Magari ya wakuu wa mikoa na wilaya wanayaacha wakistaafu au wanaondoka nayo?

Magari ya wakuu wa mikoa na wilaya wanayaacha wakistaafu au wanaondoka nayo?

Zile gari baad ya kutumika kwa miaka 5 tu, hufikia expiry date hivyo wakuu wa wilaya huzichukua moja kwa moja. Tatizo ni ngumu mkuu wa wilaya kudumu kwenye wilaya moja kwa miaka 5.
Magari ya Serikali kuu (ST) huwa yanahesabiwa thamani (value) kutoka yaliponunuliwa mpaka kufikisha miaka 5 au kufikisha kilometa laki 2, chochote kitakachowahi kufika (miaka 5 au km 200,000), hapo thamani yake inakuwa ni 0 (depreciation value).

Kwa hiyo huwa yanaondolewa kwenye daftari la mali za umma kwa njia ya mnada wa hadhara, ndio unakuta VX V8 ya mwaka 2015 inapigwa mnada leo na kuuzwa milioni 2.

Viongozi wanayoyatumia yakiwa mapya, huwa wanazingatia km, ili ikifika muda yamefika thamani 0 basi wanaomba wizarani na wanajiuzia wenyewe bila kufanya mnada.
 
Habar

Kuuliza siyo ujinga naomba majibu ya swali hilo hapo juu
Hapana, RC au DC haondoki na gari, hilo gari hubaki kama mali ya umma kwa ajili ya kiongozi anayembadili.

Hata viongozi wanaostahili kupewa magari baada ya kustaafu huwa hawaondoki na magari waliyokuwa wakiyatumia bali hununuliwa na serikali magari mapya kabisa ya muundo uleule au wa juu kidogo kwa waliokuwa wanautumia lakini kwa thamani ya fedha ya muda huo waliostaafu.
 
Hivi nikiwa mkuu wa mkoa, siwezi kuagiza gari yangu special kama ilivyokuwa kwa BASHITE?
Kwa hiyo huwa zinaenda wapi?
Zikimaliza muda wake wa kutumika Serikalini zinauzwa kwa watumiaji binafsi - so RC au DC akilihitaji huweza kutuma maombi ya kulinunua. Lkn kabla hutanguliwa na taarifa za mkaguzi na mdhibiti, mhakiki mali kn. Taarifa hizi 2 huweka uzito wa kuuziwa
 
Habari

Zile Gari za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaziacha wakistaafu au wanaondoka nazo?

Kuuliza siyo ujinga naomba majibu ya swali hilo hapo juu
RUDI SHULE mkuu hata KICHAA hawezi kuuliza UJINGA huo
 
Back
Top Bottom