI, kiukweli Mafanikio ya TARURA, Yaibeba TAMISEMI na kumng'arisha sana Rais Samia, kama kasi ya uchapakazi wa TARURA utaendelea Kwa speed hii alioanza nayo Mama Samia kwenye huu mwaka wake wa kwanza, na ikiendelea hivi, hadi, 2025, then ikitokea 2025, Watanzania tumeamua tunakwenda na Mwanamke, na Mwanamke mwenyewe akawa ni Mama Samia, amini usiamini, kuna baadhi ya maeneo, Mama Samia hatahitaji kufika kufanya kampeni, ni kupitishia bango lenye picha ya Mama Samia, akiwa amepunga mkono na wananchi hao kuwaambia, huyu kwenye picha hii anawasalimia, aliwatumia salamu zake kupitia TARURA, na kuwauliza "Jee Mlizipata?" (huku unanyua juu hilo bango lenye picha ya Samia akipunga mkono akiwa anatembea kwenye Barabara ya lami ya Vijijini iliyojengwa na TARURA), badala ya wananchi hao kujibu kuwa salaam za TARURA ziliwafikia, mtashangaa Tu kusikia kina mama wanaimba "Anameremeta...
Anameremeta...x2
Samia Anameremeta,
Anameremeta...

Yaani kazi nzuri ya TARURA, itammeremetisha Samia 2025 just incase ni yeye Samia atakuwa ndiye aliyepangiwa na YEYE.

Shuhudia

Kiukweli mimi nimeguswa sana na kazi nzuri ya TARURA, hivyo kuna makala hii, Nipashe la Leo
Screen Shot 2022-05-15 at 7.25.25 PM.png

Screen Shot 2022-05-15 at 6.16.08 PM.png

Paskali
 
Unaweza kututajia hivyo vijiji kwa idadi na walau picha ya hizo lami?

Na je kazi ya TARURA ni kumng'arisha au kumfurahisha rais?

Je watu hao kupata lami sio kwamba ndio matunda ya kodi zao?
 
Kazi nzuri ,japo kuna kazi kubwa inahitajika kuweka viraka barabara nyingi mijini Na vijijini zina mashimo sana japo ni za lami,pia kuunganisha wilaya Na wilaya kuna baadhi ya mikoa kwenda wilayani ni masaa 12 ... na wilaya haina barabara ya uhakika kuiunganisha .... utazani imetengwa! Hii niliiona Lindi huko hatari sana mnakaa porini siku mbili bana
 
Alokwambia sisi tunataka barabara Nani wakati elfu 10 imekuwa sawa na buku..?

Sisi tunataka bidhaa zipatikane kwa bei nzuri na sio kama ilivyo sasa

Mafuta Lita 9000?
Nani atafurahia barabara?

Acheni uzwazwa Nyie CCM
 
Kazi ya Magu hiyo, hiyo ni intellectual theft mnayofanya, Tanzania ingekuwa ni Kampuni tungewashitaki!
 
Ccm haitegemei kura acha upotoshaji usio na tija yoyote. Magufuli ndio alipiga propaganda mpaka wananchi wakadhani Tanzania ni peponi, lakini hakuna uchaguzi uliokuwa wa kihayawani kama enzi zake.
 
Pascal ...Naona watu Wana hasira na CCM lakini kimoyo moyo wanakubali Mama ana upiga mwingi.....kuna utulivu sana... trillion 5 zitakazoingia kwenye uchumi kwa nyongeza na posho zitaleta impact kubwa
 
Nimetamani kukuuliza picha na majina ya vijiji vyenye hizo lami nikaamua kukuhifadhi kwa leo tu sikuulizi maana rangi yetu ni moja ila siku ingine sitakubali siasa na propaganda bila ushahidi wa picha bado nasherehekea goli la Feisaaaaaaaaalll
 
Pascal ...Naona watu Wana hasira na CCM lakini kimoyo moyo wanakubali Mama ana upiga mwingi.....kuna utulivu sana... trillion 5 zitakazoingia kwenye uchumi kwa nyongeza na posho zitaleta impact kubwa
Mkuu The Boss , hakuna kitu kizuri kama kuukubali ukweli jinsi ulivyo, hizo hasira ni za muda tuu, trillion 5 zikiisha tua kwenye circulation, watamkubali wenyewe, na 2025, kama ni yeye aliyepangiwa na YEYE, then hahitaji kupiga kampeni, yeye ni kupita tuu na kupunga mkono, na kuwashukuru wananchi in advance, kazi iendelee itakuwa imemsafishia njia.
P
 
Nimetamani kukuuliza picha na majina ya vijiji vyenye hizo lami nikaamua kukuhifadhi kwa leo tu sikuulizi maana rangi yetu ni moja ila siku ingine sitakubali siasa na propaganda bila ushahidi wa picha bado nasherehekea goli la Feisaaaaaaaaalll

Karibu
P
 
Pascal ...Naona watu Wana hasira na CCM lakini kimoyo moyo wanakubali Mama ana upiga mwingi.....kuna utulivu sana... trillion 5 zitakazoingia kwenye uchumi kwa nyongeza na posho zitaleta impact kubwa
Uhuru wa watu una thamani kubwa kuliko kitu chochote.

Kwa mfumo halisi wa nchi yetu ilivyo mama atuachie tuchaguwe Wabunge na madiwani tunaowataka, Bado kwa Uchaguzi huu kuitowa CCM jumla after Magufuli effect ni jambo lisilowezekana.
 
Back
Top Bottom