Nimependa jinsi unavyokomaa katika hardware, lakni tambua mambo yafuatayo katika kuflashi simu yanayowashinda watu wa software..
1: Walio wengi hawajui driver zipi za kutumia wakati wa kuflash au namna ya kuzi-install hapa hadi ujue namna ya kufunga driver signature katika windows. Kuna driver tofauti kulingana na cpu ya simu kuna fastboot driver, adb driver, cdc driver,cpu driver nk na zote ni kwa ajili ya simu moja kulingana na unachotaka kufanya katika simu husika. Bila driver utaishia kusema simu haisomi.
2: Katika kuflash inabidi uwe na usb cable nyingi halafu origino, ikitokea ukaunganisha isisome au ikakwambia usb haitambuliki badilisha usb nyingine (hii imenitokea mara nyingi baada ya kubadilisha usb nyingine simu inakubali).
3: Uchafu au vumbi katika usb port ya simu. Ni vema ukasafisha na benzini kwanza ili kuondoa vumbi. Pia inabidi utambue boot key za kutumia wakati wa kuunganisha simu na usb sio simu zote zinazotumia power key. Hapa unaweza ukashangaa unachomeka usb simu inaanza kuchaji.
4: Mwisho kabisa usitegemee flashing box pekee kwamba litamaliza tatizo lako la simu, tumia tools mbalimbali kulingana na simu.
Ukiambiwa na fundi software kwamba memory imekufa yeye kama yeye hawezi kuiflash. Simu zinatumia memory ambayo ndo inabeba os ni kama vile kompyuta inavyotumia hdd kuwekewa windows, ile memory ikifa ukipata nyingine kama ile unaweza ukabadilisha na ukaiflash simu yako.