Magari binafsi yapigwe marufu kuingia Kariakoo

Mtu anaezuia maendeleo(watu kuingia Town na magari) kwa sababu ya foleni akili hana?

Tafuta solutions za kudumu, kwa sababu ukijenga parking, maendeleo yataendelea kuja, itafika point parking zitakua hazitoshi, what next
Una poor mindset kwa sababu baada ya kutoka kijijini kwenu Sitimbi hujawahi kutoka nje ya Tanzania
 
Wewe unefika New York au unaandika kwa kufikiria tu?
 
Kariakoo makazi ya watu tangu mzizima,ngumu kufukuza watu ujenge parking, parking wajenge jangwani na ilala huko
Hao watu hawakupaswa kuendelea kuishi hapo. Wajengewe flats kwingine...Kariakoo ibaki kama Soko tu
 
Fukuza machinga, Fukuza bodaboda, Fukuza bajaji, ONDOA daladala zote katikati ya mji, huwezi zuia magari mjini
 
Hawakupaswa!?..hapo kwao
Ni sawa naelewa soko limewakuta,

Lakini kwa hivi sasa Kariakoo ni soko la Kimataifa...wahamishiwe kwingine na kujengewa makazi, soko litanuliwe
Kwani wangapi walishahamishwa makwao?
 
Nazishauri mamlaka pale Kariakoo wangezuia gari zote za binafsi kuingia eneo lile. Waruhusu taxi mtandao (drop off & pick up), boda na gari za mizigo tu.

Raia wote wateja na wafanyabiashara wangetumia public transport kuingia Kariakoo.
POINT....WHY NOT?!
HAWATAKUELEWA MDAU..
 
Ni sawa naelewa soko limewakuta,

Lakini kwa hivi sasa Kariakoo ni soko la Kimataifa...wahamishiwe kwingine na kujengewa makazi, soko litanuliwe
Kwani wangapi walishahamishwa makwao?
Jengeni masoko mengine, ubungo si mmejenga!?
 
Ili kupunguza msongamano basi wangeleta system ya kuingia Kariakoo kwa kulipia kwa magari yote

Na mizigo ishushwe kuanzia saa nne mpaka saa moja asubuhi
Baada ya hapo ni kulipa tu
Hapo wengi wataacha kuingia na traffic itapungua sana

Na jiji litapata mapato ya ziada na kuboresha miundombinu mingine.

Hata kama kubadili mfumo wa sasa wa hizo barabara za hapo kariakoo na kufanya one way system
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…