Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Nimepitia mitandao ya kijamii leo, na habari zilizotamalaki ni makada wa CCM kuchukua fomu. Ni wazi sasa wimbo wa "Tunazima zote, tunawasha kijani" leo umepata maana halisi.
Mwitikio huu mkubwa unatoa uthibitisho wa ukweli wa takwimu kuwa hiki ndicho chama chenye wanachama wengi zaidi nchini. Mtakumbuka, katika mkutano mkuu wa CCM uliopita, Mwenyekiti wa CCM taifa, alieleza kuwa mpaka wakati huo CCM ilikuwa na wanachama milioni 13.
Kugombea ni mradi, kunahitaji tathmini ya uwezekano wakufikia safari yako ya matumaini. Ukianza safari ya kutafuta udiwani, ubunge na hata urais ni lazima upande gari imara kujihakikishia safari yenye mafanikio, ukipanda bovu, hufiki! Utitiri wa watia nia kuchukua fomu CCM ni ushahidi wa wazi kuwa wanaamini chama chenye uhakika wa kuwafikisha kwenye ndoto zao za uongozi ni CCM.
Vyama vya upinzani vinao wajibu wakujifunza kutoka CCM namna bora ya kuvijenga vyama vyao kuwa taasisi imara za kisiasa. Wahenga walitufunza, baniani mbaya kiatu chake dawa.
Nawatakia kila la kheri watia nia wote, ndani na nje ya CCM. Ni imani yangu wagombea wa CCM watafanya vizuri katika uchaguzi huu.