Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,077
- 1,439
Hili limemkuta jamaa yangu juzi. Mteja kampelekea simu ya touch ili kubadili display. Jamaa kanunua display kambadilishia baada ya makubaliano ya bei. Ilipokamilika kamtaarifu mteja wake kwamba simu iko tayari. Mteja kamwambia kama utapita maeneo ya ofisini kwangu nipitishie, wakaafikiana.Kama sio tapeli utaanzaje kudaiwa? Akileta simu kama iko ndani ya uwezo wangu wa kupona namwambia bei akiafiki namwambia kama hauna shughuli zingine subiria hapahapa uondoke nayo. Maana kwenye simu kuna lawama nyingi sana, mfano unaflash simu logo inabadilika anakwambia simu siyo yenyewe na haitaki hata umuelewesheje haamini anajua umemuibia.
Au kaleta simu imezimika unaiflash inawaka kumbe ilikuwa na tatizo lingine la sipika, maiki au batani anakomaa kwamba simu yake ilikuwa nzima labda umeibadilisha usitaarabu usipotumika hapo mteja anakuona tapeli.
Fundi wakati anaipeleka iko mfukoni akiwa na boda sijui hata ilitokea nn touch ikavunjika. Ikabidi arudi akamnunulie touch nyingine kamuwekea. Kasheshe likaibuka wakati amemaliza kuweka touch anafunga simu eti ile display aliyoweka ikafa(sikuelewa namna ilivyokufa).
Mteja alipofika kuchukua simu yake akaelezwa hiyo scenario akauliza sasa tunafanyaje? Mteja alikuwa polisi pia!
Nikaacha mjadala.