Mafuta na gesi ya Russia yaendelea kwenda kwa wingi India, China na nchi za EU. Hizo za ulaya wanayanunua kwa rubles

Du! Wazungu ni watu wabaya sana. Watu wapo vitani wanadundwa kila kukicha wao badala ya kuwasaidia wanawakopesha!
wazee wa mserereko , kodi za watu zikagaiwe kwa jiran bila ridhaa ya watu ?
 
hiko ndo wengi hawaelew , tunapokosoa uvamiz hatumaanish tunamshabikia mtu fulani bali kwa utu wa kawaida tu , alichofanya Putin ni uonevu

Wengi wao si kuwa hawaelewi ila wana agenda za kidhwalimu kama Mrusi tu.

Wengi wao (si wote) ni CCM ya leo na hawataki Katiba Mpya.

Kwao neno "haki" ni sumu!
 
Nakumbuka Vita vya TZ na Uganda,Tulifunga mikanda mpaka miaka ya 2000 bao nchi yetu imeendelea kusererka kwenye umasikini na madeni.
Kisaeti ''Regime Change in Uganda'' Hatimae Nyerer alifanikiwa kumiondoa serikali ya Amin na Kuweka Kibaraka wake Obote , lakini Hali yetu kiuchumi ilikuwa Taabani sana.
Nadhani naye Mrusi ana plan ya ''Regeme change in ukrain'' kwa maslahi mapana ya usalama na uchumi a Urusi, kama Marekani alivyofanya Irak na Libya.
Hiindiyo dunia ya Maguvu na Ubabe.
Kla la Heri urusi,
Lakini nadhani Huyu Raisi wa Ukrain angelisarenda mapema kabla nchi yake haijageuzwa Jivu. akubali kuresighn na kuruhusu mrusi aweke Kibaraka mwingine watakayeendana kimkakati.
Hebu itazameni venezuela, Ilivyovurugwa na USA wakati ni matajiri wakubwa kwa kuchimba mafuta.
H ndivyo dunia ilivyo.
Wahanga ni sisi wanonge.!!!!!!!!!!!!
 
duh ila we jamaa mwongo!! ndo maana unashindwa hata kupangilia sentensi vizuri, maneno mengi hayasomeki vizuri kisa uongo, unakimbizana na keyboard ili uingie uzi mwingine ukaendelee kudanganya.... ila we jamaa muongo
 
Kuna kitu naona Kama kinawezekana,,, Russia anaweza kuuza mafuta yake kwenda EU kupitia India, yaani India ana import halafu ndio
anafanya export
 
Kumbe biashara ya kokopesha n dili sana
 
Huyu jamaa kumbe hajaacha uongo wake. Mafuta ya Urusi yanamilikiwa na Urusi kupitia kampuni Yao , ndiyo maana ana kiburi Sana na analazimisha kuuza kwa rubles. West walivyo na roho mbaya yangekuwa makampuni Yao wangeshayafunga Ili kumkomoa mrusi akose mapato.
 
Kampuni ipi?

Waliuana warusi kuuza kampuni za Serikali kwa mafisadi

Nitajie kampuni moja tu ya Urusi kubwa na wamiliki warusi wanamiliki asilimia ngapi? Mikampuni yao iko misoko ya hisa Marekani na Ulaya asilimia kubwa zinamilikiwa na matajiri wa zulaya na Marekani

Hiyo yako ni ipi? Na warusi wanamiliki asilimia. Ngapi?
 
Sibishani na wewe mtoto mdogo bishana na Chadema, Kama hujui hata kampuni ya mafuta na gesi Urusi unaandika nini?!
 
Hata huko Saudi Arabia, Arab Emirates na Nigeria makampuni mengi yanayochimba hayo mafuta yanatoka Ulaya magharibi na USA. Makampuni haya yakiwa nchi hizo za Uarabuni na Urusi hayawi wamiliki wa hayo mafuta na gesi bali yanakuwa wajasilimali tu aka vibarua tu kwenye nchi hizo. Hawana mamlaka yo yote katika umiliki wa rasilimali hiyo na wakizengua wanatimuliwa. Rasilimali hiyo inabaki kuwa ni ya hizo nchi za kiarabu na Urusi.

Ila makampuni haya yakiwa nchi za Afrika yanajimilikisha rasilimali hizi na kuwa zao. Nchi za Afrika zinanyang'anywa kabisa rasilimali hizi na kubaki zina angalia tu makampuni haya yakipora bure rasilimali hizi na hawana cha kufanya. Mfano mzuri ni nchi ya Nigeria ambayo ni ya kwanza Afrika katika uzalishaji wa mafuta haya kwenye bara la Afrika. Lakini mafuta karibu yote yanayozalishwa Nigeria hupelekwa ulaya na makampuni haya. Mafuta yanayotumika nchini Nigeria yote wanayanunua kutoka nje (import) kwa bei ya juu sana kama sisi Tanzania tusio na mafuta. Na sasa hivi Nigeria inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta haya despite serikali yao kutenga mabillion ya dola kama subsidy kwenye mafuta haya ili kupunguza kupanda kwa bei ya mafuta baada ya vita hii ya Urusi na Ukraine.

Hata sisi huku Tanzania, hii gesi yetu tulishanyang'anywa na hiyo kampuni inayoichimba huko Songosongo. Wao ndiyo wanatupangia bei na sasa hivi itakuwa inapelekwa Kenya kwa bomba.
 
Gazprom hii kampuni ni yanani?. Acha uongo we jamaa ujue we nimtu mzima, namtu mzima kudanganya sio vizuri.
 
We jamaa muongo Sana urusi wanamiliki Rasilimali zao wenyewe
 
Hili andiko linaukweli unaouma sana..
 
Kuna kitu naona Kama kinawezekana,,, Russia anaweza kuuza mafuta yake kwenda EU kupitia India, yaani India ana import halafu ndio
anafanya export
Hana haja ya kufanya hivyo. EU wanaifuata wenyewe huko Russia na kuinunua kwa rubles badala ya dola. Na muda si mrefu rubles ndiyo itakuwa sarafu ya dunia badala ya dola ya USD. Hata hiyo dola ya USD ilipata hadhi hii kupitia biashara ya mafuta, kwa jina.jingine ni petrodollar. Sasa itakuwa ni petroruble.
 

Kuna wabongo huwaambii kitu kwa USA 😁
 
Makampuni gani yanayo uza gesi ya Urusi toka Magharibi?
Labda kwa kukusaidia Gazprom, Tatneft, Lukoil, rusneft. Haya ndio makampuni makubwa ya Kirusi ya mafuta.
Lakini ukizungumzia Schlumberger, Halliburton na Wentworth haya ni makampuni yanayotoa huduma tu kwenye industry.
 
Angalia shareholders tusiende mbali na kama yako soko la hisa za kimataifa au la jibu hilo swali wako masoko ya hisa ya kimataifa au la? Jeuri ya kampuni za Urusi ilikuwa masoko ya hisa ya kimataifa

Je yanauza hisa na hisa zao au kununuliwa masoko ya hisa ya kimataifa au la ? Ndio utajua kwa nini nchi za Magharibi zimekataa kampuni zote za Urusi kushiriki soko la hisa la masoko yao sababu wanasema pesa wanazo raise masoko yao zinaondoa ku finance war machines za Urusi na kufinance vita Ukraine kuwa masoko yao hawataki kuwa part ya financing za war machines za Russia wamezipiga marufuku kushiriki masoko ya hisa nchi za Magharibi

Hisa zao zimedondoka chini hasa hakuna foreign buyers or sellers. Soko la hisa la ndani la hizo kampuni limedondoka kila mrusi anataka kuuza hisa buyers hawapo

Wauza hisa kibao wanunuzi hamna hata hamna
 
Badala ya kujibu hoja unatoka nje ya mada? Acha assumption.
Haya Soko gani la hisa kampuni za mafuta au gesi za kirusi zimelist?
Taja moja wapo tu, sio unalukaluka makida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…