Mafunzo ya kutengeneza mkaa wa kisasa

Mafunzo ya kutengeneza mkaa wa kisasa

Status
Not open for further replies.
kweli hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke..mkaa wangu leo umewaka lakin c kwq kiwqngo cha kuridhisha kwq sabb ulikua unainekana kupoa sana,ila bado naendelea kufanya marekebisho mpaka kieleweke

Kuna mahali inaonekana unakosea maana watu wengi huwa hauwasumbui sana kuutengeneza. Hebu achana na zile ratios na tumia yale maelekezo niliyoyaandika kwenye kitabu yale ya makadirio. Tumia hayo maelekezo kwa uangalifu na relax ufanye taratibu tu utakuwa vizuri usiwe na haraka. Jaribu hivyo then utanitaarifu
 
Kuna mahali inaonekana unakosea maana watu wengi huwa hauwasumbui sana kuutengeneza. Hebu achana na zile ratios na tumia yale maelekezo niliyoyaandika kwenye kitabu yale ya makadirio. Tumia hayo maelekezo kwa uangalifu na relax ufanye taratibu tu utakuwa vizuri usiwe na haraka. Jaribu hivyo then utanitaarifu
sawq mkuu ila natumaini huu saivi utakua poa tulishea idea na bwn mbepo myamba
 
naona tatizo lako ndio nililonalo mimi,una majivu sana na moshi pia wa kwangu cjajua bado nirekebishe nn!
 
Za asubuhi wapendwa..mimi naendelea kumshukuru mungu kuwa naona mambo mazuri. Jana nilitumia mkaa ambao nilianza kama majaribio kwa kutumia kamachine kadogo. Nimeuanika kwa muda mrefu unawaka 1. vizuri 2.unakaa kwa muda mrefu bila kuzima..shida ninayoona ni majivu mengi.
 

Attachments

  • 1410502681730.jpg
    1410502681730.jpg
    70.4 KB · Views: 150
  • 1410502701859.jpg
    1410502701859.jpg
    40.1 KB · Views: 135
  • 1410502728268.jpg
    1410502728268.jpg
    70.3 KB · Views: 157
kitabu kinauzwaje... n vip soft copy zinaeza patikana alafu transaction zikafanyika
 
Za asubuhi wapendwa..mimi naendelea kumshukuru mungu kuwa naona mambo mazuri. Jana nilitumia mkaa ambao nilianza kama majaribio kwa kutumia kamachine kadogo. Nimeuanika kwa muda mrefu unawaka 1. vizuri 2.unakaa kwa muda mrefu bila kuzima..shida ninayoona ni majivu mengi.

uzuri wa mkaa huu majivu yake hayapukutiki hata ukimaliza kupikia unabaki katika shepu yake ile ile km vile wakati unauweka mwanzo. Hii inakurahisishia kuubeba na kwenda kuumwaga. Haupukutiki kama mkaa wa kawaida
 
Semeni basi kuhusu oven...napataje..mi huku niliko kuna siku jua halipo kabisaa
 
Jipange na utengeneze solar dryer itakusaidia mala dufu , na ni lahisi kutengeneza
 
Asante Ngamba..nipe muongozo je naipataje..umesema ni rahisi kutengeneza..naomba msaada tafadhali

Unaweza kwenda pale sido vingunguti ukifika pale getini ulizia jamaa anayetengeneza majiko watakupeleka kwenye karakana yake. Jamaa huwa anatengeneza majiko na ovens. Huyu pia anatengeneza kitu chochote kinachohitaji kuzalisha joto. Hivyo unaweza nenda pale ukamwelezea unataka kutengenezea oven au dryer ya mkaa naye atakupa estimate.

Ila kwa experience yangu ni kwamba mpaka sasa mimi sina oven na mkaa unakauka ila tu katika kipindi cha mvua inabidi nianike hadi siku 5 ili ukauke kabisa. Unakuwa tu na mfanyakazi wako ambaye yuko stand by akiona manyunyu yanaanza kudondoka tu anachukua plastic cover kubwa na kwenda kuyafunika. Mvua ikiisha anafunua. Unaweza nawe kufanya hivyo wakati ukisubiria mradi wako ukue ili uweze kutengeneza dryer.

Kwa experience ni kuwa ukitaka mambo yako yaende vizuri, weka focus ktk sehemu moja at a time. Usitake kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja, inakuwa ngumu kusonga mvele. Anza kwanza kuboresha product yako iwe bora, hii itaongeza wateja, utapata mapato ya kutosha, hatua inayofuata unapanua soko then unatengeneza dryer. Usitake kutafuta dryer wakati hata mkaa wenyewe hujaanzza kuuza kwa kuwa haujaridhika nao. Boresha kwanza product yako then mambo mengine yatafuata.
 
Watu wengi wamekuwa wakinipigia simu wakiwa na ishu mbalimbali wakihitaji ushauri na asilimia 95 ya watu hao kuna sehemu hapa na pale walikuwa wamekosea katika process nzima ya kutengeneza mkaa na baada ya ushauri mambo yao yameenda vizuri. Ili kuondoa matatizo mengi katika utengenezaji wa mkaa huu fanya mambo kadhaa lakini muhimu zaidi ni kufuata maelekeza yaliyoko kwenye kitabu kwa uangalifu.

1. Hakikisha raw materials ulizonazo hazina mchanga. Mchanga kazi yake ni kuzima moto hivyo ukiuchanganya kwenye raw materials yako unaua nguvu yake na haukai wakati wa kupikia

2. Hakikisha kila raw material yako imekuwa processed vizuri. Kusiwe na kitu kingine chochote katika mchanganyiko wako ambacho sio raw material. Mfano kikuwa na kipande cha jani katika mchanganyiko wako, utakapokuwa unapikia mkaa wako kile kipande cha jani kitatoa moshi mweusi kwa kuwa kitakuwa kinaungua

3. Hakikisha mkaa wako umekauka vizuri mpaka ndani kabla haujautoa juani. Mkaa unaweza kuwa umekauka nje ila kwa ndani bado. Chukua kipande kimoja na kipasue uangalie ndani. Kama kuna unyevu uache uendelee kukauka km hakuna unyevu basi uko sawa kwenda kuuza au kupikia

4. Kwa wale wanaotumia mkono na si mashine ktk kutengeneza mkaa, usitumie ratio yoyote maana zximekuwa zikiwachanganye wengi. Tumia ile njia ya kukadiria na kupima kwa kiganja inayoelezewa vizuri kwenye kitabu. Wenye mashine wao itabidi watumie ile ration ya 1 kwa 10

5. Hakikisha jivu unalotumia kutengenezea mkaa wako ni jeusi na si jeupe au kijivu. Jeupe au kijivu halina nguvu
 
bw biashara umefikia wapi katika yale majaribio yako ya zile chemicals zinazosaidia kuongeza ubora wa mkaa?
 
Ndugu biashara2000 kwanza pole na majukumu mazito ya kutusaidia sisi wajasiliamali wa hapa bongo.
Bwana biashara2000, mimi kuna ishu najiuliza sana kuhusu upatikanaji wa masoko, hapa MBEYA gunia moja la mkaa ni kuanzia Tsh.25,000 mpaka Tsh.27,000. Je naweza kutengeneza faida kweli kwenye hii mambo. Naomba unisaidie ili nijikwamue kiuchumi,
Natanguliza shukrani za dhati

.made in mby city.
 
kweli hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke..mkaa wangu leo umewaka lakin c kwq kiwqngo cha kuridhisha kwq sabb ulikua unaonekana kupoa sana,ila bado naendelea kufanya marekebisho mpaka kieleweke
Mkaa wangu nlioufanyia marekebisho baada ya kua na kasoro sample za mwanzo leo nimeujaribu umewaka vizuri leo walipikia maharage na ukaivisha bado naendelea kuutengeneza mwngne kwa majaribio nikiridhika ntapeleka kwny soko kwa majaribio
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom