Nilikuwa napanga nianzishe uzi ila kwakuwa umeanzisha ngoja nichomekee hapa hapa!
Nahisi kizazi cha baadhi ya Watanzania kwa sasa kina tatizo la kufikiri kuhusu mipango ya future ya nchi, mf mipango miji.
Achilia mbali huko Dar! Mikoani hali ya mipango miji inazidi kuwa mbaya sana kwa baadhi ya miji.
Kuna mikoa ambayo ukiwa mjini hakuna parking area maalumu. Sasa kwa miaka ijayo lazima italeta shida tu kuhusu parking!
Kwa nini baadhi ya watu wenye mamlaka hawataki kuishi kwa future? We need to live for the future and not for the current!
Hakuna namna nyingine ya kufanya kwa sasa zaidi ya kulipa fidia nyumba za watu kadhaa zinabomolewa na inajengwa parking area. Lakini cha ajabu, utakuta mahotel yanazidi kujengwa mijini na hawatengi parking area.
Huwa najiuliza, hao latra wanakusanya ushuru wa parking kwa kutumia kigezo gani wakati hawajajenga parking area baadhi ya mikoa?!
Huwa napita mkoa fulani, yaani yale maeneo ya kota za NHC, unakuta pamepangika kuanzia nyumba, soko, nyumba za ibada, parking area nk.
Pia, kotazi za railway nazo zimepangika, unakuta huduma zote muhimu zinapatikana ikiwemo viwanja vya michezo, masoko, nk.
Kupangika kwa NHC na kotazi za railway zinaonesha kabisa, wazungu wakoloni na watanzania wa kipingi cha mwl Nyerere walikuwa wanafikiri vizuri kuhusu mipango ya baadae, ila kwa sasa akili zimepararaizi kuhusu mipango miji! Tunajenga majumba mazuri bila mipango!