Mafunzo ya kutengeneza mkaa wa kisasa

Status
Not open for further replies.

Inategemea uko eneo gai, ila gharama ya kutengeneza gunia 1 kubwa kabisa la mkaa ni sh 3500 hivyo utapanga mwenyewe hapo ni bei gani uwauzie hao wateja wako kulingana na eneo uliopo.
 
mkuu hiyo costs ya 3500/- unsifikiaje. maana huu uji unapikwa na kuni au mkaa. haya mabaki ya jivu jeusi utayapata either kuyafata mashambani uje uyachome nk au kuuziwa. halikadhalika chenga za mkaa.ili uupate unga wake lazima utumie muda kuuponda nk..je muda wote huu umeupa gharama gani..point yangu hapa naona vifaa inawezekana havina bei lakini muda unaotumika kulipata hilo gunia moja ndio tatizo kubwa
 
bw biashara umefikia wapi katika yale majaribio yako ya zile chemicals zinazosaidia kuongeza ubora wa mkaa?

Nimefikia maamuzi kuwa chemicals sio za lazima kuziweka katika process nzima ya uzalishaji wa mkaa wako kwa sababu kadhaa. Chokaa kazi yake inafanya mkaa uwe mweupe pale ambapo umeuwasha na uko tayari kupikiwa. Ni kama kitu kinachokusaidia kukueleza kuwa mkaa wako ushakolea moto hivyo uko tayari kupikiwa. Tatizo ni kwamba inafanya mkaa wako uwe mweupe kitu ambacho wateja hawakipendi

Sodium nitrate inafanya mkaa wako kuwaka haraka ila kutokana na bei yake madukani inafanya gharama yake iongezeke maradufu hivyo sioni umuhimu wa kuitumia

calcium carbonate inawekwa ili kuongeza muda wa mkaa kupikia. Ila muda inaouongeza ni dk chache sana hivyo sio muhimu sana kutumika ukizingatia bei yake ni kubwa madukani

Hivyo ni kwamba utengenezaji wa nkaa bila hizi chemicals kuongezwa ndio njia sahihi kabisa ya uzalishaji mkaa. Mkaa wako utakuwa umezalishwa kwa gharama ndogo hivyo ni faida kwako na ubora wake ni wa juu kuliko mkaa wa kawaida. Hivyo inashauriwa na wataalamu kufuata maelekwezo niliyoyaandika kwenye kitabu ili kutengeneza mkaa mzuri na wa kisasa
 

Ndio maana hapo nikasema kuwa inategemea na sehemu ambayo unapata hizo materials. Mimi kiwanda changu kiko kibaha ambapo bei ya raw materials inatofautiana na dar au arusha. Huku chenga za jivu unaweza pata hata bure kwa kuwa ziko ntingi na uzalishaji wa mkaa wa kawaida ndio unafanyika maeneo ya huku. Mimi sasa hivi natumia maranda zaidi na kwa kuwa nachukua mengi nanunua gunia 1 sh. 600. Nikiprocess magunia 3 natengeneza guunia 1 la mkaa. Ukichanganya na gharama nyingine inafika 3500.

Ishu ya muda hiyo huwezi juikimbia maana mkaa unahitaji muda kuutengeneza. Pia inategemea na eneo ulipo kama nilivyosema mwanzo. Km eneo lako liko mbali na raw materials basi utatumia muda na gharama kubwa kukusanya raw materials tofauti na yule aliyeko karibu na raw materials. Kiwanda changu mimi kiko karibu kabisa na raw materials zote
 
Uko Kibaha sehemu gani? nataka nikutembelee.
 

mjin shule mwanangu jembe la nn?

Una id saba zote unazifanyia kazi duh.
 
Tripple A, huamini unaacha. Kweli ukifuatilia sana comments za watu humu huwezi fanikiwa.

Zilipotoka nafasi z ajira viettel watu walikandia sana na wengine wakaweka uzi kabisa kusema jama ni matapeli. Niliomba kazi pale nikaitwa kwenye interview ya online.
Ile interview ilifanyikia IFM, tena ikawa nongwa kuwa jamaa hawana hata ofisi. Tukaiwa kwenye oral ofisini kwao, sasa midomo ya watu kama nyie ikafungwa kabisa. Saa hizi sibabaishwi na maoni kama yako.
Mimi ni mwenyeji wa Mbeya na sasa niko dar kijitonyama. Biashara yuko kibaha ukitaka kamwone huko na ukitaka njoo kwangu au mwone lotti yeye yuko tabata au kama uko arusha mwone mwana ally. Lakini wa kwanza kutna na Biashara2000. Huji kwangu bila kukutana naye au kuwasiliana naye maana ntakuuliza maswali ambayo ukijikanyaga najua unataka kukwepa hiyo 10000 wakati kwenda kulewa au kununua malaya unatumia zaidi ya laki. Hutaki biashara, acha na funga domo fullstop
 

Well said my friend. Ukitaka kujua mtu ambaye amekuwa maisha yake yote akionewa na kubanwa utamjua tu maana anapopewa uhuru wa kuongea mtandaoni utaona comments zake tu. Huwa ni watu waliojawa na negativity kwenye akili zao. Mfano huyu bluetooth angalia posts zake nyingine ktk jf utajua tu character yake. kumbuka huwezi ridhisha mtu sana sana waache waendelee kupoteza pesa zao kwenye internet cafe. we make money
 
Kwa yule aliyeulizia kuhusu dryer ya mkaa, kuna jamaa yangu yuko iringa sasa kutokana na hali ya hewa ya kule ilivyo akaamua kujenga tanuru kama lile la kuchomea matofali ila kubwa kwa ajili ya kuanikia mkaa na inakausha siku hiyo hiyo. Nawe unaweza tumia ujanja huo
 

Hahahaaa. Kweli kabisa kaka
 

Nmefanikiwa kuutengeneza mkaa nashukur kwakweli unawaka vizuri,nafanya sample ingine sasa
 

Yaaah kweli mama angu maan hata mimi nilitumia mda kweli kutwanga mpaka nikawaza hvi hakunaga mashine ya kusaga chenga cha mkaa?maana hapa nilipo mimikupata chenga. Ni rahisi sana kuliko maaranda
 

mtaji 5,000/=
Kipato kwa siku 30,000/=
Kipato kwa mwezi 30,000 x 30 = 900,000/=
Gharama za malighafi.......?????
Upatikanaji wa malighafi......?????

Mkaa wa kisasa au mkaa mbadala?

Asante kwa teknolojia mupya mukuu!
 
Yaaah kweli mama angu maan hata mimi nilitumia mda kweli kutwanga mpaka nikawaza hvi hakunaga mashine ya kusaga chenga cha mkaa?maana hapa nilipo mimikupata chenga. Ni rahisi sana kuliko maaranda
Hizo milling machine zipo mkuu reen elius zinarahisisha sana. hata mixing machine pia zipo ila ni mtaji tu. ukiwa na mtaji mzuri unafanya production kubwa na bora zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Hizo milling machine zipo mkuu reen elius zinarahisisha sana. hata mixing machine pia zipo ila ni mtaji tu. ukiwa na mtaji mzuri unafanya production kubwa na bora zaidi.

Daah asante sana mkuu kama zipo znauzwaje? Nijue bei zake ili nione kama naweza kuhandle ama vipi
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…