Dunia Putin tunamwitaji zaidi ya anavyotuhitajiSi mnamshabikia Putin?
Tanzania inazalisha 45%ya mahitaji yake ya mafuta ya kula na huagiza 55% toka Malaysia, India na Uturuki.
Duniani mzalishaji mkubwa wa mafuta ni Ukraine, sasa baada ya uvamizi wa Urusi, Ukraine amestop uzalisha na Rassia anaemfuatia amewekewa vikwazo hivyo mafuta ya Uturuki saivi yanaenda ulaya na ya Malaysia yanaenda Japan na Korea ili kuziba pengo la mafuta ya Urusi na Ukraine ambapo hayapo sokoni. Na Korea na Japan wananunua Bei nzuri kuliko sisi
Mungu ajalie mvua Ifike mwezi wa 4 nivune alizeti yangu ni jenge.
Kujibu hili kwa ufasaha inabidi niandike volumes tatu kama ukubwa wa Bible lakini nitajitahidi kwa ufupi tu kama urefu wa SMSMasoko yapo kibao, na watu wanaweza kulima sana tu.
Sera za kumzuia mtu asiuze anapotaka mazao yanapokuwa machache na auze anapotaka mazao yanapokuwa mengi inamdumaza Mkulima na kumfilisi..., Hapo Serikali ingekuwa serious ingenunua mazao yanapokuwa bei ndogo sana na kuweka kwenye hifadhi (mfano nafaka) mizigo ikipungua wanaziachia hence kubalance ile fluctuations na ulanguzi...., Pia its easier kwa serikali / wizara kutafuta masoko kuliko hata individual...kilichopo ni serikali kuwakataza kuuza nje ili bei iwe chini nchini. Matokeo yake wakulima wakubwa hawalimi na nchi inashindwa kujitosheleza.
Leo nimenunua 35000Lita 5 = Tzs 30,000/=
Uwezo wetu wa kufikiri ndio umefikia hapo, Kwamba lazima tuagize ili kifidia deficit iliyoko. Hatuwezi kuwaza nje ya box kua badala ya kuagiza tunaweza kuongeza production kwa kutumia eneo kubwa zaidi, teknolojia bora zaidi, mtaji mkubwa zaidi au vyote kwa pamoja.Tukubali kuwa sisi ni nchi ya wapumbavu. Ukubwa wa nchi yetu ni mara tatu ya Malaysia. Lakini tunategemea mafuta ya kula toka Malaysia. Tz hii alizeti inaweza kulimwa kila kona. Kama inasitawi nchi kame kama Singida basi inaweza stawi popote. Msiba wa kujitakia huu.
Nami nimenunua jana bei hii,Leo nimenunua 35000
Kama kuna kitu kinatuletea umasikini Tanzania ni BUNGE na BAADHI ya WABUNGE kwenye 100% wapo 75% no mchango/ubunifu kwa taifa! π‘Kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais na pengine yeye hajui hili. Kwa sasa huku mitaani mafuta ni adimu sana, na pale ambapo yanapatikana basi bei yake haishikiki. Dumu/Ndoo ya Lita 20 iliyokua ikiuzwa TZS 70,000/- mwezi wa sita mwaka jana leo inauzwa TZS 140,000/-
Aliekua Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipata kusema kua sababu ya kupanda huku ni kuadimika Kwa vibarua huko Malaysia sababu ya COVID-19. Kigoma inaongoza Tanzania Kwa kuzalisha chikichi, je wameweza kuchukua mazao yote yanayozalishwa pale mpaka yakaisha imebidi waagize Malaysia sasa?
Kwanini wasi encourage na ku facilitate kilimo hiki Kwa hapa Tanzania mpaka tulazimike kuagiza nje? Singida wanalima sana Alizeti, na mikoa ya kusini wanalima sana Ufuta, je mazao haya yamechukuliwa yote na bado kukawa na upungufu wa mafuta?
Haya maeneo (Singida na Mikoa ya Kusini) bado kuna mapori mengi tu, kama wanazalisha malighafi za mafuta na bado hazitoshi kwanini Serikali isiwawezeshe basi kuongeza zaidi maeneo ya kulima kwenye hayo mapori yaliyobaki ili kuongeza zaidi malighafi hizi?
Sasa kuna Hussein Bashe kwenye hii Wizara, nilidhani ni mtu Smart lakin naona nae mfumo umemmeza, amesha adopt tabia za mfumo alioko. Juzi nimemsikia akiwa mkali kweli kweli juu ya kupanda Kwa mbolea kutoka 108,000/- Kwa gunia mpaka 140,000/-, lakini nimkumbushe tu hata hiyo 108,000/- bado tunapigwa, kwani hapo kabla ilikua haizidi 60,000/-
Mafuta Sasa hayako tena mitaani, wenye vigenge/duka wanasema Kwa yalivyopanda bei hata wakiyaleta hawajui watauzaje. Mafuta yanagusa kila mtu, isije ikawa ni bomu linategwa kwenye most consumable products ili likilipuka liguse sehemu kubwa ya watu. Zama hizi za "Kazi Iendelee" tunashuhudia mfumuko mkubwa wa Bei.
Mbolea hii hii iliyopanda kutoka 60,000/- mwaka jana mpaka 140,000/- kabla ya Waziri Bashe kuirudisha mpaka 108,000???Nimejaribu kuchunguza ukuaji wa alizeti yenye mbolea na isiyo na mbolea,kunatofauti kubwa sana. Serikali isipo weka ruzuku kwenye mbolea Nchi hii haitatoka kwenye huu mkwamo. Maana Mavuno yakianza mafusadi yataikusanya yote na bei itabakia angani.
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
πππKazi iendelee...
Mama anaupiga mwingi sana...
Muacheni mama apige kazi...
Hakuna kama Samia ndani ya miezi 6 tu....
Kupata vibonzo vingine kama hivi bonyeza CM 1774858 ama Mtanzania Halisi2021
Nunua yakutosha leta mjini huku bei ya jumla 139000Kibaha..... Mafuta KORIE yamefika TSHs 106,000 Jana
Viwanda vya mafuta ya kula vya ndani vilivyopo ni vichache na walaji ni wengiKwani hapa Tanzania viwanda vya mafuta ya kula hamna?
Mpaka tuagize nje?