Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Sitaki kujikita kwenye chanzo au sababu ya ajali, nataka hoja yangu niijenge kwenye msingi mmoja tu, USALAMA WA MAGARI WAYATUMIAYO VIONGOZI WETU.
Usalama wa chombo cha kusafiria hujumuisha mambo mengi, magurudumu, mifumo ya breki, injini, nk.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yametuletea artificial intelligence ambapo gari au chombo huwa kina kuwa na akili ya kujiuliza, kufanya hesabu na kufanya maamuzi ya jumla.
Ndio maana Kuna magari yanaweza kujiendesha yenyewe.
Back to the topic;
Hivi inakuwaje Toyota Land Cruiser viieiteee ya milioni 450 ishindwe kusoma Hali ya barabara,spidi, umbali wa vyombo vingine na Kisha kujinguza mwendo kabisa?
Kuna gari zinasoma control yako, zinasoma speed unayoendesha, zinasoma barabara na kuamua kwamba hata ukiimbiza vipi vipi haitakimbia itaishia mwendo wa kadiri tu.
Sasa haya magari ya VIONGOZI yanakosaje mifumo hiyo wakati magari kibao tu ya mtumba ya Bei poa yana hiyo mifumo?