Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
Kukata mzizi wa fitina waambie wakujengee tu ili utajirike.......usipoona ukaehuka kwa kupoteza fedha. Technology ya green house ipo kweli na ni nzuri sana lakini haiendi kirahisi rahisi na kwa faida kubwa kama hawa jamaa wanavyopamba!
Yaani ukipitia hii thread unaona Kabisa challenge tuliyonayo Kama taifa. Jamani hivi kwanini tusijijengee hata utaratibu wa kujisomea? Maana hizi information zimejaa kwenye mitandao. It's really sad kuona hata elimu tuliyonayo haitusaidii.
tutaajiliwa mpaka lini kwa hii mishahara ambayo haitoshi hata kulipia kodi ya nyumba?
kwa kweli elimu ni muhimu. Lakini hii elimu ya Akina Mulugo sijui itatupeleka wapi Kama taifa.
Baada ya kuangalia mchanganuo wa gharama za kujenga greenhouse katika kitabu chako nilikuwa na wasiwasi nazo hasa kuhusu vifaa kadhaa kama vile UV plastics kwa ajili ya kujengea greenhouse. Nikaamua kufanya research kama hii ni kweli. Nilipiga simu kwa rafiki yangu mmoja yuko arusha ambaye nilisoma nae, yeye ana greenhouse nyumbani kwake. Nikamwelezea mchanganuo wako akasema kuwa uko sahihi kwa asilimia 95. Alisema kuwa hizo UV plastics ambazo ninaongelea yeye alizinunua pale arusha kampuni inaitwa Balton, unaweza google maana sina mawasiliano yao, ambapo yeye alinunua hizo plastics kwa sh. 1350 kwa sq. meter. Hivyo kama najenga greenhouse ya 10X20 basi gharama yake inakuwa sh. 270,000
Pia nimependa wazo lako la kutumia neti za kulalia kujengea ukuta wa greenhouse hasa katika maeneo ya joto kwa kuwa hiyo inapunguza sana gharama. Hivyo nkuu uko sahihi.
garama za ku endesha kilimo cha nyanya ni kiasi gani kwa mwaka mzima ndani ya hiyo green house? soko la nyanya je? msiku wa kupanda na kuvuna je? maana kwa sasa tenga la nyanya iringa ni elfu 3. na huwezi uza bila dalali. kwanini msinikopeahe na nilipe taratibu wakati wa mavuno if tje project is worth?
Unfortunately uyoga(mushrooms) hayakuzwi kwa greenhouse. The required environment for mushrooms is a dark room that has very high levels of humidity. The greenhouse has the opposite effect.Hivi hiyo GH (Green House) inafaa Kwa Kilimo cha Uyoga?
Ndugu zangu watanzania naomba nitoe tahadhali kuhusu uanzishwaji wa greenhouse hasa haya yanayotangazwa kibiashara kabla ya kufanya uamuzi wa kuyanunua nawaomba mpate ushauri kutoka kwa wataalam wa kilimo. kuna mambo ya msingi sana yanatakiwa yazingatiwe emissivity na transmissivity ya cladding/greenhouse cover ni muhimu sana wafanyabiashara wengi wamekuwa wakidanganya hivyo kupunguza efficiency ya greenhouse yenyewe. pia greenouse inategemea na location uliyopo, hali ya hewa na availability ya resources. mimi ni mtaalam wa kilimo ambaye kwa sasa nasomea greenhouse hort nchini uholanz be careful my people.
Agric pays Do it.
Sikufundishi...na mchango wangu usione nakuharibia dili lakini nikupe reference kidogo...
Kuna bwana mmoja, ngosha alitoka Mwanza kuja mjini kujaribu bahati yake...Akajiingiza kwenye biashara ya kuuza nafaka na bidhaa nyingine za chakula Kariakoo, kwa kuwa hakuwa wa kwanza kwenye biashara hiyo na kwa kutambua kwamba ushindani wa kibiashara ulikuwa mkubwa akaamua kuwaza tofauti na wafanya biashara wakongwe aliowakuta pale...
Kuna mama lishe wengi ambao walikuwa na wateja wengi ila walishindwa kuwakidhi kutokana na mitaji midogo ama kutokuwa nayo kabisa, hivyo jamaa aliamua kila siku kuwapatia mama lishe hao mahitaji yote ya siku, kuanzia unga wa Maandazi/chapati asubuhi hadi mchele na maharage ya jioni...wakapika, wakafanya biashara...
Kesho yake kabla ya kupewa mahitaji mengine ilibidi ulipe kwanza yale ya jana yake (kutokana na hela ya mauzo) kisha ndiyo upewe mapya...guess what! Yule bwana leo ana fedha, na wale mama lishe wanajimudu, hawakopi tena na wameweza hata kusaidia familia zao...
Sasa basi ikiwa unaweza kumjengea mkulima miundo mbinu inayogharimu Mil. 5 ili apande nyanya and likely, ndani ya mwaka aweze ku gain mil 20 kwanini msingewajengea wengi kwa kadiri ya uwezo wenu na kuwaelekeza namna bora ya kilimo ili bbda ya mwaka wauze wakupeni milioni zenu tano nao kubaki na kifuta jasho cha mil 15? Yeye mtaji wake uwe ni eneo na nguvu kazi...ni wazo tu!
Elimu ni mtaji hautolewi bure nimetoa tahadhali na way forward mpate consultation ya mabwana shamba kabla hamjaingia katika kilimo hicho unataka msaada gani tena. Mabwana shamba mnao kila kata na kijiji/mtaa lkn mnashindwa kuwatumia halafu mnailalamikia serikali wake up kijana.pamoja na kudai unasomea greenhouse hort. elimu yako haujatoa msaada wowote hapa.bora ungepita kimya kimya
Kaka hiyo ni biashara,sio ruzuku wala msaada. Hakuna mfanyabiashara ambaye atakupa wewe mali umrudishie baada ya mwaka!!
Nenda uchina utakuta hizo nyumba zinauzwa madukani si chini ya dola 2000.
Tupo kwenye soko huria la mitaji,Mbona selikali yenu inashindwa wakopesha mbolea mnanunua kwa ruzuku.
Elimu ni mtaji hautolewi bure nimetoa tahadhali na way forward mpate consultation ya mabwana shamba kabla hamjaingia katika kilimo hicho unataka msaada gani tena. Mabwana shamba mnao kila kata na kijiji/mtaa lkn mnashindwa kuwatumia halafu mnailalamikia serikali wake up kijana.
China ni mtoto aliyelelewa kwenye ndoa iliyokuwa na wazazi wenye msimamo mkali...Tanzania iliwahi kuwa na baba,hamkumwelewa...akamaliza kazi yake na kwenda...sasa ina wenyewe...imeshauzwa, ukipata muda pitia kwa mjumbe wako wa nyumba kumi ukachukue elfu nne kama yako!
Nimependa sana kwa kweli....,najipanga..
Nikishanunua kitabu chako na kukisoma, kama ntakuwa nahitaji msaada zaidi hasa wa ushauri, unaweza nihudumia?
Baada ya kuangalia mchanganuo wa gharama za kujenga greenhouse katika kitabu chako nilikuwa na wasiwasi nazo hasa kuhusu vifaa kadhaa kama vile UV plastics kwa ajili ya kujengea greenhouse. Nikaamua kufanya research kama hii ni kweli. Nilipiga simu kwa rafiki yangu mmoja yuko arusha ambaye nilisoma nae, yeye ana greenhouse nyumbani kwake. Nikamwelezea mchanganuo wako akasema kuwa uko sahihi kwa asilimia 95. Alisema kuwa hizo UV plastics ambazo ninaongelea yeye alizinunua pale arusha kampuni inaitwa Balton, unaweza google maana sina mawasiliano yao, ambapo yeye alinunua hizo plastics kwa sh. 1350 kwa sq. meter. Hivyo kama najenga greenhouse ya 10X20 basi gharama yake inakuwa sh. 270,000
Pia nimependa wazo lako la kutumia neti za kulalia kujengea ukuta wa greenhouse hasa katika maeneo ya joto kwa kuwa hiyo inapunguza sana gharama. Hivyo nkuu uko sahihi.