Magari ya wakuu wa mikoa na wilaya wanayaacha wakistaafu au wanaondoka nayo?

Magari ya wakuu wa mikoa na wilaya wanayaacha wakistaafu au wanaondoka nayo?

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
345
Habari,

Zile Gari za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaziacha wakistaafu au wanaondoka nazo?

Kuuliza siyo ujinga naomba majibu ya swali hilo hapo juu.
 
Zile gari baad ya kutumika kwa miaka 5 tu, hufikia expiry date hivyo wakuu wa wilaya huzichukua moja kwa moja. Tatizo ni ngumu mkuu wa wilaya kudumu kwenye wilaya moja kwa miaka 5.
 
Viongozi wengi hawajui kwanini wanatuongoza..

Disability is not inability
 
Zile gari baad ya kutumika kwa miaka 5 tu, hufikia expiry date hivyo wakuu wa wilaya huzichukua moja kwa moja. Tatizo ni ngumu mkuu wa wilaya kudumu kwenye wilaya moja kwa miaka 5.
Kwa hiyo huwa zinaenda wapi?
 
Akija mkuu wa wilaya mwingine anaagiziwa nyingine Mpya ya 400m ile used inawekwa pembeni kisha inakuja kuuzwa kwa milioni 2.
 
Zile gari zipo chini ya mkurugenzi wa halmashauri yeye ndo anampa mkuu wa wilaya na akiondoka anaiacha
Hapana, gari zile hazipo chini ya Mkurugenzi bali zipo chini ya RAS kama kiongozi mtendaji wa mkoa. Gari za Halmashauri (chini ya Mkurugenzi) usajili wake ni SM wakati za maDC na RC usajili wake unaanza na ST.. (kwa sasa ni STM).

Kinachotokea ni kuwa ma-DC bajeti yao inapokuwa finyu huwa wanaomba mafuta kutoka kwa Mkurugenzi na baadhi ya Wilaya akikuta gari lake ni bovu, basi kwa kuwa DC ndio kiongozi mkuu wa Wilaya humwagiza DED kumpa gari na ndio unakuta gari la Halmashauri lipo kwa DC au RC
 
Zile gari zipo chini ya mkurugenzi wa halmashauri yeye ndo anampa mkuu wa wilaya na akiondoka anaiacha
No no no - Wakuu wa wilaya ni sehemu ya Sekretareti ya Mkoa. Huduma zao zote za mishahara, posho, mafuta ya gari na magari huhudumiwa na Katibu Tawala wa Mkoa si Mkurugenzi.

Kuhusu gari baada ya utumishi wao huziacha kwa DAS ingawa inapotokea gari husika limemaliza muda wake anaweza kuomba kuuziwa (Kanuni ziko wazi)
 
Back
Top Bottom