Mafuriko ya watalii nchini, nampongeza Rais Samia Suluhu

Sababu iwe yoyote ile kama wanajaa ni jambo jema kwa wakazi wa Kaskazini na jambo jema kwa nchi.
 
Haters watakwambia ni msimu 😆😆

Acheni siasa za bei chee, watalii kwenye miaka yote hii ni high season, ukizingatia na kipindi watu walichokaa ndani kutokana na Covid, kwasasa milango iko wazi, hivyo ni lazima watalii watakuwa wengi. Kwa wasiojua lolote mnaweza kuwaokota.

Kama kweli ni jitihada za rais kuleta hao watalii na sio mazingira yenyewe, mbona hatuoni wawekezaji wengi wakija kufungua viwanda? Au huko kwenye viwanda hajapapigia debe? Kwa bahati mbaya mnadhani watu bado wako usingizini hivyo mnaweza kuwajaza ujinga.
 

Huu utapeli wa kijinga alitaka kuuleta Lowassa kipindi fulani. Nakumbuka alisema ataleta Wathailand watengeneze mvua. Ila alitaka kuwaleta kipindi cha karibu na Masika. Lengo la kutaka kuwaleta kipindi hicho ni ili mvua ya Masika ikianza aseme ni yeye aliwaleta Wathailand wakatengeneza mvua hiyo. Hakuna mtalii anakuja kutokana na huo utapeli wa roho tua.
 
Acha kuingelea Petroli kwenye moto.!
Huu ni msimu wa summer nchi za ulaya na shulee nyingi kuwa zimefungwa. Watu walituma kwenye Corona na kipindi hiki cha mapumziko basi ndio wakati wa kusafiri na familia.
Kutakuwepo na upungufu wa haon watalii ifikapo September kati kuendelea. Kasi unayoiona Sasa hivi haitakuwepo! Ni swala la muda halina hata kupatuka kusifia. Nchi za wenzetu Wana Maendeleo kibao mbona hawamsifui Rais. Ni Kwa sababu kila kiongozi anawajibika eneo lake na Demokrasia iliyoshiba sio Hawa wa Teua / Tengua - Apisha!

Akiteuliwa kiongozi lazima aende kwenye jopo ajieleze anawezaje kuimudu nafasi hiyo na mwisho kupingwa kura za ushindi hakuna kuapisha kesho yake haijalishi hata kama wanatumia mwezi kumjadili mteuliwa.!
 
Kukosa exposure ni kubaya sana. Mbuga za wanyama za Tanzania na Kenya zinajulikana siku nyingi mpaka watalii wamebadilisha neno ''safari'' na kulipa maana ya kutalii mbuga za wanyama. Kwa kifupi hakuna kivutio ambacho kilikuwa hakijulikani. Watalii walikuwa wamesitisha safari kwa wingi kwa sababu ya korona. Hata nchi za Ulaya sasa hivi utalii wa ndani kwa ndani umefumuka utadhani watu wamepagawa. Sasa watu wenye upeo mfupi kama wewe wanashindwa kujua juu ni wapi na chini ni wapi!
 
Ni kipi kipya kilichooneshwa kwenye royal tour na awali hakikuwahi oneshwa? Uvivu wa kufikiri unapelekea kutoa sifa hata pasipo stahili.
 
Royol Tour hapana Kwa mwaka huu labda mwakani

Hivi umewahi kuona documentary za Serengeti zile zinaoneshwa Ile Chanel ya DStv Nat Geo ?

Ukipata bahati ya kuona zile ndio utaamini kuwa Royol Tour haina uwezo wa kujaza watalii kiasi mnachokiwaza
Royal ataour imeleta watalii wengi kwa wakati mmoja, hii haijawahi kutokea.
 
Yaani ni hatari juzi nlikua natoka manyara nlihesabu magari 65 kwa nusu saa yaliyokua yanaelekea ngorongoro
 
sio unafki wala kujipendekeza, mama amefanya kazi kubwa kuhakikisha watalii wanakuja. Huu ndio ukweli
Miaka mitatu nyuma tulikuwa tunapokea watalii wangapi kwa mwaka na sasa wameongezeka kwa kiwango gani
Angalia idadi ya sasa, wingi wao ndani ya muda mchache ndio utaamini kwamba mama ameupiga mwingi.
 
Yaani ni hatari juzi nlikua natoka manyara nlihesabu magari 65 kwa nusu saa yaliyokua yanaelekea ngorongoro
Alafu kuna watu wanabisha kwamba Royal tour haijasaidia kitu kwenye hili. Ukweli lazima usemwe mama Samia Suluhu ameupiga mwingi.
 
sio unafki wala kujipendekeza, mama amefanya kazi kubwa kuhakikisha watalii wanakuja. Huu ndio ukweli

Angalia idadi ya sasa, wingi wao ndani ya muda mchache ndio utaamini kwamba mama ameupiga mwingi.

Unafanya kampun gani ya tours? Fact zako unaongea Kwa base gani?

Me nipo kwenye hizo mambo za utalii, naongea ambacho nakiona,

Wazungu wengi wanafanya book za Safari mwaka mmoja kabla, sasa jiulize hiyo royol tour ina mwaka mmoja?

Nyie ndio wale mnasema hata immigration ya nyumbu this time imekuwa mzuri Sana because of Royol tour film
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…