Magari ya mzungu yametuacha mbali Sana Sisi akina Toyota

Nikizisifia hizi gari huwa NINAMAANISHA
 
Kwani magari si unaagiza mwenyewe? Huko wanaponunua wazungu ukienda mtanzania wanagoma kuuza? Hakuna magari special for Tanzania, ts all about unachotaka.
 
Halafu vibarabara vyetu vinawabania wenye ndinga zao. Miundombinu haiendani kabisa na ndinga hizo za mabeberu. Acha tubaki na vibao vya mbuzi tu.
 
Kwani magari si unaagiza mwenyewe? Huko wanaponunua wazungu ukienda mtanzania wanagoma kuuza? Hakuna magari special for Tanzania, ts all about unachotaka.
Kweli unaweza kununua magari wanaponunua wazungu ukapata quality yao sababu hakuna magari special kwa Tanzania lakini mimi nazungumzia soko la ulaya,wana standard zao wameziweka ndo maana lexus( Toyota Harrier) utakayonunua ulaya na ukinunua toka japan kuja bongo zina viwango tofauti wakati mwengine mpaka majina yanakuwa tofauti kidogo.
 
Sawa ndio ni magari soko la ulaya ila mwisho wa siku ni wewe Mtanzania baada ya kushauriwa na fundi Juma mwenye uzoefu na testa yake mkononi ukaamua kununua Rav 4 massawe si ndio? Hukatazwi kununua UK version.
 
Nikizisifia hizi gari huwa NINAMAANISHA
Tumelogwa na Toyota Mkuu Ila kama mtu yeyote akiingia Kwenye Magari ya mzungu ni ngumu kumbadilisha
Upo sahihi kabisaaa
 
Mkuu Toyota ni Toyota tu na BMW ni BMW tu hata ukiendesha 1series BMW utafeel tofauti. Halafu 3 series sio luxury,ni gari ya kawaida sana. Luxury ni 7series.
Mimi sio mtaalam wa magari mkuu, kwanini Toyota anauza sana then? Sababu Top 5 ya wauza Magari Toyota anaongoza na pia Kuna Kampuni Nyengine za Ki Japan Kama Nissan na Honda.

Na ukiangalia Bei ya luxury za Toyota Na kampuni kama Ford ama BMW ni sawa ama sometime Toyota Ghali. Cruiser mpya ya 2021 ni zaidi ya 80K usd wakati kuna Ford Nyingi tu unakuta 50k. Na ni class moja.
 
Mkuu hata sijui tunaongelea nini. Ngoja nimalizie bia zangu weekend ishaanza.
 
German cars ni luxury cars. Zina premium features. Hata kuzimantain ni ghali sana. Ndo maana hata hao wazungu wenye vipato vya kawaida wanazigwaya.

Luxury version ya Toyota ni Lexus. Hata hizi wazungu wanazikimbia vilevile.

Bei ya LC200 ambayo ni top model ya toyata ni bei ya kawaida kwa models nyingi za german cars.
 
Ni same Class? Sababu Toyota Na Yeye ana Brand zake Classic/Luxury kama Rav 4, Highlander, Camry e
Kuna kitu nimeshindwa kuelewa kuhusu hizi LC 300 Toyota land cruiser kwasabb hivisasa nchi kama Dubai zinatumiwa na polisi pia hata Australia nao wapo mbioni kutumia hizi gari kama gari Doria....
Ina maana ziko vizuri Sana Kwaajili ya ualifu au wameamua kuzishusha thamani?
 
Mkuu wala usihangaike kutafuta Logic Dubai, hao Wana Hadi Lamborghini za mapolisi, hawajui kazi za KUFANYIA hela zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…