Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Tanzania kama ilivyo baadhi ya mataifa, imejaliwa kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa zilizo katika maajabu saba ya dunia kwa kuwa na wanyama adimu duniani.
Filamu ya Royal Tour inaonesha vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania Bara kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kwa upande wa Zanzibar, inaonesha hoteli za kitalii ikiwemo iliyoko ndani ya bharai huko Pemba, huku Rais Samia Suluhu akiwa kiongozi wa kutoa maelezo kuhusu vivutio hivyo.
Ni wazi kuwa kwa sasa Watanzania wanashuhudia waziwazi matunda ya Filamu hiyo kutokana na ujio wa ndege nyingi kutoka mataifa mbalimbali zinazofika nchini zikiwa na idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini kutembelea vivutio hivyo.
Ujio wa watalii hao siyo tu umesaidia kuliingizia Taifa fedha za kigeni, bali pia umewezesha kukua kwa uchumi wa mtu mmojammoja wakiwemo waongozaji wa watalii, wamiliki wa hoteli pamoja na akda zingine ambazo kwa namna moja au nyingine zinajishughulisha na sekta hiyo.
Katika hili, Watanzania kwa umoja wetu, hatuna budi kumshukuru Rais Samia kwa kuitangazia dunia kuwa Tanzania ni taifa lenye vivutio vizuri ikijumlishwa na amani iliyonayo pamoja na fursa nyingi za uwekezaji.
Jambo la msingi ni kuzidi kumuombea Rais weu ili malengo yake mbalimbali aliyoyaweka katika taifa hili na wananchi yatimie na nchi izidi kuendelea katika nyanja zote.