Stevery2
JF-Expert Member
- Mar 3, 2012
- 397
- 46
Wazo zuri kwa kupambana na umasikini linatekelezeka. Fanyieni kazi wahusika
Umeona kaka?hapo jenga alafu wekeanen mikataba,mwisho unalipwa nayeye anajipatia kilicho chake.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wazo zuri kwa kupambana na umasikini linatekelezeka. Fanyieni kazi wahusika
KWA NINI UWE MASKINI?
JE, UNGEPENDA KUVUNA NYANYA NYINGI KILA WIKI NA KUJIPATA KIPATO KIKUBWA KUPITIA KILIMO CHA GREEN HOUSE?
View attachment 165705
Team ya AMKA NA BADILIKA ya CONSNET GROUP ikishirikiana na wataalamu wa GREEN HOUSE katika maeneo ya joto AFFORDABLE GREENHOUSE kutoka Kenya wanapenda kukujulisha kuwa unaweza kujengewa GREEN HOUSE ya ukubwa wa Mita 8 kwa Mita 15 na kupanda mazao upendayo ya bustani kama Nyanya; Pilipili Hoho; Vitunguu; Bilinganya; Vitunguu; Matango nk ambayo yanaweza kukupatia zaidi ya tani zaidi ya 20 kwa Mwaka na kukuingizia kipato kikubwa.
Kujengewa GREEN HOUSE moja ya 8M X 15 M (Kutumia mirunda na mbao za dawa) ni TZS 5.0 Millions Tu na unajengewa katika kipindi cha wiki 2 pamoja na kupandiwa mazao. Pesa hiyo inahusisha mbegu za kisasa, mbolea, madawa, kupima udongo na maji maabara, tank la lita 1000, drip irrigation system, na mafunzo na kujengewa.
Kwa sasa zipo KITS za kutosha za Green House. Kama utapenda kujengewa Green House na bajeti iko tayari, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba: +255 755 285 023.
Nakuelewa kaka but without basic knowledge and update info practical experience doesn't make any success and its our government policy to use their expertise to approve any new technology come into her people. I wish I could be in Tz I think I could use you to change our agric. GoodluckMkuu, ukiongelea real experience ya Green House, siwezi nikasema tuna Wataalamu waliobobea kwa vitendo zaidi ya thory nyingi tu. Na ndiyo maana hata baadhi ya hao mabwana shamba leo hii wanakuja na kuomba kujengewa greenhouse!
We trust in practical experience and attitude which makes more than 90% of life success other than the theory and books which counts on less than 10% success. Furthermore materials in the books can change but what you experience is evidential.
Mkuu niko interested tena 5 M sio nyingi kwa package hiyo. Tatizo hiyo hela sina. Nifanyeje? Ngoja nianzae kudunduliza. Hawakopeshi? At least mtu alipe nusu halafu nusu iliyobaki ulipe ukivuna? I am very much interested.
Kwenye kuezeka naona kama umekosea, juu hakuezekwi flat kama vile box, Bali kunakua na mgongo, hivyo gharama zitaongezeka.
Na Kwenye ukuta wa chini, je ni kweli wadudu hawapiti kwenye matundu ya chandarua? Vipi durability ya Net kwenye sehemu yenye upepo?
Kwenye ishu ya upepo hapo sijui labda muulize mtoa mada labda atakuelekeza
tutaajiliwa mpaka lini kwa hii mishahara ambayo haitoshi hata kulipia kodi ya nyumba?
Ila inabidi pia ukumbuke kuwa biashara nyingi za bongo magumashi mengi sana. Watu wakikueleza ukweli ni namna gani wametoboa unaweza kubaki mdomo wazi!!!Yaani nikishaona mtu katika biashara zetu za kawaida anaingiza mawazo ya kina Adam Smith, Mara sijui return of investment, accounting rate of return na mengine kama hayo, huyo hata umpe 1,000,000,000 afanye biashara kesho yake tu anafilisika. Na kawaida watu hao wengi unawakuta ana MBA au amesomea "masomo ya biashara", anadhani biashara ni vitabu, kibongobongo wanaotoboa katika biashara hata Adam Smith hamjui wala Hana mpango wa kumjua milele! Muuzlie S.H. Amon kama anamjua Adam Smith!
Hii naigeuza kuwa halisi now. I mean now!
Sanctus Mtsimbe,
Mnamo miezi michache iliyopita katika kipindi chako kinachorusha TBC ulimuhoji member mwenzetu humu Abdulatif GreenHouse kuhusu kilimo hiki cha Greenhouse. Hiyo ilikua ni baada ya Abdulatif kuleta Uzi wake hapa kuhusu kilimo hicho na uzi ukapata supporters wengi tu.
Sasa tuambie;
1) baada ya kumuhoji then ukavutiwa na idea yake then ukaamua kui-implement?
2) Wewe ni middle man, unachukua 5mil kwa wateja then unaenda kumpa Abdulatif kwa lower cost?
3) Ideas zimegongana?
Pia umezungumza mengi mazuri ya greenhouse farming, je una elimu, ujuzi na uzoefu wowote wa hiki kilimo? Kama ndio basi kwa muda gani?
pamoja na kudai unasomea greenhouse hort. elimu yako haujatoa msaada wowote hapa.bora ungepita kimya kimya