Mafundi Magari mnawadhulumu madogo, huu si ungwana

Mafundi Magari mnawadhulumu madogo, huu si ungwana

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Habari!

Mnawatoa mikoani kwa kuwaahidi kuja kuwafunza ufundi, ila wakija huku mnawatumikisha na wanakuwa mafundi wa kukariri na kujua kufunga na kufungua pekee.

Mnawanyima maarifa na kuwafanya watumwa wenu. Mnawalipa malipo hafifu ili waendelee kuwatumikia. Hii haikubaliki.

Na ndiyo maana mafundi wengi siku hizi ni hovyo kabisa, wamekariri na hawajui hata ku reason ili kutafuta tatizo.

Wamekalia kupiga nyundo, kufunga na kufungua tu. Kwa nini mnafanya hayo?

Magari hayaishi na hayatokuja kwisha. Wafunzeni madogo ufundi stahiki badala ya kuwakaririsha kimakusudi ili wawatumikie. Huo ushamba!.
 
Chanzo kilikua kuku alinunua njiani kuku wawili mweusi na mwekundi wakifika boda pale wanapaki yule dogo anaejifunza alikua anampikia sasa unajua nini kilitokea?
Dah! Yaani kuonja tu ndiyo akamuua? Mbona hawa mafundi wana chuki sana?
 
Dah! Yaani kuonja tu ndiyo akamuua? Mbona hawa mafundi wana chuki sana?
Alimwambia kwamba wakifika boda achinje kuku mweusi dogo akakosea akachinja mwekundu ugomvi ukaanzia hapo akamwambia kuku hapati na Ugali hampi na hapo Ugali kapika dogo, kilichofuata sitaki kua shahidi
 
life hili,,kuna kipindi nilikataa shule form 3 ikabid nimwambie mzee sitaki kusoma nataka kuwa fundi umeme,kuna fundi ni rafiki wa mzee akanipeleka nikakomae shule si nimeacha.

tulikuwa tunafanya kazi bila kula tokea asubuhi hadi jioni na sehemu ata iwe mbali vipi mtatembea kwa miguu ila yeye fundi mkuu anachukua usafiri nilikaa miezi 2 nikaacha nikaomba nirudi tu kusoma tu
 
😂😂😂 Kudadadeq yanini kuuana
 
Mimi naamini katika nidhamu na juhudi binafsi.....

Mafundi wengi hufanya ivyo sabb kama ukimpa maarifa yote kijana baada ya muda mfupi madogo wanaanzaga madharau unakua humbabaishi...

Na anaweza akahama ofis bila kukutaarif au kuhamisha wateja hizi zote ni assumptions tu..

NB:
Sometimes Ili uchote maarifa ya Hawa jamaa inabidi uwe zoba ila very determined...Mtulivu,msikivu,mchapakazi,kujituma, humble ukipata unachokitafuta sepa kaanzishe chako au tafuta fursa nzuri zaidi ..

Akili ku mkichwa
 
Back
Top Bottom