GE2025 Mafuriko ya uchukuaji fomu ni kipimo cha nguvu ya CCM

GE2025 Mafuriko ya uchukuaji fomu ni kipimo cha nguvu ya CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nimepitia mitandao ya kijamii leo, na habari zilizotamalaki ni makada wa CCM kuchukua fomu. Ni wazi sasa wimbo wa "Tunazima zote, tunawasha kijani" leo umepata maana halisi.

Mwitikio huu mkubwa unatoa uthibitisho wa ukweli wa takwimu kuwa hiki ndicho chama chenye wanachama wengi zaidi nchini. Mtakumbuka, katika mkutano mkuu wa CCM uliopita, Mwenyekiti wa CCM taifa, alieleza kuwa mpaka wakati huo CCM ilikuwa na wanachama milioni 13.

Kugombea ni mradi, kunahitaji tathmini ya uwezekano wakufikia safari yako ya matumaini. Ukianza safari ya kutafuta udiwani, ubunge na hata urais ni lazima upande gari imara kujihakikishia safari yenye mafanikio, ukipanda bovu, hufiki! Utitiri wa watia nia kuchukua fomu CCM ni ushahidi wa wazi kuwa wanaamini chama chenye uhakika wa kuwafikisha kwenye ndoto zao za uongozi ni CCM.

Vyama vya upinzani vinao wajibu wakujifunza kutoka CCM namna bora ya kuvijenga vyama vyao kuwa taasisi imara za kisiasa. Wahenga walitufunza, baniani mbaya kiatu chake dawa.

Nawatakia kila la kheri watia nia wote, ndani na nje ya CCM. Ni imani yangu wagombea wa CCM watafanya vizuri katika uchaguzi huu.
"Nawatakia kila la kheri watia nia wote, ndani na nje ya CCM. Ni imani yangu wagombea wa CCM watafanya vizuri katika uchaguzi huu".

Ukiwatakia kila la kheri watia nia wote maana yake unailewa!!??
Wote wakifanikiwa maana yake unaielewa!!!???
 
Hoja haipigwi rungu bali hujibiwa kwa hoja. Ulipaswa uje na tathmini kuwa kwanini watia nia wengi wameamua kugombea kupitia CCM na sio vyama vingine, **** hulioni hili kuwa ni ushahidi wa wazi wa nguvu ya CCM.
Sababu ccm wanapita billa kupingwa
 
"Nawatakia kila la kheri watia nia wote, ndani na nje ya CCM. Ni imani yangu wagombea wa CCM watafanya vizuri katika uchaguzi huu".

Ukiwatakia kila la kheri watia nia wote maana yake unailewa!!??
Wote wakifanikiwa maana yake unaielewa!!!???
Hawa watiania bila kujali vyama vyao, ni watanzania wenzetu, na wote wanaomba kututumikia sisi watanzania. Kuna ubaya gani tukiwatakia safari njema katika hizo ndoto zao?
 
Hoja haipigwi rungu bali hujibiwa kwa hoja. Ulipaswa uje na tathmini kuwa kwanini watia nia wengi wameamua kugombea kupitia CCM na sio vyama vingine, **** hulioni hili kuwa ni ushahidi wa wazi wa nguvu ya CCM.
Kwamba wewe Dr. ukienda CHAUMA utaonekana hujui kusoma na kuandika hivyo utakosa sifa ya kugombea ubunge au udiwani lakini yule Darasa la kwanza kabisa akiwa CCM ataonekana anajuwa kusoma na kuandika na kuwa na sifa ya kuteuliwa na tume.
Kwanini kusiwepo na mafuriko? Yaani mtu yeyote anayeziba macho na masikio ya kutokuona ukweli kuwa uchaguzi wetu imekosa sifa basi atakuwa na upungufu wa akili.
 
Mwaka kutakapokuwa na tume huru,
Pale dola itapoacha kuhujumu Uchaguzi kwa maslahi ya CCM
Ndipo utakapojua chama chenye nguvu Tanzania ni kipi
 
Hoja haipigwi rungu bali hujibiwa kwa hoja. Ulipaswa uje na tathmini kuwa kwanini watia nia wengi wameamua kugombea kupitia CCM na sio vyama vingine, **** hulioni hili kuwa ni ushahidi wa wazi wa nguvu ya CCM.
Kaka hilo ukiliangalia vizuri lina majibu mengi na mengine sio mazuri. Mtu mmoja alisema, ukisimamisha jiwe na CCM ........
 
Screenshot_2025-06-28-20-38-27-1.png
 
Sasa kama mpaka Sheta, Mkojani, Romy Dj naye amechukua form si ameshaona kuwa ni kama circus vile Bunge la Tanzania limekuwa kama matamasha ya Phineas Taylor Barnum, limekosa tu Tembo 🐘 , na Simba 🦁 ila kila mtu ni Clown 🤡
Watu wanalipwa kwenda kutetea masilahi ya taifa mwisho wake wanakuwa wajinga kuliko hata ambao hawataki kuwa wabunge.

Alichokifanya P. T. Barnum unadhani kina utofauti na ambacho anakifanya Tulia Ackson? Marehemu P. T. Barnum alivyoanzisha Grand Traveling Museum, Menagerie, Caravan & Hippodrome alikuwa na malengo ambayo ndo yamefanyika kwenye Bunge la Tanzania.

Enzi hizo watu kama Charles Stratton ("General Tom Thumb") pamoja na mkewe Lavinia Warren, bila kusahau Minnie na George Washington Morrison Nutt walikuwa wakitoa burudani na kufanya vitu vya mzaha kama vile wabunge wanaokwenda tena kuomba ridhaa ya kurudi kuendelea na vituko.
 
Back
Top Bottom