Magari ya kutoka China yashika soko SA


China wameanza kuunda magari yao miaka mingi sana iliyopita isipokuwa yalikuwa ni kwa matumizi ya ndani...

Wamekuwa wakifanya hivyo kwa mabasi ya abiria (long and town trips), magari ya kubeba mizigo (trucks), magari ya kijeshi n.k

Uundwaji wa magari ya kuuza nje umekuja karibuni na umechochewa zaidi wakati ambapo teknolojia ya magari ya umeme ilipoibuka na ukawa ni mpango mkakati wa kupambana na USA/Tesla...

Hizo kampuni ndogo sana unazoona zinaunda magari kwa kucopy muonekano wa magari ya kimagharibi, huwezi kukuta michezo hiyo inafanywa na Chery, BYD, Yutong, FAW n.k

Nimeandika kutokana na experience maana nimeishi China kwa muda mrefu miaka kadhaa iliyopita...
 
Watanzania sio watumiaji wa magari yanayotoka na muda tunasubiri yatumike kwa miaka mingi harafu ndio tuagize na tunaulizana mileage na kula mafuta wenzetu walishatoka huko wakiona Nchi ina magari mazuri wanawapa vibali wawauzie Raia wao haya magari huku tumeanza kuyaona yakitumika miaka kumi naa iliyopita ila mengi mpaka leo hakuna yaliyofika Tanzania na utaona tupo busy kuyaponda kwa vitu ambavyo hatuvitumii kazi kweli kweli..
 

Attachments

  • 20260303_132013.jpg
    1.3 MB · Views: 25
Hizi gari kuzagaa kwenye ardhi yetu itachukua miaka 10 ijayo wakati hapa zipo mtaani nyingi sana kama tupo Beijing.
 

Attachments

  • 20260306_151832.jpg
    976.2 KB · Views: 26
  • 20260306_151900.jpg
    1.5 MB · Views: 27
  • 20260306_151722.jpg
    1 MB · Views: 27
Magari ya kichina ni pasua kichwa nakwambia haya magari ya china yana stak barabarani baada ya muda mfupi tu hayaduku haya labad kama matymiz yako ni nyumbani na kazini lkn kikaz aisee ni heri ununue toyota used kuliko hayo ya 3yd yana goma goma sana mchina hana kitu kinachodumu kamwe.
 
Sio kweli unachoongea mkuu China wanatumia hizi gari kwao na SA zimeshika soko sana miaka mingi sasa kuna Tigo ipo sakoni sasa.
 
Yap SA ni RHD kama huku sijaona LHD..
Tanzania vitu vinachelewa sana kufika kwa sababu ya kodi kubwa ya magari watu wanabaki kumezeshana sumu kwa magari mapya na kuendelea kununua gari za mwaka 2004 tukibaki kuulizana mileage ngapi..
Kuna sedans nimeziona za Zeekr na Xpeng eti mpya chini ya $20,000 zile nazipa miaka 2-3 najua zutashuka sana.
 
Acha uwongo wa kijinga
 
Hivi hizi EVs ukinunua inabidi ujenge charging station yako home?
Hapa nimeona yapo magari ambayo unatumia cable yao ambayo unaiunga kwenye zile socket za umeme mkubwa (Jiko) vichwa vyake vipo tofauti kidogo kupata mtaalamu wa umeme ni sahihi kufanya hilo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…