'Magari ya Makonda' yakwama kukarabatiwa, mwenyewe agoma kutoa ushirikiano

Unakaribia mwezi mmoja sasa tangu msafara Ndugu Paul Makonda, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, upate ajali kule Sululu, Masasi mkoani Mtwara. Ajali hiyo iliyohusisha magari yapatayo 10, ilitokea tarehe 11 mwezi uliopita na kusababisha uharibifu wa magari kadhaa yakiwamo ya serikali.

Katika kile kinachosemwa kama kiburi na jeuri ya kimadaraka chamani, Makonda amegoma kutoa ushirikiano kufanikisha marekebisho ya magari hayo yaliyohifadhiwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA). Ushikirikiano utakiwao ni ripoti ya mkuu wa msafara juu ya ajali hiyo ambayo hadi sasa haijatolewa.

Makonda amewaambia maafisa wa kichama na kiserikali kuwa wakitaka kujua lolote wakakiulize chama kwakuwa ndicho kilichoruhusu na kuwezesha ziara yake mikoani-ikiwemo hiyo ailiyokuwa akitokea mkoani Ruvuma. Mkwamo wa matengenezo hasa unazikumba gari za serikali ambazo huhitaji ripoti kamilifu ili ziweze kutengenezwa.

Idara ambazo zinamiliki magari hayo ya serikali zilizopata ajali hiyo zinawataka maafisa wake na madereva wao waseme kwanini walikuwepo kwenye msafara huo wa kichama; hoja ambayo inapaswa kujibiwa na Makonda aliyegoma kufanya hivyo. Ripoti haijatolewa na magari hayajashughulikiwa.

Makonda, chama ni nani ili akaulizwe hata ajali yako ya Masasi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Sombetini, Arusha)

Yeye si ndiye msemaji wa Chama ...... Anaposema kiulizwe chama ana maana gani..!!? Au ni swala la Katibu kujibu.
 
Ukikutana na Afisa tawala au utumishi mkorofi anammsimamisha afisa usafirishaji na drivers kwa sababu ni kweli lazima wajibu walikua pale kwa maagizo ya nani ??
Naambiwq hata mqgizo ya makonda ya senema hayajatekelezwa hata moja …. kiutumishi hakuna na mamlaka ili mqagizo yatekelezwe ni lazima yatolewe upya na maofisa wakuu wwnye dhamana kwenye sekta
 
Back
Top Bottom