Kinumbo
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 3,039
- 5,560
Aisee! Wakati baadhi ya watanzania kila uchwao wakilalamika ugumu wa maisha mtaani wakati huo huo kuna baadhi ya watanzania kila uchwao wananunua magari ya kifahari na gharama kubwa mno. Kama wewe ni mkazi wa Dar es Salaam utakubaliana nami, huko barabarani kwa sasa magari ya gharama ni mengi mno.
Magari kama Land Cruiser 300 series (GX-R, ZX), Range Rover Sport, Ford Endeavour, Cadillac Escalade na mengine mengi tu. Haya magari kwa sasa yamekuwa mengi sana hapa Tanzania, ni nini siri ya watu kununua haya magari kwa wingi?
Au ndio ile kauli ya kula kutokana na urefu wa kamba yako? Ila wakuu kuna watu wana hela sio poa, kuna hiyo Ford Endeavour nyeusi namba E imenipita hapa mpaka nikaanza kujiuliza maswali kichwani.
Kipi kipo nyuma ya pazia ni madili gani hayo wenzetu wanapiga mpaka wanamiliki vyuma kama hivyo?