Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kuwa wa kwanza kuzaliwa hakika ni mapambano makubwa sana,kwasababu moja kwa moja unajikuta majukumu yanakuandama kwa namna moja au nyingine
Hawa watu wanajitoa sana kuokoa jahazi lisizame katika familia,tena katika hizi familia zetu ambazo bado hazija jipata hakika mafirst born wanajitoa sana kwa kupenda au kwa kutokupenda,na watafanyaje angali wanategemewa wao
Ni mara nyingi unawakuta hawa watu wanashindwa kufanya mambo yao ya maendeleo kwasababu wapo pale kusapoti familia zao na wadogo zao,kwahiyo next time ukimuona first born hajajenga au kujiimarisha kiuchumi basi tambua ana mzigo mkubwa wa ndugu na jamaa wanamtegemea
Najua kuna baadhi mtasema hayo sio majukumu yake,bali majukumu yake ni kuangalia watoto wake na familia yake,nasema hivi kwa mtu ambaye anajitambua hawezi acha wazazi wake au ndugu ambao wanahitaji msaada kisha akawapuuza,hilo haliwezekani kwasababu hao ni jamaa zake na watu wake wa karibu
Kwao wao kuwaona ndugu zao wanaenda shule kwa msaada wao ni faraja kubwa sana,kuwaona ndugu zao wanapata mkate wao wa kila siku ni jambo lenye kuwapa faraja sana,kuiona familia inatabasamu ni jambo lenye kuwapa amani katika nyoyo zao
Mafirst born aluta continua kama mlivyoanza na ndio mtakavyo maliza,daima endeleeni kushow love kwa ndugu jamaa na marafiki,mmezaliwa wa kwanza kwakuwa mna mission hapa duniani,nyie ni viongozi,na sifa kubwa ya kiongozi ni kutatua shida za ndugu zake na jamaa zake
Kiongozi siku zote huwa baina ya shida za watu wake na kutafuta namna ya kuzitatua au kama sio kuzipunguza,haukuwa mzaliwa wa kwanza kwa bahati mbaya bali ili upambanie jamii yako
Nafahamu huwa mnajitoa sana kwa ajili ya ndugu hata wakati mwingine mnakosa yale ambayo mnayapenda katika nafsi,nawapa moyo kwamba,hakika mnabadilisha maisha ya watu wengi sana,huenda msipate nafasi ya kuambiwa hayo lkn mfahamu kwamba juhudi zenu haziendi bure
Endeleeni kupambana mpaka tone la mwisho la damu
Ni hayo tu!