Mafundi umeme mnisaidie kuhusu hiki kitu

Dawa ni kumshawishi mwenye nyumba kuweka hiyo meter separator kwa mbishi wa kulipia umeme ili yeye ndiye awe ananunua token katika main meter. Akiishiwa anakosa umeme peke yake.
safi sana
 
sahihi mkuu nimekupata
 
mkuu Samico Tanzania nikinunua haka kadude mwasema,ni mali yangu mfano nayaka nikatumie kwenye frem ya biashara pamoja na hom (geto) je naweza kukatumia hako kadude kamoja sehemu,mbili tofauti?
 
Hicho ni Mali yako unahama nacho popote pale kama unavyohama na feni lako
sawa nachosemea

fremu ya biashara iko mbali na nnapoishi

na kote nimepanga

nimenunua kimoja tu je naweza kukitumia sehemu mbili tofauti kimazingira
 
Mim kuna nyumba nlikuwa nakaa ilifika kipindi tunapiga ngumi kabisa kwa sababu ya umeme mwenye nyumba akaamua kufunga hivyo vimeter kila mlango wa chumba

Tulichokifanya umeme ukiisha mnanunua umeme wote kila mpangaji labda kila mmoja unit 15 tunaweka labda mpo sita kwa hiyo itakuwa 15 x 6 mnatumia ukiisha mnaweka tena sasa hapo mnarecord matumizi yaliyopita labda kimeter changu kimeandika unit 10.00 mwanzo nilinunua unit 15 basi hapo tutatoa 15.00 - 10.00 kwa hiyo mim bado nina umeme unit 5 kama nimenunua tena unt 15 zinajumlishwa nakuwa na unt 20

Kama mwingine alinunua unit 15 tulipofanya mahesabu ikaonekana katumia unit 40 umekula umeme wa watu wallah ukinunua umeme unaulipa

So tuliishi kwa amani hapakuwa na ugomvi tena

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
mda mwingine mnajihisi mpo kwa putin kuna watu ni wabishi kulipia umeme
 
@TANESCO watwambie
 
Kinauzwa bei Gani?
Kuna gharama zozote za kukifunga?
 
Kinauzwa bei Gani?
Kuna gharama zozote za kukifunga?
Kuna aina mbili vipo vya kizamani ni tsh 20000 ambavyo havihitaji tokeni; kile cha tokeni Wauzaji huwa wanauza 150,000/=
Hapo bado gharama za waya wa kufanyia diversion ili kutenganisha approximately 20,000/= na gharama za ufundi 10000/=
Note; kinasaidia kiasi chake endapo mtakubaliana kwa pamoja na wenzio kuzingatia vigezo na masharti UNLESS otherwise kama unataka tiba ya kero kwa 100% msijuane weka LUKU YAKO full stop
 
Hapo kwenye Red ndio umenena
 
Hakuna cha mikonga mingi.ni mkonga mmoja tu wakuegemeza hizo nyaya mbili kama kawaida ila nyaya zinakua na junction kutoka mita moja kwenda nyingine.Yako majengo mengi tu kila chumba kina mita yake inayojitegemea.
 
Hivyo vi mita pamoja nakwamba vimeboreshwa ila bado havijatatua tatizo la msingi la changamoto za umeme wa kitanzania.Tatizo ni kwamba hizi technolojia inatengenezwa kwenye mazingira ambayo sio ya kwetu ndo maana unaona bado kuna hizo changamoto.Tanesco walipaswa kuja na ufumbuzi kwakutengeneza meta ndogo ndogo zenye mifumo yote ya umeme zinazojitegemea na mwananchi aweze kuipata kwa urahisi.Ilo litaondoa hiyo kero ya nyumba za kupanga na itaingiza pesa zakutosha kuanzia mauzo ya mita hadi tozo zenyewe.Kinachofanyika sasa ni kununua bidhaa za watu zisizotatua tatizo la msingi.
 
Hicho Cha kizamani kina Sifa Gani?
Je,kinasoma tu tokeni au Kuna Cha ziada yaani kujipimia unit?

NAOMBA unipe maelezo mazuri kusudi niwafungie wapangaji wangu.
 
Uongo. Wewe ni fundi umeme kweli, separate meter kazi yake ni kuhesabu matumizi ya mtu tu haina uwezo mwingine wowote
 
Uongo. Wewe ni fundi umeme kweli, separate meter kazi yake ni kuhesabu matumizi ya mtu tu haina uwezo mwingine wowote
Mi nikajua tunazungumzia matumizi ya umeme kumbe wewe unazungumzia matumizi ya MTU, Basi sawa!
Separate meter zilizoboreshwa ndizo tulizokuwa tunazungmzia hapa
 
Hicho Cha kizamani kina Sifa Gani?
Je,kinasoma tu tokeni au Kuna Cha ziada yaani kujipimia unit?

NAOMBA unipe maelezo mazuri kusudi niwafungie wapangaji wangu.
Cha zamani kinahesabu unit kama bill ya maji ilivyo! Continually! Hakistop kama last months uliishia unit 75 next kinaendelea 76,77,78.... Hivyo inakulazimu uwe na daftali kurekodi ilipoishia ili utoe unit za nyuma kupata idadi ya unit alizo tumia ndipo umuombe pesa kulingana na matumizi yake.

Kifupi ni kama ilivyo mita ya maji! Changamoto ni pale mpangaji atakubishia kwamba umekosea ndipo mtapasuana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…