Tokea uliponitumia DVD za mafunzo ya mkaa, greenhouse pamoja na ile ya ofa ya bure ya kilimo cha maua kinacholipa, naamini kuwa maisha yangu siku si nyingi yatakuwa mazuri Mungu akijaalia. Nilippokea ile DVD ya maua sikuiangalia kwa kuwa nilikuwa nataka nianzishe mradi wa mkaa na greenhouse. Ila shangazi yangu ambaye ni bwana shamba kule sakina Arusha alipokuja huku Moro kwenye sherehe ya kifamilia, akawa ananisimulia jinsi anavyowasaidia wakulima mbalimbali kule Arusha. Nikamweleza kuhusu mipango yangu ya miradi. Akanishauri nianze miradi ya mkaa na kilimo cha maua kwa wakati mmoja kwa kuwa yote naweza anza na mitaji midogo. Na pia atanisaidia kupata masok ya maua kwa kuwa yeye ameshajuana na wafanyabiashara wengi wa maua mjini Arusha.
Nimeshaanza mradi wa mkaa na wa maua. Hapo chini utaona picha ya sehemu ya shamba langu la maua. Nina eneo la mita 20 kwa 35 (20x35) miche niliyopanda mpaka sasa ni miche 105,000 ila kutokana na eneo lenyewe nililopo kuna wafugaji wanafuga karibu hivyo kuna uwezekano angalau miche 5000 ikaliwa na mbuzi ingawa najaribu kulinda mimea yangu, hivyo kuna uwezekano nikavuna miche 100,000 na kama nitauza kwa bei iliyopo ya sh. 25 kwa mche ntapata sh, 2,500,000 kila baada ya miezi 3. Baadae ntaanza kutumia ile tekniki yako ya kupanda na kuweza kuvuna kila baada ya wiki 2 badala ya kila baada ya miezi 3. Ila hata hvyo kupata sh. 2,500,000 kila baada ya miezi 3 ni kubwa sana kulinganisha na mshahara wangu wa kuajiriwa. Ubarikiwe sana bw. Biashara2000.