Utakuwa na akili mbovu ukinunua sofa za seremala wa mtaani 5M. Ni kwamba hujui maduka ya imported au??Waambie! Unakuta hayo makochi feki wameyaweka "prime area open space" kama namanga, Oystabei, masaki, mikocheni, pembeni ya barabara ya old bagamoyo, n.k. watakupiga sound mpaka ulegee!
Mimi ghetto langu la kichuochuo kuna kasofa ka 140,000 ka watu wawili. Nauza nako sura ila sio ka kukaliwa na familia. Laki tatu utapata tafuta ila ni vitambaa vya nguo ujue.Natafuta sofa simple jamani. Seti mbili za kukaa watu wawili wawili. Natapatikana Ubungo. Bajeti yangu 300,000 sofa mbili zote.
Aisee bongo hamna kitu...Tulinunua set ya sofa ila baada ya wiki mbao zimeshaanza kukatika na imagine apo hamna watoto wa kuruka ruka
Alikuuzia shingapi, seti ngapi zipo. Unaweza kudondosha picha yake.Kuna fundi mmoja Keko ustaadh Mungu amuweke muda mrefu aliniuzia sofa tangu 2014 bado linanesa tu,yule fundi ni mtu wa quality watu huwa wanadhani nimeimport kumbe ni made from Keko
Panya [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mmmh 1.5-5M hapana aisee , hayaa hayaa siku mbili panya wameshafanya ndio nyumba yao?? Ndio maana mi nimeamua kuweka antiques tu.
Kitu imported hakiwezi fanana na kitu cha KekoKuna fundi mmoja Keko ustaadh Mungu amuweke muda mrefu aliniuzia sofa tangu 2014 bado linanesa tu,yule fundi ni mtu wa quality watu huwa wanadhani nimeimport kumbe ni made from Keko
Kununua sofa kwa watengenezaji wa kitanzania ni sawa na kununua barakoa ya kushonwa na fundi cherehaniUnakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!
Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.
Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.
Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.
sitathubutu kununua hizo takatakaKitu imported hakiwezi fanana na kitu cha Keko
Yananuka hatari[emoji23][emoji23][emoji23]kwamba linanuka mkojo