Mafisadi watashinda! - A somber look

kwa kweli you are right, mimi naamini hivyo hivyo dalili zote zinanyesha ushindi kwa mafisadi. my main reason ni kuwa huyu jamaa anaetutawala ameonekana kuwaogopa kabisa kwani hatoi tamko wala ushirikiano na nasisi tuliiompigia kura na kuwa na imani nae kwa ziada.

If regii is standing on his behalf as regi stated yesterday that his confidence comes frm this jamaa why doesnt he say a thing i believe hii ingesaidia au he is one of them au anawaogopa sasa itakuwaje kuwaogopa,

solution : angetumia mwalimu's strategies wafungie kizuizini, period. nchi itatulia na imani itarudi jamani uongozi ni dhamana mtaulizwa killa kitu kesho mbele ya mwenyewe fundi mangungu, kama hamwuwezi acheni, dhuluma kubwa inaendelea hapa.
 
Wametushinda sababu ndio hao hao tuliwafuata na bakuli wakati wa uchaguzi....
 

Mkuu hapo juu tuko ukurasa mmoja...........
 
Mkuu hapo juu tuko ukurasa mmoja...........

,.............................NAUNGA MKONO HOJA NA BAADA YA HAPO UAMUZI WA ZIPI ZIWE SIRI ZITANGAZWE KWA UMMA Kwamba taarifa kadha wa kadha ni siri kama hautaki waambiewe kwa kina ni kwa nini ziwe siri
 
,.............................NAUNGA MKONO HOJA NA BAADA YA HAPO UAMUZI WA ZIPI ZIWE SIRI ZITANGAZWE KWA UMMA Kwamba taarifa kadha wa kadha ni siri kama hautaki waambiewe kwa kina ni kwa nini ziwe siri

Nakubaliana na wewe. Lakini cha msingi kwangu mimi ni kuwa pawe na mtazamo wa hakuna siri ya daima. Mtu akijua kuwa anachokifanya ni lazima kitakuja kuona mwanga wa jua siku moja basi pengine atasita kufanya mambo mengine. Na vile vile watumishi na viongozi wote walazimike kutunza nyaraka na kumbukumbu zao.

Amandla.....
 
Fundi,

Ni mwanzo mzuri kuona kuna watu wanaliangalia hili jambo la ufisadi kwa mapana yake na solution na muda mrefu.

Nimeipenda analysis yako na kwa kifupi kama ulivyoweka abundantly clear suala ni system sio kambi kama ma-pundit wetu wa JF wanavyolazimisha watu iwe. Na hilo ndio kosa kubwa tunalofanya sasa kudhani adui yetu ni a,b & c n wakitoka hao na wakiingia z,y & z mambo yetu yatakuwa poa. Tunachosahau playing ground ni ile ile na rules ni zile zile na mwishoe matokeo yatakuwa ni yale yale!

Mifano uliyotoa ni tosheleza wenye macho na waone na wenye masikio na wasikie....
 

Tukianza na hayo uliyoyachanganua Mkuu Fundi.........sasa tuangalie sheria/katiba yetu inasemaje kuhusu hivyo vipengele...ili kujenga hoja mbele ya watunga sheria wetu
 

No retreat, no surrender


there is kusurrender. Screwed up for real.
 
Last edited by a moderator:
 
Kwa kifupi, hivi kweli unaamini kuwa Mengi akiwa Rais basi ufisadi utakwisha? Au Dr. Slaa? Bila kubadilisha system, temptation zitabaki pale pale.

- Kaangalie kule nyuma maelezo yangu kuhusu mabadiliko, nimesema bila kubadili katiba huwezi kuibadili Tanzania kutokea nje, ni lazima uingie ndani yaani ujiunge nao kwanza!
[/QUOTE]

- Kupandishwa mishahara ya wabunge ni debatable ishu, kuna wabunge wanaoweza kuonyesha facts kwamba wanahitaji kupandishiwa mishahara kwa sababu karibu hela zao zote huzitumia na wanajimbo wao, I have seen it na kuna wabunegw engine hawahitaji kupandishwa, sasa una-create vipi sheria ya baadhi tu ya wabunge? Huwezi kwa hiyo either wote wanyimwe au wapewe, nina experience ya kutosha na siasa za majimbo ya ubunge ndio maana ninaamini sana kwa 100% kwamba kuna wabunge wanahitaji kuongezwa mishahara na marupurupu, na wengine hawahitaji. Kwa hiyo mawazo yako kwamba kuomba nyongeza kwa wabunge ni dhuluma ni mbali sana na ukweli wa siasa za majimbo yetu ya ubunge!

- Personalities na the rest of the story ndio ile ile tabia yako ya personal huwezi kuchangia ishu bila personal, samahani mimi sihusiki na kubadilisha system yoyote na wala sio kiongozi wa system yoyote ya siasa, zaidi tu ya kampuni yangu ambayo hahitaji mabadiliko maana nimeijenga kwa jasho na damu yangu na kwa kufuata njia zinazotakiwa, haihitaji mabadiliko.

Respect.

FMEs!
 
Mapandekezo ya kubadili CCM na uchambuzi wa tatizo la CCM yamefanyika kwa miaka 30! Haja ya mabadiliko ya Katiba ni ya zamani kwa miaka 20, kwamba jinsi gani mambo yanaweza kuendeshwa kwa uwazi zaidi ni la kale tangu mwaka wa kwanza wa Mkapa.

Hakuna jipya! Na kwa mtindo huu tutaendelea kutoa mapendekezo bora zaidi miaka 20 ijayo na hali itaendelea kuwa ile ile huku kizazi kipya cha mafisadi kikiendelea kutawala bila kulala!

Kwamba njia bora ni hii au ile yameshasemwa na kujadiliwa hadi Bungeni! Walioko huko Bungeni na wengine wanayajua mapungufu ya Katiba kuliko sisi wengine; huko huko ndiko kuliko na maprofesa na wasomi wa kila fani! Kwenye hizo wizara zao wamejanzana watu wenye uchambuzi wa kisomi wa matatizo ya nchi yetu kwa miongo..

kwamba tatizo ni "system" hili nimelisikia tangu shule ya vidudu (chekechea!)..

So.. hakuna nilichosoma ambacho ni kipya. Kinazidi tu kuthibitisha kuwa mafisadi watashinda kwa mtindo huu wa kuchambuua na kupendekeza njia bora zaidi za kufanya mambo, njia ambazo zilishapendekezwa na baba na mama zetu! Gurudumu la kushindwa linaendelea kuzunguka!
 
 
Mjj na wengine poleni kwa tafakari hii chungu ila tusikate tamaa. Hiyo ndo sala yao na naamini watafanya kweli ila bado watawezashangazwa wasivyotegemea. Pamoja na ubabe wao lakini yupo Mungu anayesikiliza sala za yatima, wajane, vilema etc wanaoteseka sana kwa kudhulumiwa huduma. Kifo cha mafisadi kitaanzia humohumo kwenye kundi lao. Ukishakula nyama ya mtu huachi. Washazoea kudhulumu na kasi ya kudhulumiana wao kwa wao ikishapanda, watajikuta wapende wasipende wanasambaratishana wenyewe na wanyonge tunaibuka kidedea. It still can be done. Ungemwambia Smith au Botha kuwa ipo siku Prisoner Mandela angejakuwa President... nahisi angecheka. Yet pamoja na mauaji ya Soweto na kwingineko bado yaligeuka. Mchaka mchakaa mama-a.. Ushindi ni we-tu.
 
Wacha tujiridhishe kwa kuichambua nchi, huu ndo uhuru na maendele tuliyonayo kizazi hiki cha Tanzania.

Labda turudi nyuma tujiulize 'chama ni nini? Kama nakumbuka vyema siasa darasa la tano-sita hivi ilitufundisha kuwa "chama ni umoja wa watu wenye itikadi moja.

ITIKADI MOJA??? tujiulize viongozi wetu itikadi yao ni nini??? Jibu ni kuifisadi Tanzania.

Hivyo hata tupige kelele vipi mjue kwamba hao waliopo huko tayari wana itikadi moja. Hakuna atakayemkosoa mwenziwe.

Kuna tetesi wakati Mkapa akiwa rais, palitokea mkoroganyo wa baadhi ya wabunge wa CCM (matabaka) wakiwashutumiana kuwa wengine walishinda kwa rushwa. Suala hilo lilizidisha matabaka, ndipo Mkapa akawaita wabunge faragha na kuwaambia "ambaye hajashinda kwa rushwa na anyoshe mkono' wabunge wote walinywea kwa kuwa mgao ulipitishwa ndani ya chama cha CCM ili majimbo mengi yapate ushindi. Hii inaonyesha tu jinsi gani walivyo na itikadi moja. Hata kwa kuua ili mradi wazidi kutawala.

Huko kujigawia mafungu kumeota mizizi hata hakuna uoga tena. Vivyo hivyo sasa hivi wanajiandaa kwa kificha pesa za kutosha kwa kipindi cha 2010. Huenda zile za DECI zitafanya hiyo kazi.

Watanzania wamekata tamaa na maisha magumu, wanasubiri kwa hamu kanga na T-shirt za kipindi cha uchaguzi.
NANI WANA PESA KAMA MAFISADI???
NANI ATAWAONDOA MAFISADI MADARAKANI?? HAKUNA, Wamemiliki kila kitu kama mitandao ya MAFIA.

LABDA TUINGIE MSITUNI TUJIPANGE UPYA. Tuvurugane kama nchi nyingine walivyofanya, tuanzia na vijiji kuelekea mijini.
na tusipoangalia tudhalilishwa na tuachwe hoi kama Wazimbabwe.

Mungu ibariki Tanzania.
 

- Mkuu unachosema ni sawa sana, na ulichofanya katika kutoa hii hoja ya msingi ilikuwa ni fair politics na hasa politics za inclusion, kwa sababu hukuwa mbinafsi kwamba umefikiri na umefikia mwisho wa uamuzi wako peke yako hapana, umeileta hapa kwa majadiliano hii ishu ni very serious wka wanaoelewa siasa zetu na walio na nia njema na taifa letu, kwamba njia tunayoitumia sasa is not working, sasa ni wakati muafaka wa kutafuta njia nyingine na ukweak mifano na mifano ipo anyways kwamba we are not making any serious progress, na hata tunapojaribu kuvuta hatua mbili mbele wanakuja kina Rostam na Makamba na kuturudisha hatua mbili nyuma,

- Sasa Mwanamapinduzi hawezi kukalia hapo hapo tu aaaah we are winning, we are winning swali ni you are winning what? na Where? na when was that ulipo win mara ya mwisho? Ume-win with who? Ukweli ni kwamba hakuna majibu concrete with facts, sasa ni wakati wa kukaa chini na kutafuta mikakati mingine, na sio lazima wote tukubaliane on how to proceed kwa sababu tunajua lengo letu ni moja, lakini lazima kuwe na facts katika hizi argiuments badala ya zile zile blah! blah! ambazo zimetufikisha hapa tulipo yaani njia panda!

- Kuwashinda mafisadi kwa nje ni simple and clear haiwezekani ndio maana viongozi wetu wengi wa upinzani wameamua kugombea ubunge, badala ya urais that is political maturity kuna kitu wameona, haiwafanyi kwamba sasa wamekubali kuwa mafisadi no! ila wamekubali reality na kuanza na mbinu nyingine, sasa sisi tunafanya nini tutakalia pale pale ohh we are winning!

Tujifunze kubadilika na wakati jamani, kuwashinda mafisadi kwa nje sio rahisi na kwa sasa haiwezekani! Tutoe hoja ambazo ni applicable kwenye political ground zero yetu, badala ya imaginations kwa sababu our people are suffering wakuu! Maneno ya kutafuta ushujaa JF ni one thing na political reality ya taifa letu iko mbali sana na hizi alinachas!

Mwanakijiji uko right, tunahitaji muelekeo na muongozo mpya kwa wananchi namna ya kupigana na ufisadi, untili tutakapoupata tutaendelea kuwapigia kelele mpaka kieleweke!

Respect.

FMEs!
 

Kumbuka kelele za vyura mtoni...
 
Kumbuka kelele za vyura mtoni...


QUOTE=chamtumavi;454175]Wacha tujiridhishe kwa kuichambua nchi, huu ndo uhuru na maendele tuliyonayo kizazi hiki cha Tanzania.

Labda turudi nyuma tujiulize 'chama ni nini? Kama nakumbuka vyema siasa darasa la tano-sita hivi ilitufundisha kuwa "chama ni umoja wa watu wenye itikadi moja.

ITIKADI MOJA??? tujiulize viongozi wetu itikadi yao ni nini??? Jibu ni kuifisadi Tanzania.

Hivyo hata tupige kelele vipi mjue kwamba hao waliopo huko tayari wana itikadi moja. Hakuna atakayemkosoa mwenziwe.

Kuna tetesi wakati Mkapa akiwa rais, palitokea mkoroganyo wa baadhi ya wabunge wa CCM (matabaka) wakiwashutumiana kuwa wengine walishinda kwa rushwa. Suala hilo lilizidisha matabaka, ndipo Mkapa akawaita wabunge faragha na kuwaambia "ambaye hajashinda kwa rushwa na anyoshe mkono' wabunge wote walinywea kwa kuwa mgao ulipitishwa ndani ya chama cha CCM ili majimbo mengi yapate ushindi. Hii inaonyesha tu jinsi gani walivyo na itikadi moja. Hata kwa kuua ili mradi wazidi kutawala.

Huko kujigawia mafungu kumeota mizizi hata hakuna uoga tena. Vivyo hivyo sasa hivi wanajiandaa kwa kificha pesa za kutosha kwa kipindi cha 2010. Huenda zile za DECI zitafanya hiyo kazi.

Watanzania wamekata tamaa na maisha magumu, wanasubiri kwa hamu kanga na T-shirt za kipindi cha uchaguzi.
NANI WANA PESA KAMA MAFISADI???
NANI ATAWAONDOA MAFISADI MADARAKANI?? HAKUNA, Wamemiliki kila kitu kama mitandao ya MAFIA.

LABDA TUINGIE MSITUNI TUJIPANGE UPYA. Tuvurugane kama nchi nyingine walivyofanya, tuanzia na vijiji kuelekea mijini.
na tusipoangalia tudhalilishwa na tuachwe hoi kama Wazimbabwe.

Mungu ibariki Tanzania.
[/QUOTE]
 
"The pessimist complains about the wind; the optimist expects it to change; the realist adjusts the sails." -William Arthur Ward
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…