Sikufundishi...na mchango wangu usione nakuharibia dili lakini nikupe reference kidogo...
Kuna bwana mmoja, ngosha alitoka Mwanza kuja mjini kujaribu bahati yake...Akajiingiza kwenye biashara ya kuuza nafaka na bidhaa nyingine za chakula Kariakoo, kwa kuwa hakuwa wa kwanza kwenye biashara hiyo na kwa kutambua kwamba ushindani wa kibiashara ulikuwa mkubwa akaamua kuwaza tofauti na wafanya biashara wakongwe aliowakuta pale...
Kuna mama lishe wengi ambao walikuwa na wateja wengi ila walishindwa kuwakidhi kutokana na mitaji midogo ama kutokuwa nayo kabisa, hivyo jamaa aliamua kila siku kuwapatia mama lishe hao mahitaji yote ya siku, kuanzia unga wa Maandazi/chapati asubuhi hadi mchele na maharage ya jioni...wakapika, wakafanya biashara...
Kesho yake kabla ya kupewa mahitaji mengine ilibidi ulipe kwanza yale ya jana yake (kutokana na hela ya mauzo) kisha ndiyo upewe mapya...guess what! Yule bwana leo ana fedha, na wale mama lishe wanajimudu, hawakopi tena na wameweza hata kusaidia familia zao...
Sasa basi ikiwa unaweza kumjengea mkulima miundo mbinu inayogharimu Mil. 5 ili apande nyanya and likely, ndani ya mwaka aweze ku gain mil 20 kwanini msingewajengea wengi kwa kadiri ya uwezo wenu na kuwaelekeza namna bora ya kilimo ili bbda ya mwaka wauze wakupeni milioni zenu tano nao kubaki na kifuta jasho cha mil 15? Yeye mtaji wake uwe ni eneo na nguvu kazi...ni wazo tu!