Mafisadi watashinda! - A somber look

Mafisadi watashinda! - A somber look

kwa kweli you are right, mimi naamini hivyo hivyo dalili zote zinanyesha ushindi kwa mafisadi. my main reason ni kuwa huyu jamaa anaetutawala ameonekana kuwaogopa kabisa kwani hatoi tamko wala ushirikiano na nasisi tuliiompigia kura na kuwa na imani nae kwa ziada.

If regii is standing on his behalf as regi stated yesterday that his confidence comes frm this jamaa why doesnt he say a thing i believe hii ingesaidia au he is one of them au anawaogopa sasa itakuwaje kuwaogopa,

solution : angetumia mwalimu's strategies wafungie kizuizini, period. nchi itatulia na imani itarudi jamani uongozi ni dhamana mtaulizwa killa kitu kesho mbele ya mwenyewe fundi mangungu, kama hamwuwezi acheni, dhuluma kubwa inaendelea hapa.
 
Wametushinda sababu ndio hao hao tuliwafuata na bakuli wakati wa uchaguzi....
 
Mimi ninatofautiana na hoja hii. Kwa mtizamo wangu naona hoja inatupa nafasi ya ku-posture na ku-grandstand bila kutueleza haswa namna gani tutaweza kufanikiwa katika vita hii. Badala yake imetupa jibu jepesi. Tatizo si kuchagua upande kati ya RA na Mengi. Cha msingi ni kusimamia haki bila kujali sura ya mhusika.

Hatujiulizi kuwa hao mafisadi tunaowaandama tukishawashinda, nini kitafuata? Jirani zetu Kenya waliing'oa KANu na kuweka matumaini yake kwa waliokuwa wakitema cheche dhidi ya ufisadi na sote tunajua yaliyotokea. Bila shaka kuna wengine wao wanaona heri wakati wa Moi. Na sisi hivyo hivyo. Tunadhani tukiitoa CCM, tukamfunga RA basi mambo yetu yatatunyookea! Si hivyo hata kidogo.

Tunachotakiwa kufanya ni kuangalia namna gani system yetu ilivyoruhusu na kulazimisha wakati mwingine vitendo vya ufisadi. Wenzetu Uingereza ilipoibuka scandal ya madai ya kurejeshewa expenses yaliyokuwa yakifanywa na wabunge, kitu cha kwanza walichofanya ni kuangalia ni namna gani ya kuzuia vitendo hivyo visije tokea tena. Nasi tunatakiwa kufanya hivyo.

Kwa mfano, tudai:
a) ulazima wa kuwepo na full disclosure kwa umma kwa mapato na kodi wanayolipa kila mwaka kwa wale wote walio katika nafasi za uongozi. Kila kiongozi atoe tax returns zake kila mwisho wa mwaka. Yake na ya spouse wake. Katika return hizo, mishahara, allowances, mapato kutoka biashara n.k. yote yawekwe wazi. Kama kiongozi anapewa allowance kwa ajili ya kulipia huduma alazimishwe kuwasilisha ushahidi wa kufanya malipo hayo. K.m. kama analipwa kwa ajili ya kuajiri dereva basi jina la huyo dereva, sifa zake na mshahara anaomlipa na ushahidi kuwa kweli analipa viambatanishwe.
b) ulazima wa kuwepo na full disclosure ya mapato na matumizi ya vyama vyote vya siasa. Mapato yaainishe makampuni na watu binafsi waliochangia na kiasi walichotoa.
c) pawe na limits cha kiasi ambacho mtu binafsi au kampuni anaweza kuchangia chama chochote kinachopokea ruzuku ya serikali.
e)Malipo na mapato ya Benki Kuuyawasilishwe kila quarter kwa kamati ya fedha ya bunge ambayo mwenyekiti wake atakuwa wa chama kikuu cha upinzani. Gavana wa Benki Kuu atoe ripoti kwa bunge kila mwaka kuhusu matumizi na mapato ya benki hiyo.
f) Nafasi zaote za watendaji wa juu wa serikali zipitishwe na bunge baada ya kuteuliwa na Rais.
g) Wakati wa uchaguzi, wagombea wote wawasilishe ripoti ya matumizi yao, gharama zao na michango yao. Ripoti iainishe nani katoa mchango na kiasi alichotoa pamoja na nani kalipwa, kwa nini kalipwa na kiasi alicholipwa.
h) Ripoti za utekelezaji wa bajeti kwa kila wizara zote ziwasilishwe kila robo mwaka kwa kamati ya bunge ya fedha niliyoitaja hapo juu. Kamati hiyo ndiyo itakayoamua kama ripoti hizo ziwe siri au ziwasilishwe kwa umma.
i) Usiri wa ripoti zote udumu kwa miaka mitatu isipokuwa zile zinazohusu usalama wa taifa. Maamuzi wa zipi zinastahili kuitwa za usalama wa taifa ufanywe na serikali ikishirikiana na kamati ya bunge husika. Ripoti hizi zifungiwe kwa kipindi kisichozidi miaka itano ambapo nazo ziwekwe wazi kwa umma.

Na kadhalika kadhalika.

Kwa kufanya hivi tutahakikisha kuwa yeyote atakaeingia, tutaweza kumbana. Ni system mbovu tuliyonayo ndiyo inaruhusu vitendo hivi. System hii hii ndiyo inayolazimisha wafanya biashara kujikomba kwa chama tawala ili mambo yao yawanyookee. Tukiondoa uwezo wa viongozi wa juu kutoa upendeleo bila kuhojiwa, basi ulazima huu utatoweka. Hakuna mfanyabiashara ambae atakuwa tayari kuwekeza mahali ambapo hana uhakika wa kufaidika!

Amandla.......

Mkuu hapo juu tuko ukurasa mmoja...........
 
Mkuu hapo juu tuko ukurasa mmoja...........

,.............................NAUNGA MKONO HOJA NA BAADA YA HAPO UAMUZI WA ZIPI ZIWE SIRI ZITANGAZWE KWA UMMA Kwamba taarifa kadha wa kadha ni siri kama hautaki waambiewe kwa kina ni kwa nini ziwe siri
 
Nakubaliana na wewe. Lakini cha msingi kwangu mimi ni kuwa pawe na mtazamo wa hakuna siri ya daima. Mtu akijua kuwa anachokifanya ni lazima kitakuja kuona mwanga wa jua siku moja basi pengine atasita kufanya mambo mengine. Na vile vile watumishi na viongozi wote walazimike kutunza nyaraka na kumbukumbu zao.

Amandla.....
 
Fundi,

Ni mwanzo mzuri kuona kuna watu wanaliangalia hili jambo la ufisadi kwa mapana yake na solution na muda mrefu.

Nimeipenda analysis yako na kwa kifupi kama ulivyoweka abundantly clear suala ni system sio kambi kama ma-pundit wetu wa JF wanavyolazimisha watu iwe. Na hilo ndio kosa kubwa tunalofanya sasa kudhani adui yetu ni a,b & c n wakitoka hao na wakiingia z,y & z mambo yetu yatakuwa poa. Tunachosahau playing ground ni ile ile na rules ni zile zile na mwishoe matokeo yatakuwa ni yale yale!

Mifano uliyotoa ni tosheleza wenye macho na waone na wenye masikio na wasikie....
 
Mimi ninatofautiana na hoja hii. Kwa mtizamo wangu naona hoja inatupa nafasi ya ku-posture na ku-grandstand bila kutueleza haswa namna gani tutaweza kufanikiwa katika vita hii. Badala yake imetupa jibu jepesi. Tatizo si kuchagua upande kati ya RA na Mengi. Cha msingi ni kusimamia haki bila kujali sura ya mhusika.

Hatujiulizi kuwa hao mafisadi tunaowaandama tukishawashinda, nini kitafuata? Jirani zetu Kenya waliing'oa KANu na kuweka matumaini yake kwa waliokuwa wakitema cheche dhidi ya ufisadi na sote tunajua yaliyotokea. Bila shaka kuna wengine wao wanaona heri wakati wa Moi. Na sisi hivyo hivyo. Tunadhani tukiitoa CCM, tukamfunga RA basi mambo yetu yatatunyookea! Si hivyo hata kidogo.

Tunachotakiwa kufanya ni kuangalia namna gani system yetu ilivyoruhusu na kulazimisha wakati mwingine vitendo vya ufisadi. Wenzetu Uingereza ilipoibuka scandal ya madai ya kurejeshewa expenses yaliyokuwa yakifanywa na wabunge, kitu cha kwanza walichofanya ni kuangalia ni namna gani ya kuzuia vitendo hivyo visije tokea tena. Nasi tunatakiwa kufanya hivyo.

Kwa mfano, tudai:
a) ulazima wa kuwepo na full disclosure kwa umma kwa mapato na kodi wanayolipa kila mwaka kwa wale wote walio katika nafasi za uongozi. Kila kiongozi atoe tax returns zake kila mwisho wa mwaka. Yake na ya spouse wake. Katika return hizo, mishahara, allowances, mapato kutoka biashara n.k. yote yawekwe wazi. Kama kiongozi anapewa allowance kwa ajili ya kulipia huduma alazimishwe kuwasilisha ushahidi wa kufanya malipo hayo. K.m. kama analipwa kwa ajili ya kuajiri dereva basi jina la huyo dereva, sifa zake na mshahara anaomlipa na ushahidi kuwa kweli analipa viambatanishwe.
b) ulazima wa kuwepo na full disclosure ya mapato na matumizi ya vyama vyote vya siasa. Mapato yaainishe makampuni na watu binafsi waliochangia na kiasi walichotoa.
c) pawe na limits cha kiasi ambacho mtu binafsi au kampuni anaweza kuchangia chama chochote kinachopokea ruzuku ya serikali.
e)Malipo na mapato ya Benki Kuuyawasilishwe kila quarter kwa kamati ya fedha ya bunge ambayo mwenyekiti wake atakuwa wa chama kikuu cha upinzani. Gavana wa Benki Kuu atoe ripoti kwa bunge kila mwaka kuhusu matumizi na mapato ya benki hiyo.
f) Nafasi zaote za watendaji wa juu wa serikali zipitishwe na bunge baada ya kuteuliwa na Rais.
g) Wakati wa uchaguzi, wagombea wote wawasilishe ripoti ya matumizi yao, gharama zao na michango yao. Ripoti iainishe nani katoa mchango na kiasi alichotoa pamoja na nani kalipwa, kwa nini kalipwa na kiasi alicholipwa.
h) Ripoti za utekelezaji wa bajeti kwa kila wizara zote ziwasilishwe kila robo mwaka kwa kamati ya bunge ya fedha niliyoitaja hapo juu. Kamati hiyo ndiyo itakayoamua kama ripoti hizo ziwe siri au ziwasilishwe kwa umma.
i) Usiri wa ripoti zote udumu kwa miaka mitatu isipokuwa zile zinazohusu usalama wa taifa. Maamuzi wa zipi zinastahili kuitwa za usalama wa taifa ufanywe na serikali ikishirikiana na kamati ya bunge husika. Ripoti hizi zifungiwe kwa kipindi kisichozidi miaka itano ambapo nazo ziwekwe wazi kwa umma.

Na kadhalika kadhalika.

Kwa kufanya hivi tutahakikisha kuwa yeyote atakaeingia, tutaweza kumbana. Ni system mbovu tuliyonayo ndiyo inaruhusu vitendo hivi. System hii hii ndiyo inayolazimisha wafanya biashara kujikomba kwa chama tawala ili mambo yao yawanyookee. Tukiondoa uwezo wa viongozi wa juu kutoa upendeleo bila kuhojiwa, basi ulazima huu utatoweka. Hakuna mfanyabiashara ambae atakuwa tayari kuwekeza mahali ambapo hana uhakika wa kufaidika!

Amandla.......

Tukianza na hayo uliyoyachanganua Mkuu Fundi.........sasa tuangalie sheria/katiba yetu inasemaje kuhusu hivyo vipengele...ili kujenga hoja mbele ya watunga sheria wetu
 
There will be no compromise, no surrender no retreat; we intend to win, to defeat those who threaten our democracy, we intend to squash them like little stupid ants under our feet and we intend methodically and scientifically to remove them from their grip of power.

... is worthy fighting and dying for! We will oppose you, we will expose you, we will challenge your leadership, and we will defeat you.

... it doesn't matter the number of intelligence officers that you have corrupted, ...

.... as long as you continue to corrupt our young generation,...

No retreat, no surrender

Hatimaye nimefikia hitimisho kuwa juhudi za kupambana na ufisadi nchini hazitofanikiwa na ya kuwa upepo wa ushindi unavuma kuelekeza merikebu za mafisadi kuelekea ushindi! ....

...Kuelekea uchaguzi mkuu mwakani himaya hiyo imepanga sasa watu wapya kabisa kuanza kuingia katika safu za uongozi na hasa Bungeni ili hatimaye usalama wao uzidi kuhakikishwa. Kiwango kikubwa cha fedha kimeshatengwa kuhakikisha (na hili limeshasemwa na wengine) wabunge wote ambao wanapigia kelele ufisadi wanaaungushwa kwenye kura za maoni na watu wapya kuingia. Lengo la hilo ni kuhakikisha kuwa inapofika Bunge jipya ule upinzani ambao umekuwa ukisikika utakuwa umezimwa kwa kiasi cha kutosha na ukabakia kuwa ni upinzani wa magazetini.

Vyovyote vile ilivyo, naomba niwakatishe matumaini kabisa kuwa kufikiria kuwa "vita ya ufisadi ambayo bado inaendelea" kwa mujibu wa Mkuchika ni vita ambayo mafisadi watashinda. Watashinda kwa sababu kubwa tano.

a. Wamejipanga vizuri zaidi kuliko wanaopinga ufisadi (well organized)....

b. Wamewekeza fedha pale wanapokula na hawaoni haya kufanya hivyo (well funded). Wanaopinga ufisadi wanatumia maneno tu, wenye kuwekeza fedha wanaonekana wanataka kujitajirisha na wale ambao wanatumia fedha zao kupigana na ufisadi na wenyewe wanageuziwa kibano alimradi kuvuruga juhudi zao. ...

c. Wamejikita vizuri na kuwabana watawala na vyombo mbalimbali...

d. Wanaogopesha; wanatumia serikali na vyombo vyake kuingiza hofu kwa watu wa kawaida kwa kauli za "kuvunjika kwa amani", "watachukuliwa hatua za kisheria", n.k (they command fear). ...

e. Wako tayari kwenda umbali wowote ule kuhakikisha hawaondoki madarakani au mirija yao kukatwa (ready to sacrifice). Katika hili watawatoa sadaka wenzao wachache ili kutuliza munkari wa jamii lakini wakati huo huo wakiwapanga wengine.

Ninachosema kwa maneno mawili ni kuwa 'we are screwed!" (najua ni matatu!) hakuna matumaini, hakuna njia ya kutokea, na hakuna mashujaa wetu wa kutuongoza vitani. .....

there is kusurrender. Screwed up for real.
 
Last edited by a moderator:
Na point yako? Kwamba wakenya walimchagua Kibaki wakijua kuwa Moi ataendelea kupeta! Zambia kumenyooka? Tangu lini? Au kwa vile Chiluba ( another anti fisadi aliyegeuka kuwa fisadi) anasumbuliwa?

- Wakenya walimchagua Kibaki wakiwa na mawazo kama yako kwamba wamewashinda mafisadi, kumbe ndio kwanza wamejichimbia kaburi maana Moi na Kibaki lao lilikuwa moja, kama unajua siasa vizuri hasa za East Africa, Moi huwezi kumuweka mtoto mdogo kama Uhuru Kenyatta, asimame kugombea utawala na mafisadi papa kama kina Saitoti na Kibaki, halafu ukasema eti unaitakia mema taifa lako, ndio maana Wakenya walipogundua mistake waliyoifanya wakakataa kubadilishwa katiba.

- Zambia haijanyooka as the meaning ya kunyooka if you will, lakini hatuko sawa nao kwenye hiyo njia, wao wako mbali sana maana walishaanza kufanya kweli, ni kwa sababu Mwanawasa aijiunga na mafisadi baadaye akiwa ndani akawageuka.

FMEs!

Kwa kifupi, hivi kweli unaamini kuwa Mengi akiwa Rais basi ufisadi utakwisha? Au Dr. Slaa? Bila kubadilisha system, temptation zitabaki pale pale.

- Kaangalie kule nyuma maelezo yangu kuhusu mabadiliko, nimesema bila kubadili katiba huwezi kuibadili Tanzania kutokea nje, ni lazima uingie ndani yaani ujiunge nao kwanza!

Mfano rahisi, ni wangapi kati ya hao wanaopiga kelele kuhusu ufisadi bungeni wamenyanyua sauti zao dhidi ya dhulma hii wanayotaka kufanya ya kujipandishia mishahara? Wangapi wako na Slaa katika kilio chake kuwa malipo yao ni kupita kiasi? Hawa ndio unadhani wakipata nafasi ya kutu-EPA wataacha kweli? Lame excuses ni zako. Kudhani kuwa tatizo ni personalities na si system! Mnaogopa kubadilisha system maana mnajua kuwa nanyi mkipata nafasi mtafanya haya haya mnayowalaumu wenzenu!

Amandla......
[/QUOTE]

- Kupandishwa mishahara ya wabunge ni debatable ishu, kuna wabunge wanaoweza kuonyesha facts kwamba wanahitaji kupandishiwa mishahara kwa sababu karibu hela zao zote huzitumia na wanajimbo wao, I have seen it na kuna wabunegw engine hawahitaji kupandishwa, sasa una-create vipi sheria ya baadhi tu ya wabunge? Huwezi kwa hiyo either wote wanyimwe au wapewe, nina experience ya kutosha na siasa za majimbo ya ubunge ndio maana ninaamini sana kwa 100% kwamba kuna wabunge wanahitaji kuongezwa mishahara na marupurupu, na wengine hawahitaji. Kwa hiyo mawazo yako kwamba kuomba nyongeza kwa wabunge ni dhuluma ni mbali sana na ukweli wa siasa za majimbo yetu ya ubunge!

- Personalities na the rest of the story ndio ile ile tabia yako ya personal huwezi kuchangia ishu bila personal, samahani mimi sihusiki na kubadilisha system yoyote na wala sio kiongozi wa system yoyote ya siasa, zaidi tu ya kampuni yangu ambayo hahitaji mabadiliko maana nimeijenga kwa jasho na damu yangu na kwa kufuata njia zinazotakiwa, haihitaji mabadiliko.

Respect.

FMEs!
 
Mapandekezo ya kubadili CCM na uchambuzi wa tatizo la CCM yamefanyika kwa miaka 30! Haja ya mabadiliko ya Katiba ni ya zamani kwa miaka 20, kwamba jinsi gani mambo yanaweza kuendeshwa kwa uwazi zaidi ni la kale tangu mwaka wa kwanza wa Mkapa.

Hakuna jipya! Na kwa mtindo huu tutaendelea kutoa mapendekezo bora zaidi miaka 20 ijayo na hali itaendelea kuwa ile ile huku kizazi kipya cha mafisadi kikiendelea kutawala bila kulala!

Kwamba njia bora ni hii au ile yameshasemwa na kujadiliwa hadi Bungeni! Walioko huko Bungeni na wengine wanayajua mapungufu ya Katiba kuliko sisi wengine; huko huko ndiko kuliko na maprofesa na wasomi wa kila fani! Kwenye hizo wizara zao wamejanzana watu wenye uchambuzi wa kisomi wa matatizo ya nchi yetu kwa miongo..

kwamba tatizo ni "system" hili nimelisikia tangu shule ya vidudu (chekechea!)..

So.. hakuna nilichosoma ambacho ni kipya. Kinazidi tu kuthibitisha kuwa mafisadi watashinda kwa mtindo huu wa kuchambuua na kupendekeza njia bora zaidi za kufanya mambo, njia ambazo zilishapendekezwa na baba na mama zetu! Gurudumu la kushindwa linaendelea kuzunguka!
 
Obama anasafishaje Democratic party? Mwanawasa alibadilishaje MDD? Umeishasahau ushindi wake ulivyojaa mizengwe? Alihakikishaje kuwa uchaguzi wowote utakaomfuata utakuwa fair? Angalia yaliyompata Michael Sata aliposhindana na Rupiah Banda! Kiini macho kile kile kilirudiwa. Rupiah Banda aliyepewa umakamu na Mwanawasa kama shukrani kwa watu wa mashiriki ya Zambia kwa kumpigia kura!

- Obama mfano ni mdogo sana tu, umesikia aliioyafanya na pirates, piga risasi hakuna kujadiliana na mafisadi hiyo haijawahi kuwa tabia ya democrats hii ni mara ya kwanza katika historia ya Democratc party huko US.

- Mwanawasa, alishinda uchaguzi kwa kusaidiwa na mafisadi kama Chiluba Vernon Mwaanga, na kina Wilson Nchikuli na Nlumino Mundia, hawa ndio the Rostams wa huko Zambia, ambako nimewahi kuishi sana mkuu wangu, lakini Mwanawasa baada tu ya kushinda akamgeuka Chiluba na mafisadi wengine wengi wa kutupwa kama kina Elijah Mudenda,

- By the time anakufa tayari alishkuwa half way kuwashikisha adabu mafisadi, alishaweza ku-secure a convinction against Chiluba katika mahakama za UK, na kuweza ku-freeze hela zote za Chiluba UK, ambazo ni millions of dollars, huwezi safisha system kabla hujaanza na wahusika yaani viongozi na mafisadi wote, Mwanawasa was on the right track, as opposed na sisi bongo ambako rais wetu anawaogopa kina Rostam, Mwanawasa alianza na marafiki kama rostam kwanza.

- Rupia Banda, alikuwa ni kiongozi wa UNIP kwa muda mrefu sana under Kaunda, ameshika nafasi nyingi sana za chama cha UNIP wa-Zambia karibu wote wanamfahamu, Sata sijui kama unamfahamu viuri mkuu ni fisadi nambari moja, na ni mgeni wa siasa za Zambia, wananchi wa Zambia sio wajinga walishagundua kwamba Mwanawasa hayupo tena na mambo yake yamesha isha, kwa hiyo wakachagua experience in Banda, meaning political stability over fisadi Sata.

Unamtoa Muluzi kama mfano? Muluzi aliyetaka kubadili katiba ili aendelee kutawala.? Muluzi ambae serikali yake iliuza akiba ya mahindi ya nchi yake na kuleta janga la njaa Malawi? Mapato ya mauzo hayo ambayo hadi sasa hayajaonekana mahali! Muluzi ambae anashitakiwa na ACB ( Anti Corruption Bureau) kwa kubinafsisha mamilioni ya dola za wamalawi! Huyu ndiyo mfano wako wa wanaongoza mapambano dhidi ya mafisadi?[/QUOTE]

- Hapana hapa ni my bad, nilidhamiria kumtaja rais aliyechukua utawala baada ya Muluzi, samahani sana kwa hilo kosa.

Mvivu wa kufikiri ni wewe, Mkuu!

Amandla......
- This is typical you, bila maneno ya hovyo hovyo personally huwezi kumaliza hoja, mimi niliposema uvivu wa kufikiri sikumlenga anybody personally, lakini mkuu wangu huwezi andika hoja bila hizi lugha vipi mkuu ukiziacha maana uvumilivu huwa una kikomo chake, kama huwezi hizi debate hasa na mimi bila hizi maneno ya hovyo hovyo, please acha kunijibu na sitagusa hoja zako, ninajaribu kukupa heshima naona huitaki mkuu hatuhitaji hizi katika kujadili mustakabali wa masilahi ya taifa letu, sitasema on this personal thing tena maana nimesema ya kutosha sasa.

Respect.

FMES!
 
Mjj na wengine poleni kwa tafakari hii chungu ila tusikate tamaa. Hiyo ndo sala yao na naamini watafanya kweli ila bado watawezashangazwa wasivyotegemea. Pamoja na ubabe wao lakini yupo Mungu anayesikiliza sala za yatima, wajane, vilema etc wanaoteseka sana kwa kudhulumiwa huduma. Kifo cha mafisadi kitaanzia humohumo kwenye kundi lao. Ukishakula nyama ya mtu huachi. Washazoea kudhulumu na kasi ya kudhulumiana wao kwa wao ikishapanda, watajikuta wapende wasipende wanasambaratishana wenyewe na wanyonge tunaibuka kidedea. It still can be done. Ungemwambia Smith au Botha kuwa ipo siku Prisoner Mandela angejakuwa President... nahisi angecheka. Yet pamoja na mauaji ya Soweto na kwingineko bado yaligeuka. Mchaka mchakaa mama-a.. Ushindi ni we-tu.
 
Wacha tujiridhishe kwa kuichambua nchi, huu ndo uhuru na maendele tuliyonayo kizazi hiki cha Tanzania.

Labda turudi nyuma tujiulize 'chama ni nini? Kama nakumbuka vyema siasa darasa la tano-sita hivi ilitufundisha kuwa "chama ni umoja wa watu wenye itikadi moja.

ITIKADI MOJA??? tujiulize viongozi wetu itikadi yao ni nini??? Jibu ni kuifisadi Tanzania.

Hivyo hata tupige kelele vipi mjue kwamba hao waliopo huko tayari wana itikadi moja. Hakuna atakayemkosoa mwenziwe.

Kuna tetesi wakati Mkapa akiwa rais, palitokea mkoroganyo wa baadhi ya wabunge wa CCM (matabaka) wakiwashutumiana kuwa wengine walishinda kwa rushwa. Suala hilo lilizidisha matabaka, ndipo Mkapa akawaita wabunge faragha na kuwaambia "ambaye hajashinda kwa rushwa na anyoshe mkono' wabunge wote walinywea kwa kuwa mgao ulipitishwa ndani ya chama cha CCM ili majimbo mengi yapate ushindi. Hii inaonyesha tu jinsi gani walivyo na itikadi moja. Hata kwa kuua ili mradi wazidi kutawala.

Huko kujigawia mafungu kumeota mizizi hata hakuna uoga tena. Vivyo hivyo sasa hivi wanajiandaa kwa kificha pesa za kutosha kwa kipindi cha 2010. Huenda zile za DECI zitafanya hiyo kazi.

Watanzania wamekata tamaa na maisha magumu, wanasubiri kwa hamu kanga na T-shirt za kipindi cha uchaguzi.
NANI WANA PESA KAMA MAFISADI???
NANI ATAWAONDOA MAFISADI MADARAKANI?? HAKUNA, Wamemiliki kila kitu kama mitandao ya MAFIA.

LABDA TUINGIE MSITUNI TUJIPANGE UPYA. Tuvurugane kama nchi nyingine walivyofanya, tuanzia na vijiji kuelekea mijini.
na tusipoangalia tudhalilishwa na tuachwe hoi kama Wazimbabwe.

Mungu ibariki Tanzania.
 
kwamba tatizo ni "system" hili nimelisikia tangu shule ya vidudu (chekechea!)..

So.. hakuna nilichosoma ambacho ni kipya. Kinazidi tu kuthibitisha kuwa mafisadi watashinda kwa mtindo huu wa kuchambuua na kupendekeza njia bora zaidi za kufanya mambo, njia ambazo zilishapendekezwa na baba na mama zetu! Gurudumu la kushindwa linaendelea kuzunguka!

- Mkuu unachosema ni sawa sana, na ulichofanya katika kutoa hii hoja ya msingi ilikuwa ni fair politics na hasa politics za inclusion, kwa sababu hukuwa mbinafsi kwamba umefikiri na umefikia mwisho wa uamuzi wako peke yako hapana, umeileta hapa kwa majadiliano hii ishu ni very serious wka wanaoelewa siasa zetu na walio na nia njema na taifa letu, kwamba njia tunayoitumia sasa is not working, sasa ni wakati muafaka wa kutafuta njia nyingine na ukweak mifano na mifano ipo anyways kwamba we are not making any serious progress, na hata tunapojaribu kuvuta hatua mbili mbele wanakuja kina Rostam na Makamba na kuturudisha hatua mbili nyuma,

- Sasa Mwanamapinduzi hawezi kukalia hapo hapo tu aaaah we are winning, we are winning swali ni you are winning what? na Where? na when was that ulipo win mara ya mwisho? Ume-win with who? Ukweli ni kwamba hakuna majibu concrete with facts, sasa ni wakati wa kukaa chini na kutafuta mikakati mingine, na sio lazima wote tukubaliane on how to proceed kwa sababu tunajua lengo letu ni moja, lakini lazima kuwe na facts katika hizi argiuments badala ya zile zile blah! blah! ambazo zimetufikisha hapa tulipo yaani njia panda!

- Kuwashinda mafisadi kwa nje ni simple and clear haiwezekani ndio maana viongozi wetu wengi wa upinzani wameamua kugombea ubunge, badala ya urais that is political maturity kuna kitu wameona, haiwafanyi kwamba sasa wamekubali kuwa mafisadi no! ila wamekubali reality na kuanza na mbinu nyingine, sasa sisi tunafanya nini tutakalia pale pale ohh we are winning!

Tujifunze kubadilika na wakati jamani, kuwashinda mafisadi kwa nje sio rahisi na kwa sasa haiwezekani! Tutoe hoja ambazo ni applicable kwenye political ground zero yetu, badala ya imaginations kwa sababu our people are suffering wakuu! Maneno ya kutafuta ushujaa JF ni one thing na political reality ya taifa letu iko mbali sana na hizi alinachas!

Mwanakijiji uko right, tunahitaji muelekeo na muongozo mpya kwa wananchi namna ya kupigana na ufisadi, untili tutakapoupata tutaendelea kuwapigia kelele mpaka kieleweke!

Kumbuka kelele za vyura mtoni...
 
Kumbuka kelele za vyura mtoni...

QUOTE=chamtumavi;454175]Wacha tujiridhishe kwa kuichambua nchi, huu ndo uhuru na maendele tuliyonayo kizazi hiki cha Tanzania.

Labda turudi nyuma tujiulize 'chama ni nini? Kama nakumbuka vyema siasa darasa la tano-sita hivi ilitufundisha kuwa "chama ni umoja wa watu wenye itikadi moja.

ITIKADI MOJA??? tujiulize viongozi wetu itikadi yao ni nini??? Jibu ni kuifisadi Tanzania.

Hivyo hata tupige kelele vipi mjue kwamba hao waliopo huko tayari wana itikadi moja. Hakuna atakayemkosoa mwenziwe.

Kuna tetesi wakati Mkapa akiwa rais, palitokea mkoroganyo wa baadhi ya wabunge wa CCM (matabaka) wakiwashutumiana kuwa wengine walishinda kwa rushwa. Suala hilo lilizidisha matabaka, ndipo Mkapa akawaita wabunge faragha na kuwaambia "ambaye hajashinda kwa rushwa na anyoshe mkono' wabunge wote walinywea kwa kuwa mgao ulipitishwa ndani ya chama cha CCM ili majimbo mengi yapate ushindi. Hii inaonyesha tu jinsi gani walivyo na itikadi moja. Hata kwa kuua ili mradi wazidi kutawala.

Huko kujigawia mafungu kumeota mizizi hata hakuna uoga tena. Vivyo hivyo sasa hivi wanajiandaa kwa kificha pesa za kutosha kwa kipindi cha 2010. Huenda zile za DECI zitafanya hiyo kazi.

Watanzania wamekata tamaa na maisha magumu, wanasubiri kwa hamu kanga na T-shirt za kipindi cha uchaguzi.
NANI WANA PESA KAMA MAFISADI???
NANI ATAWAONDOA MAFISADI MADARAKANI?? HAKUNA, Wamemiliki kila kitu kama mitandao ya MAFIA.

LABDA TUINGIE MSITUNI TUJIPANGE UPYA. Tuvurugane kama nchi nyingine walivyofanya, tuanzia na vijiji kuelekea mijini.
na tusipoangalia tudhalilishwa na tuachwe hoi kama Wazimbabwe.

Mungu ibariki Tanzania.
[/QUOTE]
 
"The pessimist complains about the wind; the optimist expects it to change; the realist adjusts the sails." -William Arthur Ward
 
Back
Top Bottom