Hatuna watunga sera wazuri;
Kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania; serikali inashindwa kutengeneza mazingira bora kwa wakuli wa mazao muhimu kama alizeti na chikichi kwa ajili ya uzalishani wa mafuta ya kula?
Wizara imejaa maandiko na mipango lakini hakuna utekelezaji. Kila siku ni maneno ya ''tutafanya'' na wala husikii waziri wa kilimo akisema ''tumefanya''
Tunaishi tu bila mipango endelevu.
Lakini wanasiasa hawaishi kusema kuwa tunajitosheleza.
Tumekabidhi hatma ya taifa kwa watu wasio na mipango ila wana maneno mengi mazuri.
KIla kinachotokea duniani kinaongeza ugumu wa maisha kwa mtanzania.
Si mpango wa wanasiasa huo! Huu ushenzi unaoendelea una baraka za watawala na ndio maana huwezi ona ukiisha. Ukiwa mzalendo wanakuua kwa sababu uzalendo hauendani na ufisadi.Tatizo pia serikali yetu si wezeshi linapokuja swala la kuplan kwa ajili ya muda mrefu utasikia sera sera za miaka 20 lakini hakuna cha maana.
Tuweze niche ndogo za kilimo tuwatoe wanaolima hekari chache kua wakulima wa hekari nyingi.
Si mpango wa wanasiasa huo! Huu ushenzi unaoendelea una baraka za watawala na ndio maana huwezi ona ukiisha. Ukiwa mzalendo wanakuua kwa sababu uzalendo hauendani na ufisadi.
Kinacholiponza hili taifa hakuna vipaumbele wala visionary leaders ila kuna politicians kwenye strategic positions.
Kuna billions of money za kukodisha mfumo wa kuendeshea shirika ila hakuna hela kwa ajili ya ku support kilimo kwenye taifa. Kuna billions za kusaport vitu visivyo na tija ila hakuna hela ya kufanya mambo muhimu.
Kuanzisha estate za kilimo ambazo watu watazalisha malighafi kwa ajili ya ku process mafuta na kutumia ndani ya nchi pia ku export hazimalizi hata trillion 1 ila tunaweza kuimaliza hio hela kufanyia mikutano kulipana posho na anasa za ajabu ajabu.
Na Qaswidah ...Tutaimba kwaya mwaka huu..😀
Tatizo pia serikali yetu si wezeshi linapokuja swala la kuplan kwa ajili ya muda mrefu utasikia sera sera za miaka 20 lakini hakuna cha maana.
Tuweze niche ndogo za kilimo tuwatoe wanaolima hekari chache kua wakulima wa hekari nyingi.
Kila kitu mnasema Ukraine na Russia inazalisha mbna waongo sana nyieSi mnamshabikia Putin?
Tanzania inazalisha 45%ya mahitaji yake ya mafuta ya kula na huagiza 55% toka Malaysia, India na Uturuki.
Duniani mzalishaji mkubwa wa mafuta ni Ukraine, sasa baada ya uvamizi wa Urusi, Ukraine amestop uzalisha na Rassia anaemfuatia amewekewa vikwazo hivyo mafuta ya Uturuki saivi yanaenda ulaya na ya Malaysia yanaenda Japan na Korea ili kuziba pengo la mafuta ya Urusi na Ukraine ambapo hayapo sokoni. Na Korea na Japan wananunua Bei nzuri kuliko sisi
Mungu ajalie mvua Ifike mwezi wa 4 nivune alizeti yangu ni jenge.
Mafuta sehemu nyingi tuu sio tz tu. Nilikuwa nafikiri sababu ni vita ya UkraineKuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-
Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?
Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?
Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?
Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-
Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.
Hawa Wa Ukraine na Urusi mnawasingizia, wameanza kuchapana February tu hapa, mafuta yamepanda toka mwaka jana. Mmeapata Sababu Kwa kila kitu sasa, pengine hata Nyanya zikiadimika tutaambiwa ni vita y Urusi vs Ukraine.Mafuta sehemu nyingi tuu sio tz tu. Nilikuwa nafikiri sababu ni vita ya Ukraine
Safi huyu jamaa wa Kenya atupe Bei za kwao.
Mimi jana nimenunua lita 3 kwa 21000