Magari 10 yanayonunuliwa sana na Watanzania

Ungeleta data toka tra ingekusaidia sana kusuport uzi wako ! Namba mbili weka Vits, carina TI na Noah !
 
Hizo zote ni vyombo vya usafiri barabarani tu hakuna gari ata moja
 
Which of those cars has the highest price of all ?
 
'Ka-CAG' ndo namba moja. Vimemwagwa barabarani haswa. Ukisema uvihesabu mpaka kufika tu kituoni ni 58.
 
X trail imenunuliwa mno pia
Sure watu wamenunua sana, nadhani urahisi wa bei inaweza kuwa sababu. Vyuma vimebana sana mtu anataka gari ya juu i.e. SUV , akichungulia zilizopo zinazoendana na bajeti yake anajikuta kaangukia xtrail.
 
Kluger ya 2016 ipo kati ya 27,000 to 51,000 US$ wakati Harrier ya 2016 ipo kati ya 24,000 to 36,000 US$ ,kutegemeana na muundo wa gari husika ( model) kwa hiyo utaona kuna mahali bei zinaweza kuwa sawa ila moja ikawa 4× 2 wakati nyingine ni 4×4
Ukiweza kununua gari ya mwaka 2016 hata kama ni vitz nakupa hongera!
 
Toa alpard, weka toyota wish...

Hakuna mwaka Subaru kauza magari Tanzania kama 2019..
 
Ukienda Europe hakuna gari hata moja kati ya hizo utakayoiona barabarani hapo ndo nilijua tofauti ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea

Sure..lakn hata huko europe kuna watu wana magar ya kawaida kabisa..sema wanafaidika kwa vile hawana makodi makubwa...kwa gharama unazotoa kununua lets say kluger tu,hiyo hela ukiwa nje unapata gari kali sana!!
 
Sure..lakn hata huko europe kuna watu wana magar ya kawaida kabisa..sema wanafaidika kwa vile hawana makodi makubwa...kwa gharama unazotoa kununua lets say kluger tu,hiyo hela ukiwa nje unapata gari kali sana!!
Sheria ndo zinawakaba wasimiliki magari ya kawaida. Gari iliyotengenezwa zaidi ya miaka mitano nyuma hairuhusiwi kutembea. Ina maana kwa sasa ni gari za kuanzia 2016 kuja mbele ndo zinazoruhusiwa kutembea. Hi so gari kwenye list nyingi ni za mwaka 2004 kurudi nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…