Unakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!
Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.
Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.
Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.