Kuna kitu kinanishangaza kwenye ujenzi wetu. Ukiangalia hiyo picha ya daraja la Wami, utaona kuwa baada tu ya kuvuka daraja unaanza mpando na kona ya wastani kuelekea kulia na kona kali kuelekea kushoto mita kadhaa mbele.
Daraja la zamani hivyo hivyo, ukivuka tu daraja kuna mpando mkali, kona kulia kisha kushoto. Tofauti iliyopo kati ya daraja jipya na lile la zamani ni upana wa daraja jipya na kuinuliwa juu zaidi.
Najiuliza, kwa akili ya kawaida tu bila kuathiri taaluma za watu: Kwa nini hawakufikiria kutengeneza "Tunnel" iliyonyooka usawa na daraja ili iungane mbele na barabara mbele kwenye kona kali?
Kama "Tunnel ina gharama sana, kwa nini mpando usingechongwa pande mbili ili kupata barabara iliyonyooka kutoka kwenye daraja kwa kuzingatia usawa daraja lililojengwa.?
Nawaza tu kwa sauti, Wataalamu watatupa sababu kwa nini waliamua daraja liwe kama la zamani lakini jipya tu.